SERIKALI YA MKOA WA KILIMANJARO YALETA MATUMAINI MAPYA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI.
           
       
   
     
     
......................................................................................................................................................................................................................................................................................
     
     
     
Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla wanatarijia kupata manufaa makubwa yanayotokana na bidhaa za kilimo
 
 
PICHANI : Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro.( Picha na Shaban Pazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
 
 
Matumaini hayo yameanza kuonekana baada ya uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kutiliana saini na Benki ya Uwekezaji Tanzania TIB mkubaliano ya mkopo wenye thamani shilingi bilioni kumi za kitanznia kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la mazao ya kilimo.
 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Faisal H. Issa kwa niaba ya serikali aliwekeana saini makubaliano ya mkopo wa kiasi hicho na Allan Magoma ambaye ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la bidhaa za nafaka na mbogamboga linalotarajiwa kujengwa katika eneo la Lokolova katika Halmashauri ya Moshi vijijini.Akizungumza baada ya kushuhudia shughuli ya uwekaji saini Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama alisema upatikaji wa soko hilo la kisasa litasaidia wananchi kuongeza kipato kitakachowawezesha kujikimu kimaisha na kuongeza pato la mkoa na taifa kwa ujumla.
 
Akitoa mfano wa mafanikio yaliyopatikana katika soko la muda lililopo katika kijiji cha Himo katika Halmashauri ya Moshi, Mhe. Gama amesema katika kipindi kilichoanzia mwezi wa tatu mwaka huu hadi mwezi wa saba kiasi cha tani 26,585 za nafaka zimeweza kusafirishwa nje ya nchi. Kuhusu mapato Mheshimiwa Gama amesema tangu kuanzishwa kwa soko hilo mwezi wa tatu mwaka huu,Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia Kodi ya Barabara imeweza kukusanya kiasi cha Dola za Kimarekani Elfu thelasini na sabini na mbili (30,072)
 
 
 
Aidha katika kipindi hicho, Mheshimiwa Gama amesema Halmashauri ya Moshi imeingiza jumla Shilingi za kitanzania milioni themanini( 80,000,000/=) huku Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ikiingiza jumla ya shilingi za kitanzania milioni ishirini na moja, laki moja na sabini na sita ( 21,10076) Mheshimiwa Gama ameongeza kuwa Serikali ya Kijiji cha Himo imeingiza zaidi ya ya shilingi za kitanznia milioni ishirini na tano (25,000,000/=) Naye Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe. Samwel Sitta ambaye alishuhudia uwekeji saini huo alitoa pongezi kwa Benki ya TIB na Uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa Mkoa Mh. Gama kwa kutafuta ufumbuzi wa kero za kiuchumi zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa umla kwa vitendo.
 
Amesema wakulima na wafugaji wa kitanzania wamekua wakiuza mazao yao kwa bei ambayo haina maslahi kwao kutokana na utaratibu waliokuwa wakiutumia wa kupeleka mazao yao nje ya nchi hali inayofanya wanunuzi kununua bidhaa hizo kwa bei wanayoipanga wao bila kujali maslahi ya watanzania.Mheshimiwa Sitta ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa ujumla kila mmoja kwa kipaji na uwezo wake kujipanga na kujidhatiti kutafuta namna ya kutumia vizuri fursa hii.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
rudi nyuma
     
© 2013 OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, S.L.P 3070, SIMU: 027 2752184/54236-7, FAX: 027-2753248   Rudi juu