KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA SEKRETARIETI YA MKOA WA KILIMANJARO NA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI SEPTEMBA, 2014
           
       
   
     
     
......................................................................................................................................................................................................................................................................................
     
     
     
Mh. Balozi Ombeni Sefue amewakumbusha watumishi kujipima wao wenyewe mara wanapotoa huduma kwa wananchi ni kwa kiasi gani huduma hiyo imemfaa na kuwaridhsha wananchi. Aidha balozi sefue amewataka watumishi kutoingiza siasa katika utumishi kwani kufanya hivyo kunaweza kumfanya mtumishi kutoto huduma kwa kutozingatia haki na usawa kwa wananchi wote kwani wananchi wana itikadi tofauti za kisiasa.
 
 
PICHANI : MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO( Picha&Stori na Shaban Pazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
 
 
Balozi Sefue amewataka watumishi wote wa umma kuzijua na kuzifuata sheria na taraibu za utumishi ili waweze kufanya kazi zao kwa uaminifu na uadilifu ili wawewze kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.
 

Utumishi wa Umma unaongozwa na Sheria ,Kanununi na Sera. Viongozi lazima mzijue vizuri na watumishi wa chini yenu wanatakiwa wazijue Alifafanua Balozi Sefue.

 
Mbali na hilo Balozi Sefue amewaagiza viongozi wenye majukumu ya kusimamia nidhamu kwa watumishi umma wafanye kazi hiyo ipasavyo ili watumishi wanaokwenda kinyume warudishwe kwenye mstari..
 
 
 

Aidha Balozi Sefue amewakumbusha watumishi wa umma kuwa wanawajibu wa kuwakumbusha wananchi kutii sheria.

 

For Qns or additionals please consult ICT Unit.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
rudi nyuma
     
© 2013 OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, S.L.P 3070, SIMU: 027 2752184/54236-7, FAX: 027-2753248   Rudi juu