AFYA
   
Rudi nyumbani
................................................................................................................................. ................................................................................................................................. .................................................................................................................................
         
 
UTANGULIZI
 
 
 
Dk.
 
Mkoa wa Kilimanjaro una jumla ya watu 1,560,354 wenye umri kati ya miaka 15-49 ni 285,263 ; watoto chini ya miaka mitano 224,712 na watoto chini ya mwaka mmoja 45,280, ambao wanatumia vituo mbalimbali vya afya vipatavyo 378 vya ngazi mbalimbali zikiwemo zahanati 322,vituo vya afya 37 na hospitali 19 (zikiwemo za wilaya, mkoa, maalum ya rufaa, vituo vya afya vya watu binafsi na za mashirika ya dini) Zahanati na vituo vya afya ni pamoja na serikali, mashirika dini, mashirika ya umma na binafsi.
 
Mkoa una jumla ya watumishi wa kada mbali mbali za afya wapatao 1,676. Kati yao Madaktari Bingwa ni 3, Madaktari wa kawaida 27, madaktari wa meno 3, Famasia 10, Wauguzi 180, Matabibu 393, Madaktari Wasaidizi 65, Fundi Sanifu Maabara 27 na watumishi wengine wa kada mbali mbali.
 
Kulingana na takwimu bado kuna mapungufu ya watumishi wa kada ambali mbali 1,456.
 
DIRA(Vision)
 
Kuwa mfano wa mafanikio katika kutoa huduma za afya na ustawi wa jamii zenye ubora unaokidhi viwango na kwa uwiano ulio sawa.
 
DHIMA ( Mission )
 
Kuwezesha utoaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii ulio bora na unaokidhi viwango ili kuboresha afya za wananchi
 
MUUNDO WA MFUMO
 
Idara ya afya inafanya kazi chini ya uongozi wa mkoa (Ofisi ya RAS). Hata hivyo Wizara ya Afya inasimamia idara ya afya mikoani kwa kutengeneza na kutuma sera za afya , miongozo, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa shughuli zote kwa ujumla. Uongozi wa mkoa uko katika seksheni mbalimbali na afya iko kwenye seksheni ya huduma ya za jamii, inayosimamiwa na AA-SSS.
 
Mkoa unasimamia afya kwenye halmashauri za wilaya saba za mkoa huu ambazo ni Hai, Siha, Moshi Manispaa, Moshi vijijini, Rombo, Mwanga na Same. Zote zina Waganga wakuu wa wilaya na Kamati za Uendeshaji za Wilaya (CHMT) ambazo zina wajumbe wa kudumu 8 na wajumbe mbali mbali wa kuazimwa
 
UONGOZI WA AFYA MKOA NA WILAYA
 
Shughuli za Afya katika Mkoa zinasimamiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa akisaidiana na Kamati ya Uendeshaji ya Afya ya Mkoa. Wajumbe wa kamati hiyo wapo wa kudumu na wa kuazimwa nao ni kama wafuatao:-
 
Reginal Medical Officer. Regional Health Secretary , Reginal Health Officer, Regional Dental Officer, Regional Nursing Officer, Regional Laboratory Technologist, Regional Pharmacist, Regional Social Welfare Officer, Regional Cold Chain Officer, Regional Reproductive Child Health Coodinator, Regional Aids Control Coordinator, Regional Malaria Focal person na wengineo. Wakati Wilaya zinaongozwa na Mganga Mkuu wa wilaya na kamati za uendeshaji za wilaya (CHMT) zenye wajumbe wafuatao:- DMO. DHS, DHO, DDO, DNO, DLT, DPHARM, DSWO, DCCO, DRCHCO, DACC, DMalaria Focal person,
 
 
SHUGHULI ZA VIONGOZI WA AFYA MKOA NA WILAYA
 
•  Ufuatiliaji na usimamizi wa afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika mkoa na wilaya zote
 
•  Kusambaza sera na miongozo mbalimbali itokayo wizara ya afya na ustawi wa jamii, TAMISEMI, Utumishi NK
 
•  Kupitia mipango kabambe na bajeti ya afya CCHP za wilaya zote
 
•  kupitia taarifa za utendaji za kila robo mwaka za wolaya zote na kuzipeleka wizara ya afya / TAMISEMI
 
•  Kuitisha mikutano mbalimbali yamfano mkutano wa wafanyakazi TUGHE , RHMT/HMT ya hospitali ya mkoa , RHMT/CHMT,nk
 
•  Kuhudhuria mikutano ya mkoa mf Mock-LAAC. RCC NK
 
•  Kusimamia usambazaji wa vifaa na madawa (mf. dawa za TB na ARVS, antirabies ) pindi yapitiapo mkoani.
 
•  Kutatua kero za wafanyakazi na za wananchi pindi ziletwapo RHMT
 
•  Serviallence juu ya magonjwa ya kuambukiza kila wiki
 

HALI HALISI YA UKIMWI MKOANI KILIMANJARO

 
Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa mikoa iliyoathirika sana na janga la UKIMWI tangu ulipo gundulika mwaka 1983 hapa nchini. Aidha mkoani Kilimanjaro mgonjwa wa kwanza aligundulika Manispaa ya Moshi mnamo mwaka 1984 na kwamba hadi 2006 watu 21,476 walikwisha ripotiwa kuugua UKIMWI kote mkoani. Kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa mujibu wa utafiti wa 2003/2004 ni asilimia 7.3 hali inayoufanya mkoa wetu kukadiriwa kuwa na WAVIU wapatao 100,000.
 
Aidha inakadiriwa kwamba 40% ya makadirio ya WAVIU 100,000 sawa na watu 40,000 wanakadiriwa kuugua UKIMWI na hivyo kuhitaji huduma kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya. Pia asilimia 20 ya wanaokadiriwa kuugua UKIMWI sawa na watu 20,000, wanahitaji kuanzishiwa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs).
 
Mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI yameonyesha mwelekeo mzuri kutokana na kupungua kwa kiwango cha uambukizo toka asilimia 7.3 cha Utafiti wa mwaka 2003/04 (THIS) hadi asilimia 2 mwaka 2008 (THMIS).
 
MAFANIKIO
 
•  Vifo ya akina mama wajawazito vimepungu
 
•  Vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano vimepungua
 
•  Previlence ya maambukizi ya UKIMWI imeteremka
 
•  Ukarabati mbalimbali
 
•  Usambazaji huduma za kuzuia maabukizi ya mama kwenda kwa mtoto PMTCT
 
•  Vituo vya kutolea huduma za dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (CTC) zimeongezeka kwa sasa ziko 40 na zimefikia vituo vya afya na zahanati.
 
•  Kuanzisha huduma za kubaini maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda mtoto mapema kwa kutumia DNA-PCR katika hospitali ya KCMC na hospitali ya mkoa ya Mawenzi . (Early infant diagnosis)
 
 
CHANGAMOTO
 
•  Upungufu wa wafanya kazi wilaya zote pamoja na hospitali ya mkoa
 
•  Upungufu wa magari kwenye hospitali ya mkoa, ofisi ya RMO, baadhi ya Ofisiza Ma DMO, vituo vya afya
 
•  Uchakavu wa miundombinu
 

•  Upungufu wa baadhi ya dawa, vitendanishi na vifaa tiba katika mkoa

 
MATARAJIO (WAY FORWARD)
 
•  Kuendelea kuboresha huduma mbalimbali za afya katika mkoa
 
•  Kuendelea kupunguza maabukizi ya VVU
 
•  Kuendelea kupunguza vifo vya mama na mtoto
 
•  Kuendelea kuboresha miundombinu katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya ili kuzingatia sera ya afya ya nchi (MMAM)
 
•  Kuendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa afya ilii kukidhi mahitaji ya watumishi
 
•  Kuanza mchakato wa kuunda bodi ya afya ya hospitali ya mkoa
 
Hitimisho
 
Lengo letu liwe ni kutoa Afya bora kwa watu wote
 
BONYEZA HAPA KUSOMA TAARIFA FUPI YA HOSPITALI YA MKOA - MAWENZI
         
Rudi juu   Rudi juu   Rudi juu
 
.........................................................................................................................................................................................................................................................................................
 
COPYRIGHT© OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, S.L.P 3070, SIMU: 027 2752184/54236-7, FAX: 027-2753248. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.