TAARIFA YA WILAYA YA HAI KWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA MIZENGO PETER KAYANZA PINDA [MB]  TAREHE 22/10/2008

 

 

 

1.0.1  ENEO LA WILAYA

Wilaya ina ukubwa wa kilometa za mraba 1,011 sawa na Hekta 101,100.

 

1.0. 2  IDADI YA WATU

Kwa mujibu wa Sensa ya Kitaifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, Wilaya ilikuwa na wakazi wapatao 167,097.  Wanaume 82,053 na wanawake 85,044. Kwa maoteo ya  ukuaji wa asilimia 1.9 kwa mwaka (projection), idadi ya watu kwa mwaka 2008, inakisiwa kuwa 183,712 kwa mgawanyo wa  wanaume 90,214 na wanawake 93,498.  Kwa wastani msongamano wa watu kiwilaya katika kilometa 1 ya mraba ni kati ya watu 182 ukanda wa tambarare na hufikia hadi 700  katika Ukanda wa Juu.

 

1.0.3 DIRA NA MWELEKEO

 

Katika miaka kumi ijayo Halmashauri ya Wilaya ya Hai ichangie juhudi za kuondo umaskini kwa kutoa huduma bora, endelevu na shirirkishi kwa kuzingatia utawala wa sheria na usawa wa kijinsia kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuwajibika kwa jamii.

 

 

 

 

LENGO KUU

Lengo kuu ni kuwa katika kipindi cha miaka mitatu halmashauri ya Wilaya ya Hai iboreshe huduma zitolewazo za kiuchumi na kijamii kwa wastani wa asilimia kumi.

1.0.4 HALI YA HEWA

Wilaya imegawanyika katika Kanda Kuu tatu (3) za kijiografia ambazo ni;

 

      i.     Ukanda wa Tambarare

Ukanda huu uko chini ya meta 900 juu ya usawa wa bahari.  Hupata mvua za wastani wa  kiasi cha mm. 700 kwa mwaka.  Hali ya hewa ni ya joto wakati wa kiangazi.

 

    ii.     Ukanda wa Kati

Uko kati ya meta 900 – 1,660 juu ya usawa wa bahari.  Mvua ni za wastani wa kiasi cha mm. 750 – 1,250 kwa mwaka.  Hali ya hewa ni ya vuguvugu wakati wa kiangazi.

 

  iii.     Ukanda wa Juu

Uko juu ya meta 1,700 juu ya usawa wa bahari.  Mvua ni za wastani wa kiasi kati ya mm. 1,250 – 1,750 kwa mwaka na muda mwingi ukanda huu ni wa baridi.

 

MATUMIZI YA ARDHI

Matumizi ya ardhi ya Wilaya hii, yamegawanyika katika sehemu kuu nne, kama ifuatavyo;

1.      Hekta 46,506 (46%) zinafaa kwa kilimo

2.      Hekta 14,154 (14%) ni eneo la misitu

3.      Hekta 13,143 (13%) ni eneo la miamba na

Hekta 27,297 (27%) ni eneo lifaalo kwa malisho ya mifugo.

 

1.0.5  HALI YA UCHUMI

Wastani wa pato la mkazi wa Wilaya hii kwa mwaka 2005/2006 kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2005, lilikadiriwa kuwa Tshs. 385,000/= kwa mwaka.  Hii ikiwa ni sawa na Tshs. 32,000/= kwa mwezi. Hali hii ilisababishwa na kufululiza kwa vipindi vya ukame, kuanguka kwa bei na kupungua kwa ubora na wingi wa zao la kahawa ambalo ndilo zao kuu la biashara kwa wenyeji wa Wilaya hii. Kwa mwaka 2006/2007 pato la mkazi wa Wilaya ya Hai linakadiriwa kuwa ni Shs. 450,000/= hii ni sawa na pato la Shs. 37,500/= kwa mwezi (Chanzo: Takwimu za CSPD Januari – 2007)  

 

UCHUMI WA HALMASHAURI

 

Idara ya Fedha na Biashara ni mojawapo ya Idara nane (8) za Halmashauri ya Wilaya ya Hai kwa mujibu wa maboresho ya serikali za Mitaa na ndiyo yenye jukumu kubwa katika ukusanyaji wa mapato.

 

Idara ya Fedha na Biashara imegawanywa katika sehemu Kuu tano (5) ili kurahisisha utendaji na utakelezaji  wa majukumu yake.

 

Sehemu hizo ni kama ifuatavyo:-

(i)                 Mapato

(ii)               Matumizi

(iii)             Mishahara

(iv)              Hesabu za Mwisho

(v)                Biashara

 

Majukumu ya Idara ya Fedha na biashara ni kama  yafuatavyo:-

(i)                 Kuhakikisha, kanuni, taratibu za fedha  mbalimbali inayotolewa na Serikali inafuatwa na kutekelezwa.

(ii)               Kuandaa Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara na kusimamia utekelezaji wake.

(iii)             Kuandaa taarifa mbalimbali za fedha kulingana na miongozo na mahitaji ya Halmashauri , Wizara ya fedha na Wizara ya Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa.

(iv)              Kuandaa  Mahesabu ya kila mwisho wa mwaka  wa Fedha.

(v)                Kujibu hoja za Mdhibiti Mkuu wa Mahesabu ya Serikali

(vi)              Kuandaa mahesabu kwa ajili ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)

 

Mafanikio ya Idara ya Fedha na biashara ni kama  yafuatavyo:-

 • Katika kipindi cha miaka ya Fedha ya  2006/2007, 2007/2008 na 200/2009 ( hadi 30/09/2008) Idara ya Fedha na Biashara iliweza kuandaa kila mwezi taarifa za Mapato na Matumizi ambazo zilijadiliwa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kwa mujibu wa  kanuni za uendeshaji wa Halmashauri..
 • Katika vipindi tajwa hapo juu Idara iliandaa taarifa zote za Robo mwaka na kuziwasilisha TAMISEMI, HAZINA na Ofisi ya Katibu  Tawala Mkoa wa Kilimanjaro kwa wakati.
 • Katika mwaka wa Fedha wa  2006/2007 na 2007/2008,  tulifunga mahesabu  na kuyawasilisha kwa Mkaguzi  na Mdhibiti wa Serikali kabla ya tarehe 30 Septemba ya baada ya kumalizika kwa mwaka wa fedha husika. Chini ya usimamizi wa Idara ya Fedha tuliweza kupata Hati Safi mfululizo kuanzia mwaka  2005/2006.  Kwa mwaka wa 2006/2007 mahesabu yako kwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi.

 

 • Idara ya Fedha  inaratibu  maandalizi ya hesabu kwa ajili ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na kuziwasilisha kwenye Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa

 

 •  Idara ya Fedha na Biashara wakishirikana na Idara nyingine tumeweza kukidhi vigezo vilivyowekwa ili kupata Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo na kujengea Uwezo kwa mwaka 2005/2006, 2006/2007 na 2007/2008.

 

 

TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA KIPINDI CHA 2006/2007, 2007/2008 NA 2008/2009

 

Idara ya fedha na bishara katika ukusanyaji wa mapato ya halmashauri imeweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2006/2007 ilikusanya asilimia 83.03 na mwaka 2007/2008 kuvuka lengo la bajeti kw asilimia 101.22. Mafanikio yametokana na kushirikiano wa wakuu wa idara na waheshimiwa madiwani kwa kuwashawishi wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi za serikali ka ujumla wanapokuwa katika mikutano katika kata zao.

 

Idara ya fedha na biashara kwa upande wa matumizi kwa kipindi cha mwaka 2006/2007, 2007/2008 na 2008/2009 imeendelea kufanya matumizi kwa mujibu wa kanuni na tartatibu za fedha na miongozo kutoka serikalini na kwa wahisani mbalimbali.

 

Yafuatayo ni majedwali yanayoonyesha mapato na matumizi kwa vipindi vya 2006/2007, 2007/2008 na 2008/2009 kama ifuayavyo :-

 

Mapato

2006/2007

 

 

 

Maelezo

Makisio

Halisi

Asilimia

Mapato ya Halmashauri

353,289,200.00

293,351,783.92

83.03

Ruzuku(GPG)

144,000,000.00

119,795,563.45

83.19

Ruzuku Mbalimbali

8,293,000,000.00

8,548,366,023.51

103.08

Wahisani Mbalimbali

3,030,878,200.00

2,082,788,145.88

68.72

Jumla

11,821,167,400.00

11,044,301,516.76

93.43

Matumizi

2006/2007

 

 

 

Maelezo

Makisio

Halisi

Asilimia

Mapato ya Halmashauri

353,289,200.00

249,334,578.77

70.58

Ruzuku(GPG)

144,000,000.00

133,580,371.13

92.76

Ruzuku Mbalimbali

8,293,000,000.00

8,397,866,108.86

101.26

Wahisani Mbalimbali

3,030,878,200.00

1,530,850,455.99

50.51

Jumla

11,821,167,400.00

10,311,631,514.75

87.23

 

 

 

 

 

 

 

Mapato

2007/2008

 

 

 

Maelezo

Makisio

Halisi

Asilimia

Mapato ya Halmashauri

315,495,817.00

319,342,124.55

101.22

Ruzuku(GPG)

187,845,000.00

133,249,608.56

70.94

Ruzuku Mbalimbali

11,350,969,596.11

10,588,324,495.91

93.28

Wahisani Mbalimbali

1,542,292,632.00

934,079,774.47

60.56

Jumla

13,396,603,045.11

11,974,996,003.49

89.39

 

Matumizi

2007/2008

 

 

 

Maelezo

Makisio

Halisi

Asilimia

Mapato ya Halmashauri

315,495,817.00

300,342,124.55

95.20

Ruzuku(GPG)

187,845,000.00

130,249,608.56

69.34

Ruzuku Mbalimbali

11,350,969,596.11

10,646,999,393.42

93.80

Wahisani Mbalimbali

1,542,292,632.00

994,079,774.47

64.45

Jumla

13,396,603,045.11

12,071,670,901.00

90.11

 

Mapato

2008/2009

 

 

 

Maelezo

Makisio

Halisi

(Hadi 30/09/2008)

Asilimia

Mapato ya Halmashauri

342,016,157.00

68,624,368.74

20.06

Ruzuku(GPG)

150,816,000.00

23,268,212.50

15.43

Ruzuku Mbalimbali

8,228,083,947.00

1,223,915,040.67

91.68

Wahisani Mbalimbali

1,334,951,880.12

415,142,461.00

4.13

Jumla

10,055,867,984.24

1,730,950,082.91

17.21

 Matumizi

2008/2009

 

 

 

Maelezo

Makisio

Halisi

(Hadi 30/09/2008)

Asilimia

Mapato ya Halmashauri

342,016,157.00

54,899,494.99

16.05

Ruzuku(GPG)

150,816,000.00

20,941,391.25

13.89

Ruzuku Mbalimbali

8,228,083,947.00

1,221,500,475.30

14.85

Wahisani Mbalimbali

1,334,951,880.12

373,628,214.90

27.99

Jumla

10,055,867,984.24

1,670,969,576.44

16.62

MAFANIKIO

Halmashauri imekuwa ikivuka Malengo yake ya ukusanyaji wa Mapato ya kutoka vyanzo vyake iliyojiwekea kila Mwaka.

 

CHANGAMOTO

1.      Kumekuwa na uelewa potofu kwa walipa ushuru kuhusu kodi na shuru     mbalimbali ambazo zimefutwa na wanazostahili kuzilipa.

2.      Hali ya ukame iliyoikumba Nchi nzima hivyo kusababisha uzalishaji wa Kahawa kushuka sambamba na ushuru wa kahawa.

3.       Vyanzo muhimu vya Mapato vimepungua kutokana na kugawanyika kwa Wilaya ya Siha.

 

Mwelekeo kwa mwaka 2008/2009

Katika mwaka wa fedha 2008/2009 tunatarajia kukusanya jumla ya Tshs 10,055,867,984.24 na tunatarajia kufikia lengo katika ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kama inavyoonekana hadi kufikia tarehe 30/09/2008 tumeweza kukusanya asilimia 20% ya makisio kwa mwaka 2008/2009.

 

Kwa upande wa matumizi tutaendelea kufanya matumizi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za fedha na miongozo mbalimbali.

 

MAPATO YA SERIKALI KUU (TRA)

Taarifa ya makusanyo ya kodi ya Wilaya Hai/Siha kwa mwaka wa fedha 2005/2006 hadi nusu mwaka wa fedha [2007/2008 Julai – Desemba 2007]. Wilaya ya Hai kwa ujumla imekuwa ikivuka lengo la Ukusanyaji Kodi kila Mwaka kutokana hii imetokana na sababu zifuatazo;- 

 

o       Kupanuka kwa wigo wa walipa Kodi [Tax Base], hili limechangiwa zaidi kutokana na kugawanywa maeneo ya Wilaya katika Blocks (Blocks Management).

 

o       Elimu ambayo imetolewa kwa Walipa Kodi kwa njia ya kuwatembelea sehemu zao za Kazi.

 

o       Kuanzishwa kwa Kamati za Kodi za Wilaya [District Tax Advisory Committees] ambazo zimekuwa chini ya Uenyekiti wa Mkuu wa Wilaya ambapo Katibu wake ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato wa Wilaya kwa mujibu wa sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 kifungu namba 129.

 

o       Kukua kwa Miji ya Bomang’ombe na Sanya Juu

 

Kwa ujumla Wilaya imekuwa ikivuka malengo yake Mwaka hadi Mwaka, kwa mfano katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2005/2006 Makusanyo yalikuwa Tshs 728,226,964.92 dhidi ya lengo la Tshs 518,466,454.00 hivyo kuvuka lengo kwa asilimia 140.46%. Katika kipindi cha Mwaka 2006/2007 jumla ya Tshs 1,845,242,589.53 zilikusanywa dhidi ya lengo la Tshs 1,258,598,134.00 hivyo kuvuka lengo kwa asilimia 146.61%. Na katika Kipindi cha 2007/2008 kuanzia Julai – Desemba jumla ya Tshs 1,845,242,589.53 zilikusanywa dhidi ya Tshs 1,258,598,134.00 zilizolengwa na hivyo kuvuka lengo kwa asilimia 101.39 kama inavyojidhihirisha kwenye Majedwali chini.

 

 

 

 

 

MWAKA WA FEDHA 2005/2006

MWEZI

LENGO KWA MWEZI

MAKUSANYO HALISI

ASILIMIA

Julai 05

22,037,226.00

25,028,938.42

113.58%

August 05

19,256,874.00

42,832,907.13

222.43%

Sept 05

52,378,362.00

63,361,306.06

120.97%

Oct 05

25,817,529.00

36,557,499.93

141.60%

Nov 05

34,008,239.00

42,078,000.86

123.73%

Dec 05

55,196,597.00

58,758,943.81

106.45%

Jan 06

38,754,581.00

42,429,901.05

109.48%

Feb 06

54,021,666.00

56,445,636.57

104.49%

March 06

84,194,274.00

173,005,445.26

205.48%

April 06

39,089,750.00

51,226,011.72

131.05%

May 06

47,204,981.00

55,459,158.50

117.45%

June 06

46,506,375.00

81,043,215.61

174.26%

JUMLA

518,466,454.00

728,226,964.92

140.46%

 

MWAKA WA FEDHA 2006/2007

MWEZI

LENGO KWA MWEZI

MAKUSANYO HALISI

ASILIMIA

Julai 06

51,513,623.00

66,833,131.44

129.74%

August 06

65,631,623.00

83,104,137.08

126.62%

Sept 06

75,299,320.00

155,015,682.28

205.87%

Oct 06

53,826,870.00

71,751,066.48

133.30%

Nov 06

53,518,490.00

79,595,372,40

148.72%

Dec 06

66,152,580.00

185,243,831.07

280.03%

Jan 07

51,969,520.00

83,281,584.71

160.25%

Feb 07

63,271,610.00

112,801,646.64

178.28%

March 07

301,599,310.00

340,726,041.90

112.97%

April 07

191,273,509.00

245,128,842.84

128.16%

May 07

60,842,761.00

103,951,897.28

170.85%

June 07

223,698,857.00

317,809,355.41

142.07%

JUMLA

1,258,598,134.00

1,845,242,589.53

146.61%

 

MWAKA WA FEDHA 2007/2008 [JULY 2007 – DESEMBA 2007]

 

MWEZI

LENGO KWA MWEZI

MAKUSANYO HALISI

ASILIMIA

Julai 07

155,195,592.00

148,078,298.49

95.41%

August 07

187,816,596.00

149,614,141.32

79.66%

Sept 07

241,717,847.00

339,760,329.46

140.56%

Oct 07

185,281,367.00

98,118,298.67

52.96%

Nov 07

182,801,373.00

103,466,533.63

56.60%

Dec 07

270,461,254.00

401,194,856.38

148.34%

JUMLA

1,258,598,134.00

1,845,242,589.53

101.39

 

 1.1 UTAWALA

 

Kiutawala, Wilaya ina Tarafa 3 (Lyamungo, Machame na Masama) Kata 10, Vijiji 55 na Vitongoji 260.

 

Wilaya ina Jimbo moja la uchaguzi. Katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2005 vyama vitano vya siasa vilishiriki navyo ni; CCM, CHADEMA, TLP, CUF na SAU. Chama kilichoshinda uchaguzi ni CCM kwa kumpata Mbunge Mheshimiwa Fuya . G. Kimbita.

Pia katika uchaguzi huo tuliwapata Madiwani wa kuchaguliwa 8 kutoka chama cha Mapinduzi na 2 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Aidha wapo madiwani wa viti maalum wanawake 4 kutoka CCM na 1 kutoka CHADEMA.

 

1.1.1 HALI YA ULINZI NA USALAMA

Hali ya ulinzi na usalama ni shwari kwa ujumla.  Wananchi wanaendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii bila kujali tofauti zao za kidini, itikadi, kabila wala rangi.

 

Changamoto zinazoikabili wilaya katika ulinzi na usalama ni:

1.      Uthibiti wa mivutano ya wakulima na wafugaji ambao hutokea katika vijiji vya Mungushi, Kware, Rundugai, Chekimaji, Chemka na Kawaya.

2.      Uthibiti wa matukio ya ujambazi

3.      Uhamasishaji wa wananchi kuhifadhi chakula cha kutosha kwa kila kaya

4.      Ufumbuzi wa migogo ya mashamba na mipaka yake.

 

 

1.1.2 HALI YA KISIASA

 

Wilaya ya Hai ina Jimbo moja la Uchaguzi. Katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2005 vyama vitano vya siasa vilishiriki navyo ni CCM, CHADEMA, TLP, CUF na  SAU. Chama kilichoshinda uchaguzi ni CCM kwa kumpata Mbunge Mheshimiwa Fuya G. Kimbita. Kwa ujumla hali ya kisiasa katika Wilaya yetu ni shwari pamoja na mchanganyiko wa vyama tulionao, kwani tuna Kata kumi kati ya kata hizo tuna jumla ya madiwani nane wa kuchaguliwa kutoka CCM na wawili kutoka CHADEMA. Madiwani wa kuteuliwa tunao wanne kutoka CCM na mmoja kutoka CHADEMA ambao kwa ujumla wao pamoja na Mbunge wanakuwa kumi na sita ambao wanaunda Baraza la Madiwani.

 

 

 

 

 

 

2.0     UTEKELEZAJI WA MKUKUTA NA ILANI YA UCHAGUZI 2005

2.1     MALENGO, MAFANIKIO NA CHANGAMOTO 2006/2007

2.1.1  UKUAJI WA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI WA KIPATO

 

2.1.1.1 KILIMO/MIFUGO 2006/2007:

 

Katika wilaya ya Hai kuna hekta 46,506 zinazofaa kwa kilimo. Wilaya ina watu 183,712 ambao wanahitaji tani 50,291.16 za wanga na tani 5,029.11  za utomwili. Kutokana na uzalishaji wa tani 183,760 za wanga na tani 18,376 za utomwili zilizozalishwa 2005/2006 wilaya ilikuwa na chakula cha kutosha.

 

Katika mwaka wa 2006/2007 Halmashauri ilipata TSh. 15,998,400 kwa matumizi ya kawaida na TSh. 1,109,044,480 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kujenga uwezo wa wadau mbalimbali.

 

MALENGO:

i)Mwaka 2006/2007 Halmashauri ililenga kulima jumla ya hekta 58,749  za mazao ya chakula kwa misimu ya masika, vuli na umwagiliaji na kuzalisha jumla ya tani 239,350 za mavuno.

ii)Kuendelea kutunza hekta 12,655 za  kahawa  na kuzalisha tani1,800.

iii)Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji

iv)Kuongeza tija katika mazao ya chakula na biashara

v)Kuwajengea uwezo wadau mbalilmbali wa sekta ya kilimo na mifugo

 

UTEKELEZAJI:

i)Jumla ya hekta 62,930 za mazao ya chakula zililimwa katika misimu ya masika, vuli na umwagiliaji na kuvuna tani 172,512 za chakula

 

ii)Jumla ya hekta 12,655 za kahawa ziliendelea kutunzwa na kuzalisha tani 1,543.9

 

iii)Mifereji 13 ya umwagiliaji yenye thamani ya TSh. 498,098,730 ilikarabatiwa na

kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 3,120 hadi 4,215. Kumekuwa na ongezeko la uzalishaji kahawa, ndizi, mahindi mpunga, maharage, mbogamboga na hatimaye ongezeko la kipato kwa mkulima

 

iv)Miradi 9  ya ngo’ombe wa maziwa yenye thamani ya TSh. 258,750,000/= ilitekelezwa. Uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita 5 hadi lita 8 kwa ng’ombe kwa siku

 

 • Mmiradi 3 ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa yenye thamani ya TSh. 7,999,200 ilitekelezwa. Uzalishaji wa maziwa umeongezeka toka lita 0.5 hadi lita 2 kwa siku

 

 • Miradi 8 ya ufugaji wa kuku yenye thamani ya TSh. 13,338,000/= ilitekelezwa .Utagaji mayai umeongezeka toka mayai 50 hadi 80  kwa kuku kwa mwaka

 

 • Miradi 15 ya kilimo bora cha mahindi, maharahe, alizeti na ngwara yenye thamani ya TSh. 49,500,000/= ilitekelezwa. Uzalishaji wa mahindi umeongezeka kutoka tani 1.5 hadi tani 3.5 kwa hekta

 

 • Miradi 5  ya kilimo bora cha mboga mboga yenye thamani ya TSh. 13,365,000/= ilitekelezwa. Uzalishaji wa mbogamboga umeongezeka kutoka tani 3 hadi tani 5 kwa hekta

 

 • Miradi 5 yenye lengo la kuboresha afya ya mifugo na masoko ya mifugo yenye thamani ya TSh. 37,739,159 ilitekelezwa. Vifo vya mifugo vinavyotokana na magonjwa yaenezwayo na kupe vimepungua kwa 40 %

 

 • Mashamba darasa  2 yenye thamani ya TSh. 2,000,000/= yalianzishwa.

Wakulima 285 wameitikia kilimo cha mazao yanayostahimili ukame mfano   mihogo na ngwara.

 

 • Kuendeleza kilimo cha kahawa – Miradi ya kilimo bora cha kahawa 16 yenye thamani ya TSh. 34,753,191 ilitekelezwa.

Uzalishaji wa kahawa umeongezeka kutoka tani 1,300 mwaka wa 2005/2006  hadi tani 1,543.9 mwaka 2006/2007

 

v)Warsha za utambulisho wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP) ziliendeshwa  kwa viongozi, watendaji na wadau wengine wa kilimo, pia mafunzo kwa wagani yalitolewa na vitendea kazi vilinunuliwa kwa gharama ya TSh. 29,748,000/=.

 

 • Uibuaiji wa miradi ya kilimo/mifugo ulifanyika kuanzia ngazi ya vijiji.
 • Jumla ya wakulima 25,000 walipatiwa ushauri wa kilimo na ufugaji bora.

 

 • Pembejeo zenye ruzuku:

Mahitaji ya wilaya yalikuwa tani 6,300 za aina mbalimbali za mbolea na tani 542    za aina mbalimbali za mbegu. Wilaya ilipata tani 2,087.4 za mbolea na tani 195 za mbegu zenye ruzuku na kuzisambaza kwa wakulima kupitia mawakala 22.

 

Mahitaji ya dawa za kuogesha mifugo aina mbalimbali yalikuwa lita 6,000. Wilaya ilipata lita 502 za dawa aina ya granade na kutumika kwenye majosho 2 na wafugaji 15 wanaotumia mabomba ya mikono.

 

 • Katika kupambana na baa la panya serikali ilitoa Kg 72  za dawa aina ya “ Zinc Phosphide” iliyotumiwa na wakulima katika hekta 2,210 tu (sawa na 40% ) ya eneo lililoathirika la hekta 5,520.
 • Katika jitihada za kuutokomeza ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF) serikali ilitoa dozi 125,000  za dawa ambayo ilitumika kuchanja ng’ombe 57,549 mbuzi na kondoo 61,438 na ngamia 35.

 

Changamoto:

 • Kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi na pembejeo
 • Bei ndogo ya mazao kwa wakulima hususan kahawa
 • Magonjwa katika mazao na mifugo mfano chulebuni na kutu ya majani, na homa ya bonde la ufa katika mifugo
 • Ukame ambao ulisababisha vijiji 16 vya ukanda wa tambarare kukumbwa na upungufu wa chakula
 • Baa la panya
 • Wakulima kupenda kuuza chakula nje ya nchi ambako bei ni nzuri.
 • Pembejeo zenye ruzuku zilipatikana kwa msimu wa masika tu, hivyo wakulima wa umwagiliaji hawakupata pembejeo za ruzuku

 

 

2.1.1.2 VIWANDA NA BIASHARA 2006/2007

 

 VIWANDA

Kwa ujumla Wilaya yetu imekuwa na kiwanda kimoja kikubwa cha ‘Tanzania Machine Tools’ ambacho kilikuwa kinatengeneza zana za kilimo na vipuri vya mashine, kiwanda hicho hakifanyi kazi yake sawasawa kwa sasa kwa kuwa kipo chini ya PSRC bado kinatafutiwa mwekezaji.

 

MALENGO

Katika utekelezaji wa MKUKUTA na Ilani ya Uchaguzi kama inavyotuelekeza katika ukurasa wa 36 Ibara ya 36, Wilaya ya Hai ililenga kuhamasisha jamii na vikundi waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao

 

UTEKELEZAJI

Sekta ya Biashara kwa kushirikiana na idara ya Maendeleo ya jamii ilitoa mafunzo kwa vikundi ishirini vya wajasiriamali ili viweze kupatiwa mikopo tayari kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

 

MAFANIKIO

Viwanda vidogo vidogo 15 vya usindikaji vimeanzishwa  mfano; usindikaji wa unga, maziwa, mafuta ya alizeti, uyoga nk.

 

CHANGAMOTO

1. Bajeti ni finyu na hivyo kushindwa kutoa mafunzo kwa vikundi vingi zaidi ili viweze kuanzisha viwanda vya usindikaji zaidi..

2. Kiwanda cha “Tanzania Machine Tools” kutofanya kazi yake sawa sawa na    hivyo kuathiri soko la ajira.

 

 

 

BIASHARA

 

Eneo lingine ambalo Halmashauri inawajibika ni kuratibu shughuli zote za biashara zinazofanyika Wilayani Hai  Katika eneo hili Halmashauri inawajibika kuhakikisha biashara zote zinafuata taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa  kwa mujibu sheria mama za biashara  na sheria ndogo ndogo za Halmashauri. 

 

MALENGO

Katika kipindi cha 2006/2007 malengo yalikuwa kuongeza utambuzi wa wafanyabiashara na lesseni za biashara ili kuongeza mapato ya Halmashauri. Hali ya biashara katika Halmasahuri ya Wilaya ya Hai  ilikuwa kama ifuatavyo:-

 

 

 

KIPINDI

 

IDADI YA WAFANYA BIASHARA WALIOKUWEPO

 

LESENI MPYA ZILIZOTOLEWA WAFANYA BIASHARA (WAPYA)

2006/2007

1766

69

 

MAFANIKIO

Kutokana  na kukua Kibiashara katika Wilaya yetu mwaka  mwaka 2006/2007 wafanyabiashara waliongezeka   69 na kufanya idadi kuwa jumla ya wafanyabiashara 1,766.

 

 

CHANGAMOTO

4.      Ufinyu wa bajeti.

5.      Wafanyabiasgara wengi kutolipia lesseni zao za biashara kwa wakati.

 

2.1.1.3    MALIASILI, MAZINGIRA NA ARDHI 2006/2007

 

Katika utekelezaji wa MKUKUTA  na Ilani ya Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya imetunga na kupitisha sheria ndogo ya hifadhi ya mazingira, ambayo pamoja mambo mengine, inakataza ukataji miti ovyo, uchomaji wa misitu  na uharibifu wa vyanzo vya maji. Pia sheria hiyo inaelekeza ni sehemu gani ambazo mifugo inatakiwa kufugwa na sehemu ambazo kilimo kinatakiwa kufanywa.

 

Kwa mwaka wa 2006/2007 malengo katika Ardhi na uhifadhi wa mazingira yalikuwa kama ifuatavyo:-

 

 1. ARDHI : Kupima viwanja zaidi ya 500.
 2. MISITU : Kuweka utaratibu shirikishi wa upandaji na Uvunaji Miti, kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa kuhusisha sekta binafsi, NGOs, Vijiji [Jamii]
 3. NYUKI : Kuongeza msukumo katika kuendeleza ufugaji nyuki kwa ajili ya kuzalisha asali na nta kibiashara. Katika vikundi Taasisi na Watu Binafsi.

 

 1. WANYAMAPORI: Kulinda mali na maisha ya Watu dhidi ya Wanyama Wakali na waharibifu.

 

Bajeti:

SEKTA

2006-2007

 

H/SHAURI

RUZUKU

JML

Ardhi

7,423,755.00

 

7,423,755.00

Maliasili

4,763,986.00

 

4,763,986.00

 

Utekelezaji:

Utekelezaji ulikuwa  kama ifuatavyo:-

1.      Viwanja 200 vilipimwa na 300 kurudishiwa ‘beacons’ kwa kuwa ziling’olewa katika kitalu N.

2.      Upandaji Miti  - Jumla ya miti 1,200,000 ilipandwa katika maeneo mbali mbali ambayo ni sawa na asilimia 80% ya lengo la miti 1,500,000.

3.      Kila Kijiji kina Kamati ya Mazingira jumla ya Kamati 55 zimeundwa na zinafanya kazi.

4.      Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya za kudhibiti uharibifu wa Mazingira zipo na zinatumika.

5.      NGOs 5 zinashiriki kupanda miti.

6.      Vikundi 6 vinashiriki katika upandaji wa Miti.

 

Mafanikio:

 

 1. Migogoro ya ardhi na viwanja imepungua na watu wanaendelea kujenga kufuata utaratibu wa Mipango Miji.  Mwongozo wa sheria mpya ya ardhi na mipango miji unazingatiwa na wananchi wamehamasika..
 2. Vyanzo vya maji vimeboreka na jamii inazingatia utunzaji na ulinzi wa vyanzo hivyo. 
  1. Kiwango cha upandaji miti katika juhudi za kuboresha mazingira kimeongezeka mijini na vijijini.
  2. Jamii imeelimika na kuzingatia sheria za hifadhi na matumizi endelevu ya ardhi, maliasili na mazingira.  Kiwango cha ukataji miti ovyo kimepungua.
  3. wananchi wamepata mwamko wa kutumia teknolojia rahisi na sahihi katika matumizi ya rasilimali za maliasili.  Kiwwango cha uelewa wa matumizi ya nishati mbadala kimeongezeka.
 3. Jamii imeelimika juu ya ufugaji bora wa nyuki na matumizi ya mazao yake.

Changamoto

Katika kipindi hiki cha 2006/07 changamoto zifuatazo ziliikabili Idara:-

 

 1. Uhaba wa Ardhi na ukosefu wa fedha za fidia kwa ardhi inayotarajiwa kutwaliwa.
 2. Uhaba wa Vitendea Kazi.
 3. Upungufu wa Watumishi/Watalaamu
 4. Uelewa mdogo wa Jamii kuhusu sera na sheria za kisekta.
 5. Uhaba wa ardhi kwa ajili ya uzalishaji

Technolojia duni.                    

 

 

2.1.1.4    USHIRIKA

 

Katika Halmashauri ya wilaya ya Hai kuna jumla ya vyama vya Ushirika 67 vya aina mbalimbali kama ifuatavyo:

 1. Vyama vya mazao                                          25
 2. Vyama vya akiba na mikopo(SACCOS)       26
 3. vyama vya mziwa                                            7
 4. Vyama vya Umwagiliaji                                  2
 5. Vyama vya Uzalishaji biashara                       2
 6. Vyama vya Maduka                                        1
 7. Vyama vya Uzalishaji asali                             1

 

Katika utekelezaji wa malengo ya MKUKUTA na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010, Halmashauri ya wilaya ya Hai kupitia Idara ya Ushirika imetekeleza mambo yafuatayo:

 

      MALENGO KWA MWAKA  2006/2007

 • Kutoa mafunzo kwa bodi za vyama vya ushirika kuhusu majukumu yao ya kila siku
 • Kuhamasisha wananchi kujiunga na vyama vya ushirika
 • Kuhamasisha wananchi kuanzisha vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS)
 • Kufanya ukaguzi wamara kwa mara katika vyama vya ushirika
 • Kutoa mafunzo kwa wanachama kuhusu  haki na wajibu wao
 • Kuimarisha kuendeleza vita dhidi ya rushwa katika vyama vya ushirika

 

           BAJETI

 

      Ili kufikia malengo hayo, Halmashauri ya wilaya ilitenga jumla ya    Tshs: 12,000,000/= toka DADPs na Tshs: 4,000,000.00 toka mapato ya ndani ya Hamashauri.

 

 

 

 

 

 

         UTEKELEZAJI

  

    Mambo yaliyotekelezwa kwa mwaka huu ni kama yafuatayo:

·        Elimu ya ushirika ilitolewa kwa viongozi wa vyama vya ushirika 55.

·        Jumla ya viongozi 440 wa vyama vya ushirika walihudhuria mafunzo hayo

·        Vyama vilivyokaguliwa, ukaguzi wa mara kwa mara  vilikuwa vyama 4 na ukaguzi wa mwisho ilikuwa vyama 34

·        Elimu ya ubaya wa rushwa umeelezwa katika mikutano na vikao vya vyama vya ushirika.

 

 MAFANIKIO

              

·        Hadi kufikia mwishoni mwaka 2006/2007 wanachama  780 waliongezeka, kutoka wanachama 25,024 hadi kufikia wanachama 25,804

·        Vyama vya ushirika wa Akiba na mikopo (SACCOS) viliongezeka toka vyama vya Akiba na mikopo (SACCOS) 13 hadi vyama 20

·        Wanachama wa SACCOS waliongeza hisa zao kufikia  Tshs: 316,082,441.00, waliongeza akiba zao hadi kufikia             Tshs: 913,146,249.00,amana ziliongezeka kufikia                        Tshs: 225,945,073.00 na Mikopo iliyotolewa kwa wanachama ni   Tshs: 1,334,823,331.00

 

2.1.1.5 MASHAMBA MAKUBWA 2006/2007

 

 

MASHAMBA MAKUBWA YANAYOMILIKIWA NAVYAMA VYA USHIRIKA

 

Katika wilaya ya Hai kuna mashamba 17 yanayomilikiwa na vyama vya ushirika kama inavyoonekana kwenye Jedwali

 

ORODHA YA MASHAMBA YANAYOMILIKIWA NAVYAMA VYA USHIRIKA.

 

Na.

Jina la Shamba

Hekta

Mmiliki

Mwekezaji

Mazao

1.

Narumu

17,116

Chama cha Msingi - Lyamungo

African Plantation Kiimanjaro

Kahawa

2.

Xeno

82.0

Chama cha Msingi - Lyamungo

African Plantation Kiimanjaro

Kahawa

3.

Edelweiss

59.2

Chama cha Msingi - Lyamungo

African Plantation Kiimanjaro

Kahawa

4.

Helena

33.5

Chama cha Msingi - Lyamungo

Chama cha Msingi - Lyamungo

Kahawa

mahindi

5.

Two bridges

421.6

Chama cha Msingi Narumu na Manushi

Afican Plantation

Kahawa

6.

7.

Silverdale na Mbono

397.24

Kyeeri, Shari na Uswaa

M/s Fiona Tz. Ltd.

Kahawa mahindi

mbogamboga

8.

Glastra

68.3

Chama cha Msingi Foo, Wari na Nronga

Mkomari & Godbless Farm Enterprises

Kahawa

Mahindi

Vanilla

9.

Sirra

21.92

Chama cha Msingi Foo, Wari na Nronga

Mkomari & Godbless Farm Enterprises

Kahawa

mahindi

10.

Lambo

625.2

Chama cha Msingi Foo, Wari na Nronga

SHITECO

Kahawa

Mahindi

Snap beans

11.

Makoa estate.

143.2

Chama cha Msingi Uduru Makoa

Tierhife (T) Ltd.

Kahawa

Mahindi

12.

Makuru

194

Chama cha Msingi Nshara

N.G. Emanuel & Sons

Kahawa

mahindi

13.

Mkufi

310.8

Chama cha Msingi Machame Nkuu

N.G. Emanuel & Sons

Kahawa na

Maua

14.

Kibo/Kikafu

814

Vyama vya Msingi Roo, Saawe,Sonu,Ngira, Mudio na Masama Mula

Tudeley Estates Ltd.

Kahawa

Mahindi

15.

Nkwansira

218

Vyama vya Msingi Nkwansira, Kyuu, Isuki, Marukeni, Lemira na Mroma

P H Ghikas & Sons Ltd.

Kahawa

Mahindi

16.

Mbosho/Uwau

217.3

Chama cha Msingi Masama Mula

Shira farming Co.ltd

Kahawa

Mahindi

Mboga

17.

Boloti

196.8

Lukani Losaa

Bourbon Coffee Estate

Kahawa

18

Bondeni Estate

311.2

Chama cha Mashua na Kashashi

Shira Farming

Kahawa

mahindi

 

MALENGO 2006/2007

 

 • Mashamba yote 18 yawe na wawekezaji
 • Wawekezaji waweze kufufua zao la kahawa

 

MAFANIKIO

·        Mashamba 17 yalikuwa na wawekezaji

·        Ongezeko la ajira kwa wananchi

 

 

CHANGAMOTO

 • Baadhi ya wawekezaji huwakodishia wananchi kwa ajili ya kilimo cha mahindi
 • Baadhi ya wawekezaji kutolipa kodi ya pango kwa vyama vya ushirika
 • Baadhi ya wawekezaji hulima mazao mengine badala ya kahawa.
 • Baadhi ya mikataba haikufuata taratibu na sheria za vyama vya ushirika.

 

2.1.1.6 BARABARA:

 

Wilaya ya Hai ina  barabara zenye urefu wa Km.466.2.  Kati ya kilomita hizo,  km. 32 ni za barabara Kuu (Trunck Roads), km. 42 ni za Mkoa (Regional Roads), km.  175.93 ni za Wilaya (District Roads) na km.150.27 ni za vijiji (Feeder roads) na barabara za Hai Mjini ni km.66 (Hai urban roads)

 

Katika kutekeleza MKUKUTA na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 hadi 2010 ukurasa wa 52.( ibara ya 44)  Halmashauri ya Wilaya ya Hai imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara za Wilaya kadri bajeti ilivyoongezeka na hivyo kupunguza adha ya usafiri na usafirishaji wa mazao mbalimbali kwa wananchi wa Hai.

 

MALENGO YA  MATENGENEZO YA BARABARA KWA MWAKA WA FEDHA WA 2006/2007 :-

Matengenezo  ya kawaida ya  (km.140.4)

matengenezo ya  sehemu  korofi (km 26.2)

matengenezo ya muda maalum  ( km 5 )

kuimarisha madaraja na   makalvati

usimamizi na matengenezo ya gari la barabara,

 

UKARABATI WA MIUNDOMBINU WA MIRADI YA MIFUMO YA MASOKOYA KILIMO (AMSDP)

barabara ya Kwasadala – Longoi (km. 17.3)

Barabara ya Mungushi – Kware (km. 3.2)

 

Katika mwaka wa fedha 2006/07 barabara zenye urefu wa km. 291.2 zilifanyiwa matengenezo kwa gharama ya TShs. 515,049,000/=  kutoka Mfuko wa barabara na mradi wa Mazao na Masoko (AMSDP). Kati ya fedha hizo Tshs. 147,600,000/= zilitoka mfuko wa barabara (Road Fund) na zilitumika kutengeneza km. 271.2 ambapo km. 140.4 zilifanyiwa matengenezo ya kawaida kwa TShs. 62,870,000/=, km 26.2 zilifanyiwa matengenezo ya  sehemu  korofi kwa Tshs. 35,024,000/=, km. 5 zilifanyiwa matengenezo ya muda maalum kwa TShs. 35,000,000/=, kuimarisha madaraja na   makalvati  kwa TShs. 2,080,000/=    na gharama za usimamizi na matengenezo ya gari la barabara, ni TShs. 8,000,000/=.

 

Mradi wa Mazao na Masoko (AMSDP) ulitoa kiasi cha Tshs. 367,449,000/= kwa ajili ya kukarabati barabara ya Kwasadala – Longoi (km. 17.3) kwa gharama ya Tshs. 312,449,000/= na barabara ya Mungushi – Kware (km. 3.2) kwa gharama ya Tshs. 55,000,000/=.

Mapato haya ni sawa na asilimia 100 ya  utekelezaji wa  kazi  ya  lengo lililokusudiwa.

 

MAFANIKIO

 

Halmashauri ya Wilaya ya Hai inapata mafanikio makubwa kwa kuboresha miundo mbinu mbalimbali kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya barabara kila mwaka (Road Fund) na vianzia mbali mbali na kufanya barabara nyingi kupitika wakati wote.

Barabara kupitika kwa wakati wote kumepunguza kero na adha ya usafiri na usafishaji wa mazao mbalimbali ya wananchi kutoka mashambani kwenda nyumbani na masoko mbalimbali ya ndani na nje ya Wilaya.

 

CHANGAMOTO

Halmashauri ya Hai inafanya juhudi kubwa ya kuendeleza kuboresha miundo mbinu lakini bado kuna baadhi ya wananchi wa korofi wanarudisha nyuma juhudi hizo kwa kupitisha maji barabarani wakati wanamwagilia mashamba yao,kufukia mifereji ya kuzuia/kutolea maji yasiende barabarani, wanaiba alama/samani za barabara, wanaweka matuta barabarani bila utaratibu wa kiutaalam, wanaharibu kingo za mito kwa kuchimba mawe na michanga hivyo kuhatarisha misingi ya madaraja, wanaswaga/kupitisha mifugo barabarani wakati wa kupeleka malishoni au kurudisha nyumbani.

 

 

2.1.2       UIMARISHAJI WA HUDUMA ZA JAMII

 

2.1.2.1MAJI 2007/2008

 

Wilaya ya Hai imeweka mipango ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa kutoa huduma ya maji Safi na Salama katika umbali usiozidi   mita 400 kama ilivyo katika sera ya maji ya Taifa (2002).  Miradi hiyo imetekelezwa kwa kushirikisha wananchi katika hatua za kutoa huduma ya maji kwa kupanga, kujenga, kuendelesha na kumiliki kwa kupitia vyombo vyao walivyoanzisha wenyewe kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya CCM 2005  na malengo ya MKUKUTA.

 

Wilaya inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 183,712 kwa sasa na wananchi wanaopata huduma ya maji Safi na Salama ni 141,712 ambao ni sawa na asilimia 77 ya wakazi wote.

 

UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI MWAKA 2006/07

Malengo:

Kupeleka huduma ya maji katika vijiji sita vya kata ya Machame Mashariki na Zahanati ya Mkalama.

 

Skimu ya maji Lyamungo.

Gharama za mradi: Mradi huu umegharimu Tshs. 1.2 billion ambazo zimetolewa na Serikali  ya Ujerumani (KFW)  kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.

 

Utekelezaji: Kazi zilizotekelezwa katika mradi huu ni ujenzi wa matanki mbalimbali  yenye ujazo wa  lita 1,500, ununuzi wa bomba na viungio  18km na ujenzi wa matanki  ya vunja msukumo  matatu.

 

Mafanikio:  Vijiji  vitatu vya  Lyamungo Kilanya, Kati na Sinde vilifanikiwa kupata huduma ya maji safi na salama.

 

Uvunaji wa maji ya mvua:

Gharama za Mradi: -  Mradi huu umegharimu Tshs. 10,500,000/=

 

Utekelezaji: -  Ujenzi wa  tanki la kuvuna maji ya mvua lenye ujazo wa lita  50,000.

 

Mafanikio:  -   Zahanati ya Mkalama imefanikiwa kupata maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa.

 

MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KATIKA WILAYA YA HAI

Hadi sasa wananchi wanaopata  huduma ya maji ni asilimia 77% na inatarajiwa 

kuwezesha upatikanaji wa huduma ya maji Safi na Salama katika umbali  usiozidi mita 400 kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2012 ambapo malengo ya MKUKUTA ni asilimia 65 na Milenia 74% (2015).

 

Changamoto:

Tatizo la mazoea. Miradi yote ya Wilaya ya Hai ni ya Mtiririko hivyo wananchi hawajui  aina nyingine ya  mradi wa maji.

Mfano Mradi wa Kisima kirefu (borehole) wa Kijiji cha Mtakuja.

Elimu duni juu ya aina ya vyanzo vya maji.

 

Biashara ya vyuma chakavu inasababisha wananchi wasio waaminifu kuharibu miundo mbinu ya maji.

 

Huduma ya maji  kuonekana kwamba ni ya bure.

 

Wananchi kutoelewa madhara ya uhabifu vyanzo vya maji na  uchafuzi wa mazingira.

 

Mkakati

Kushirikisha kamati ya maji safi na usafi wa mazingira katika ngazi ya kijiji, kata na Wilaya kwa ajili ya kutoa elimu.

 

Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na kamati ya maji Safi na Mazingira ya Wilaya kuelimisha wananchi  wa kijiji cha Mtakuja ili waweze kufikia uamuzi wa kuchagua mradi wa maji endelevu na unaowafaa.

 

2.1.2.2   AFYA

 

Katika kutekeleza MKUKUTA na Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005 Ibara ya 66 kifungu (a) hadi (j) Idara imetekeleza huduma zake kulingana na malengo ya Idara kama ilivyo orodheshwa hapo chini.

 

HALI HALISI YA WILAYA

Wilaya ya Hai ina jumla ya Hospitali 2, Vituo vya afya 3, Zahanati 48

 

AINA YA KUTUO CHA HUDUMA

IDADI

UMILIKI

Serikali

Shirika la Dini

Binafsi

Hospitali

2

1

1

0

Vituo vya Afya

3

3

0

0

Zahanati

48

22

10

16

 

Pamoja na Vituo hivyo vya kutolea huduma Wilaya pia ina maduka ya kuuza madawa yapatayo 22 na kila kijiji kina wahuduma wa Afya wawili (2) wanaofanya kazi ambao idadi yao ni110.

 

USHIRIKISHWAJI WA JAMII

Katika utekelezaji wa huduma za Afya, Wilaya imeanzisha mfuko wa Afya ya Jamii, na Jamii imeshirikishwa kwa kuunda Kamati za usimamizi za Hospitali, Vituo vya Afya, na Zahanati pia Bodi ya Afya ya Wilaya imeundwa na kufunya kazi.

 

UIMARISHAJI WA HUDUMA ZA AFYA.

Katika kipindi cha mwaka 2006/2007 idara iliidhinishiwa jumla ya Tshs 2,158,252,910/= kati ya fedha hizo jumla ya Tshs. 1,261,793,659/= zilitumika kulipa mishahara ya watumishi na kiasi cha Tshs. 619,212,151/= matumizi ya kawaida. 

 

 

 

MIRADI YA MAENDELEO

Idara iliidhinishiwa kiasi cha Tsh. 277,247,100/= ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

MALENGO:

 1. Ujenzi wa jengo la uzazi na Afya ya mtoto pamoja na nyumba ya mtumishi Lambo.
 2. Kufanya ukarabati wa majengo ya kutoa huduma.
 3. Kupunguza vifo vya akina mama wajawazito
 4. Kupunguza vifo watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
 5. Kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria
 6. Kuongeza vituo vya kutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI toka kwa mama kwenda kwa mtoto

 

Utekelezaji:

 1. Ujenzi wa jengo la kutolea huduma ya uzazi na Afya ya mtoto na nyumba ya mtumishi zilikamilika.
 2. Ukarabati ulifanyika katika vituo saba (7) vya kutolea huduma
 3. Kupunguza vifo vya mama vitokanavyo na uzazi vimepungua toka 44/100,000 hadi 40/100,000
 4. Chanjo ilitolewa kwa watoto chini ya mwaka mmoja kama ifuatavyo:
  • BCG 98.2%
  • Polio3 96.3%
  • DPT HB3 95.2%
  • Surua 93.6%
  • Vitamin A 96%
 5. Chanjo ilitolewa kwa akina mama wajawazito kama ifuatavyo:-

TT2+ 91%

 1. Kiwango cha Malaria kimepungua toka 20% hadi kufikia 17%
 2. Vituo vya kutolea huduma vimeongezwa hadi kufikia vituo 38.

 

Changamoto

 1. Baadhi ya vifaa muhimu na madawa havipatikani katika bohari ya madawa MSD
 2. Uhaba wa wataalam wa afya.
 3. Ukosefu wa jengo la upasuaji na X-ray na mitambo yake.

 

Mkakati:

 1. Kuhakikisha jengo limekamilika na kufanya kazi.
 2. Kuhakikisha majengo ya kutolea huduma yamekarabatiwa.
 3. Kuhakikisha vifo vya mama vitokanavyo na uzazi vinapungua toka 44/100,000 hadi 40/100,000.
 4. Kuhakikisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinapungua  toka 124/1,000 hadi 74/1,000.
 5. Kuhakikisha kiwango cha Malaria kimepungua kutoka 20% hadi 17%.
 6. Kuhakikisha vituo vya kutolea huduma ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda  kwa  mtoto vimeongezeka toka kimoja hadi vitano.

 

MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

 

Ili kutimiza kauli mbiu; ondoa woga, pata ushauri nasaha, pima kwa hiari,

yafutayo yalilengwa kwa mwaka 2006/2007

 1. Kuhamasisha/mafunzo kwa wananchi juu ya suala zima la kujikinga na ukimwi
 2. Kuhamasisha/mafunzo kwa wananchi juu ya upimaji wa hiari wa afya zao
 3. Kufungua vituo vya PMTCT 10 katika Zahanati za Wilaya.

Fedha zilizoidhinishwa na Halmashauri kwa mwaka wa 2006/2007 kutumika katika kazi hizo zilikuwa Tsh 67,000,000/=

 

Utekelezaji:

 1. Uhamasishaji na utoaji mafunzo kwa wananchi juu ya suala zima la kujikinga na UKIMWI yalitolewa kwa  viongozi Kata 10 za Wilaya.
 2. Uhamasishaji/mafuzno yalifanyika katika vijiji vyote 55 na vitongoji 260.
 3. Vituo vya PMTCT katika Zahanati za Wilaya zimefunguliwa.

 

Mafanikio:

 1. Wananchi wamepata ufahamu namna ya kufanya ngono iliyo salama
 2. Baadhi ya wananchi wamekubali kupima afya zao.
 3. Jamii imepata huduma kwa karibu zaidi.  

Changamoto:

 1. Baadhi ya wananchi bado hawako tayari kutumia kondomu
 2. Ufahamu mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu wa kupima afya zao.

Mkakati:

 1. Kuendelea kutoa elimu sahihi ya matumizi ya kondomu kwa jamii.
 2. Kuendelea kutoa elimu ya UKIMWI na athari zake kwa wananchi.

 

2.1.2.3            ELIMU

 

MALENGO, MAFANIKIO NA CHANGAMOTO 2006/2007

 

Kulingana na malengo ya MKUKUTA na ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005 kwa upande wa Elimu ililenga yafuatayo:-

 

 1. Uandikishaji wa watoto wote wenye umri wa miaka 7
 2. Kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliofaulu Elimu ya Sekondari wanajiunga kidato cha kwanza.
 3. Kuhakikisha kwamba watoto wote waliokosa Elimu ya Msingi wanasajiliwa
 4. Kuwapatia Elimu watoto wenye mahitaji maalum.

 

 

BAJETI YA IDARA YA ELIMU:

 

MAELEZO

2006/2007

YA KASMA

 

 

 

MAKISIO

MATUMIZI

PE & OC

5,046,168,758.00

4,919,194,266.84

MMEM CAP

414,344,000.00

227,262,904.96

MMEM DEV

792,300,000.00

110,525,000.00

 

 

Utekelezaji wa malengo kwa  Halmashauri ya Wilaya ya Hai:

 

Ø      Uandikishaji  wa wanafunzi:

Ø      Elimu ya Awali:

 Idadi ya wanafunzi waliandikishwa katika  madarasa ya Awali ni

                Wav: 2028        Was: 1875      Jml: 3903

 

Ø      Elimu ya Msingi.

Katika swala la uandikishaji,wa wanafunzi wa darasa la kwanza tumeandikisha watoto wote wenye wenye umri wa miaka 7 na kuondoa mlundikano wa waliozidi  umri wa miaka saba waliostahili kuandikishwa shule ya msingi kama inavyooneshwa  katika Jedwali lifuatalo.

 

 

Uandikishwaji  wa wanafunzi  darasa la I

 

MWAKA

WALIOATARAJIWA

WALIOANDIKISHWA

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

%

2006

4072

3921

7993

3992

3992

7915

99

2007

3175

2739

5914

2766

2595

5361

90

 

 

 

Ø      Ufaulu  wa wanafunzi na kujiunga na kidato cha kwanza

Wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la VII  na kufaulu kuanzia mwaka 2005 – 2007 wamepata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza   kutoka asilimia 59% hadi 100% .  Mafanikio haya yametokana na kuwepo kwa juhudi za ujenzi wa vyumba vya madarasa  katika shule za Sekondari za wananchi kama inavyooneshwa katika Jedwali  lifuatalo:-

 

Ufaulu wa wanafunzi na kuchaguliwa  kujiunga na kidato cha kwanza

 

MWAKA

WALIOFANYA

WALIOFAULU

WALIOPATA NAFASI

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

%

WAV

WAS

JML

%

2006

3225

3507

6732

2631

3177

5808

84.35%

2435

2682

5117

92.4%

2007

2425

2399

4822

1083

1267

2350

48.73%

1083

1267

2350

100%

 

 

Ø                  Kusajiliwa kwa wanafunzi wote waliokosa Elimu ya Msingi:-

Kumekuwepo jitihada  za  kuanzisha  vituo kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi Elimu ya Msingi kwa wale walioikosa ( MEMKWA)  kwa wale wote wenye umri zaidi miaka 10 ambao walikuwa hawajaandikishwa darasa la kwanza.    Mafanikio yameonekana kuwa mazuri kwani  wanafunzi 37 waliofanya mtihani wa darasa la nne mwaka 2007 wote wamefaulu kuendelea darasa la tano kama ilivyooneshwa kwenye Jedwali  lifuatalo:-

 

UANDIKISHAJI WA MEMKWA

 

MWAKA

WALIOANDIKISHWA

 

KUNDI RIKA I

KUNDI RIKA II

JUMLA 

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

2005

52

38

90

46

34

80

98

72

170

2006

79

46

125

64

26

90

143

72

215

2007

22

15

37

-

-

-

22

15

37

 

 

 

Ø      Elimu kwa wenye mahitaji maalum.

Wilaya inafanya juhudi kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanatambuliwa na kuthaminiwa. Katika mchakato wa kuhakikisha kwamba wanapata  Elimu kama watoto wengine tayari imeanzisha vituo vya kutolea Elimu Maalum kama inavyoneshwa katika Jedwali lifuatalo:-

 

ELIMU KWA WENYE  MAHITAJI MAALUM

NA

SHULE

WASIIONA

VIZIWI

ALBINO

ULEMAVU WA AKILI

 

 

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

1

St.Francis wa Asis

9

5

14

17

27

44

11

5

16

1

1

2

2

Mbweera

-

-

-

-

-

-

-

-

-

31

16

47

3

KIA

-

-

-

-

-

-

-

-

-

5

6

11

4

Rundugai

-

-

-

-

-

-

-

-

-

4

4

8

 

Jumla

9

5

14

17

27

44

11

5

16

41

27

68

 

 

ELIMU YA UFUNDI:

 

Wilaya inayo vituo vya Ufundi Stadi  3 na kituo kimoja cha VETA.   Vituo hivi 3 viko katika shule za msingi.  Idadi ya wanafunzi katika vituo vya Ufundi Stadi

 

 

KITUO

MWAKA WA 1

MWAKA WA II

 

JUMLA KUU

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

NSHARA

29

-

29

18

-

18

47

MROMA

14

-

14

18

-

18

32

SERE

12

-

12

16

-

16

28

JUMLA

55

-

55

52

-

52

107

            

 

MIUNDO MBINU :Wilaya kupitia idara ya Elimu ilikusudia kuongeza miundo  mbinu yakiwemo madarasa, nyumba za walimu vyoo na utengenezaji wa madawati. Taarifa za 2005, 2006 na 2007 zinahusiana na Wilaya ya Hai na Wilaya ya Siha

 

MAFANIKIO: MWAKA 2006/2007

 1. Kumekuwa na ongezeko la miundo mbinu katika kupunguza msongamano wa wanafunzi – darasa I wanafunzi 40 – 50. Dawati  1 wanafunzi 2 – 3.
 2. Shule nyingi zimeboresha mazingira hasa uoteshaji wa miti ya kivuli, uzio (sawa na shule 68 kati ya shule 103) sawa na asilimia 66%.
 3. Walimu wamejiendeleza katika programu ya MUKA na waliobaki ni walimu daraja B/C ambao ni 35 kati ya walimu 539 sawa na asilimia 6.4
 4. Ujenzi wa visima vya kuvuna maji.  Hadi sasa vimejengwa visima  35 kati  ya vituo 103 sawa na asilimia 32%.

 

Changamoto katika Elimu ya Msingi 2006/2007

 

 1. Baadhi ya familia kuwaficha  baadhi ya watoto wenye kuhitaji Elimu maalum.
 2. Miundo mbinu kutokukamilika kwa wakati kutokana na mfumuko wa bei na kipato cha wananchi.
 3. Idadi ya watoto wanaoandikishwa na wanaomaliza kutofautiana hasa maeneo ya wafugaji.
 4. Ujenzi wa kituo kikuu cha Wilaya cha walimu kwa ajili ya kuendesha  mafunzo na semina mbalimbali.
 5. Kutokana na eneo la shule kuwa finyu miundo mbinu mingine inashindikana kuwepo shuleni – mfano nyumba za walimu, maktaba, bwalo la chakula, viwanja vya michezo n.k.
 6. Ujenzi wa shule ya waalemavu ya Wilaya (Multipurpose Centre)
 7. Vituo vya Ufundi vina uhaba mkubwa wa vifaa na upungufu wa walimu wa fani za ufundi

               

 

ELIMU YA  SEKONDARI:2006/2007

Wilaya ya Hai ina shule 40 za Sekondari zikiwemo 27  za Serikali na 13 binafsi. Shule za Serikali zina wanafunzi 8202 kati yao Wavulana 3746 na Wasichana 4456.

 

Mwaka 2005 tulikuwa na Sekondari za Serikali 14

Mwaka 2006 tulikuwa na shule za Sekondari za Serikali  27.

Mwaka 2007 na 2008 lengo ni kuongeza vyumba vya madarasa  26.

 

MIUNDO MBINU: 2006/2007

 1. Viko vyumba vya madarasa 212
 2. Ziko nyumba za walimu 51
 3. Yamejengwa matundu ya vyoo 341 kwa mwaka 2008
 4. Miundo mbinu ilikuwa kama ifuatavyo:-

(i)                 Mwaka 2006 vilijengwa vyumba  vya  madarasa 44.

(ii)               Mwaka 2007 – Vilijengwa vyumba vya madarasa  18.

            Jumla ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa ni 62.

 

MAFANIKIO:

 

 1. Shule 10 zimepata maeneo ya ujenzi
 2. Upatikanaji wa fedha za TASAF, LCDG na MMES umeongeza kasi ya ujenzi na upanuzi wa Sekondari  (TASAF Tshs. 336,546,541/= LGDG Tshs 44,000,000/=na MMES  Tshs,. 170,000,000/=).   Fedha kutoka mfuko wa TASAF umejenge vyumba 39 vya madarasa.

 

 

CHANGAMOTO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI 2006/2007

 

 1. upungufu wa majengo ya utawala katika shule za sekondari 19
 2. upungufu wa nyumba za walimu katika shule 12
 3. upungufu wa maabara katika shule za Sekondari 23
 4. Upungufu wa mabwalo katika shule za sekondari 24
 5. Upungufu wa maktaba katika shule za Sekondari 25
 6. Baadhi ya wananchi kutochangia mipango ya Elimu ya Sekondari ambayo inasababishwa na kipato duni
 7. Mfumuko wa bei za vifaa vya ujenzi
 8. Upungufu wa walimu
 9. Maeneo ya kujenga miundo mbinu ya sekondari yamekuwa haba kutokana na ufinyu wa ardhi.

 

 

2.1.3       UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI

 

Katika kutekeleza MKUKUTA na Ilani ya CCM 2005 -2010 kwa kuhakikisha kuwa serikali inawajibika katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia Demokrasia Ushirikishwaji na uwazi,Halmashauri imejiwekea malengo yafuatayo;

1.Kujaza nafasi wazi za viongozi wa kuchaguliwa ngazi ya vijiji na vitongoji.

2.Kuweka mbao za matangazo katika ofisi 10 za kata na 55 za vijiji.

3.Kuweka masanduku ya maoni katika kata vijiji na sehemu zote za kutolea huduma.

4.Kutoa mafunzo kwa viongozi wa kuchaguliwa ngazi ya kata na vijiji ili wafahamu wajibu wao.

5.Kufanya vikao vya kisheria kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya.

6.Kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kupambana na Rushwa na madawa ya kulevya.

7.Kuweka wazi taarifa zote za mapato na matumizi ya Halmashauri ili wananchi wote    waweze kusoma.

8.Kuelimisha wananchi namna ya kuibua miradi kwa kuzingatia dhana shirikishi.

 

Utekelezaji wa malengo hayo unaonekana katika nyanja za Demokrasia, Uwazi na Ushirikishwaji.

 

DEMOKRASIA

Kwa mwaka 2006/2007 nafasi wazi za uongozi ngazi za chini zilijazwa kama ifuatavyo:-

-Wenyeviti wa vijiji - 2

-Wenyeviti wa vitongoji -15

-Wajumbe wa Serikali ya Kijiji - 34

 

Kwa mwaka 2007/2008 nafasi hizo zilijazwa kama ifuatavyo:-

-Wenyeviti wa vijiji - 1

-Wenyeviti wa vitongoji -10

-Wajumbe wa Serekali ya Kijiji - 77

 

Aidha Halmashauri imesimamia uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, zoezi lililoanza tarehe 22-27 Septemba 2008 ambapo wananchi wenye sifa waliojiandikisha

Kwa mara ya kwanza walikuwa 5,315 , walirekebisha taarifa walikuwa 3,897 na waliofuta taarifa walikuwa 322.

 

Kwa mwaka 2006/2007 vikao na mikutano ngazi ya Halmashauri, ilifanyika kwa asilimia 100% kama ilivyopangwa. Ngazi ya Kata (WDC), asilimia 40% mikutano mikuu ya vijiji na asilimia 51% , halmashauri za vijiji 62.4%  na mikutano ya vitongoji 46%  kama inavyoonekana katika kiambatanisho, Jedwali A:

Wilaya inaendelea kuhamasisha  na kusimamia ngazi zote ziweze kufanya mikutano na vikao kama ilivyo kwa mujibu wa sheria.

 

JEDWALI A.

NA

MKUTANO/VIKAO

VILIVYOTARAJIWA

VILIVYOFANYIKA

ASILIMIA

1

Mikutano ya Halmashauri

4

4

100

2

Vikao vya Maendeleo ya Kata (WDC)

40

16

40

3

Mikutano mikuu ya Vijiji

220

112

51

4

Vikao vya serekali ya Vijiji

660

412

62.4

5

Vikao vya Vitongoji

3084

1424

46.2

 

 

UWAZI

Ili kuimarisha uwazi,Halmashauri imeweka masanduku ya maoni katika ngazi zote za utawala na vituo vya kutolea huduma ambapo yamewekwa katika kata 10, vijiji 55, Vituo vya Afya 3 na Zahanati 22.

 

Halmashauri pia imeweka mbao za matangazo katika kata zote 10 na vijiji 55,ambapo taarifa zote muhimu za Halmashauri na Serikali za vijiji kama vile taarifa za mapokezi ya fedha, taarifa za mapato na matumizi na matangazo mbalimbali kwa umma hubandikwa. Wilaya inamiliki Redio yake ya Jamii ambayo husaidia kuifikishia jamii taarifa zote muhimu za kiwilaya na zile za Serikali kwa ujumla. Pia inatoa ajira kwa vijana kwa sasa imeajiri vijana 12 waliopewa mafunzo mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa Redio. Mafunzo waliyopewa tangu mwaka 2003 ni yale ya fani za Utangazaji, Uandishi, Ufundi mitambo, UDJ na Utayarishaji vipindi. Shirika la UNICEF pamoja na kugharamia mafunzo limetoa vifaa vya redio vyenye thamani ya Shs. 97,050,00/= Halmashauri imegharamia Shs. 85,000.000/= 

 

USHIRIKISHWAJI

Upangaji, Usimamizi na Utekelezaji wa Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika ngazi ya Vijiji umekuwa ukifanywa kwa kutumia dhana shirikishi ya Fursa na Vikwazo          (O & OD). 

-Mafunzo yametolewa kwa viongozi ngazi ya kata na vijiji kuhusu namna ya kuibua miradi,kusimamia na kutoa taarifa.

 

MAFANIKIO

-Wananchi wanaibua miradi yao wenyewe na kuisimamia.

-Kata na Vijiji  vyote vimepata wawakilishi wao katika vikao mbalimbali.

-Wananchi wameelewa wajibu wao katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

 

Changamato

-Hali ya uitishwaji na mahudhurio kwenye vikao ngazi ya chini ni dhaifu hasa wakati         msimu wa kilimo

-Wananchi kutokuwa na utamaduni wa kusoma mbao za matangazo

 

2.1.4 MAENDELEO YA JAMII (JINSIA, WATOTO NA RUSHWA) 2006/2007

 

JINSIA NA WATOTO

Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Ibara ya 17.1 ambayo ni kuelekeza nguvu katika kuwezesha wananchi ili waweze kujiajiri mijini na vijijini, kulikuwa na malengo yafuatayo kwa mwaka 2006/2007:

 

MALENGO

Kwa kipindi cha mwaka 2006/2007 malengo yalikuwa kufanya utambuzi wa watu wanaoishi katika mazingira magumu mfano; watoto, wazee, walemavu na wanawake kwa lengo la kupata takwimu sahihi na kuwawezesha kuanzisha miradi midogo midogo ili kumudu maisha yao wenyewe. Pia kutekeleza sera ya jinsia na maendeleo

 

MAFANIKIO

1.      Kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali mfano UNICEF na taasisi za kifedha zinazowezesha jamii, zoezi la kutambua watoto wanaoishi katika mazingira magumu lilifanyika pamoja na uundaji wa kamati za kuwahudumia. Jumla ya watoto 350 walisajiriwa.

2.       Halmashauri inatekeleza sera ya jinsia kila wakati inapofanya zoezi la kuajiri watumishi.

 

 

CHANGAMOTO

 

Kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika mazingira magumu na ufinyu wa rasilimali (fedha)  bado nguvu kubwa inahitajika ili kupunguza umaskini  uliokithiri miongoni mwa jamii.

 

MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

MALENGO

 1. Kufanya mikutano na wananchi kuwaelimisha juu mapambano dhidi ya rushwa.
 2. Kuanzisha klabu za wapinga rushwa shuleni.

 

MAFANIKIO

1.         Katika kupambana na rushwa, Halmashauri imeteua Afisa ambaye anashughulika na masuala yote yanayohusiana na rushwa.

2.         Halmashauri kwa kushirikiana na TAKUKURU imeanzisha klabu za wapinga Rushwa  na kuizuia madawa ya kulevya katika shule za Sekondari ili kuwaelimisha vijana kutojihusisha katika vitendo vya Rushwa na madawa ya kulevya.

3.         Taasisi ya kupambana na kuzuia  Rushwa  imekuwa ikifanya Mikutano na Wananchi kwa minajiri ya kuwaelewesha haki zao za kimsingi, na namna wananchi wanavyotakiwa kutoa taarifa pale ambapo wanahisi kuwepo na mianya au dalili za rushwa.

4.        Aidha Zabuni zote zinazotolewa katika kutekeleza Miradi mbali mbali   hupitia ngazi husika na kubandikwa kwenye mbao za matangazo ili kuwa na uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji wa pamoja.

 

 

CHANGAMOTO

 1. Elimu zaidi juu ya Rushwa inahitajika kwakuwa wananchi wana uelewa mdogo juu ya aina mbalimbali za rushwa.
 2. Wanachi bado wanahofu ya kutoa taarifa sahii juu rushwa kwa kuhofia usalama wao na kukosa baadhi ya haki fulani katika jamii

 

 

UTEKELEZAJI WA MKUKUTA NA ILANI YA UCHAGUZI 2005

 

2.2 MALENGO, MAFANIKIO NA CHANGAMOTO 2007/2008

2.2.1 UKUAJI WA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI WA KIPATO

 

2.2.1.1 KILIMO/MIFUGO 2007/2008

 

Katika wilaya ya Hai kuna hekta 46,506 zinazofaa kwa kilimo. Wilaya ina watu 183,712 ambao wanahitaji tani 50,291.16 za wanga na tani 5,029.11  za utomwili. Uzalishaji ulikuwa tani 62,917 za wanga na 4,635 za utomwili. Kulikuwa na ziada ya vyakula vya wanga kwa wakazi wa ukanda  wa juu wanaozalisha ndizi. Upungufu wa utomwili uilifidiwa na mazao ya mifugo mfano nyama, maziwa, mayai na mbogamboga. Katika ukanda wa tambarare kulikuwa na upungufu wa chakula kwa vatu 64,848 ambao walihitaji tani 4,438 za wanga na tani 443 za utomwili.

 

Katika kukabiliana na tatizo hili wilaya ilipewa chakula cha msaada kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya vijiji 16 vilivyokuwa na upungufu. Tani 165.5 zilikuwa ni za kuuza kwa bei ya soko na tani 151 kwa bei ya Sh. 50 kwa kilo. Pia Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa Sh. 2,718,000 kwa ajili ya kuchukua tani 151 kutoka SGR – Arusha hadi wilayani.

 

Katika mwaka wa 2007/2008 Halmashauri ilipata TSh 15,998,400  kwa matumizi ya kawaida na TSh.203,576,692/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo, kujenga uwezo wa wadau mbalimbali na shughuli za ugani.

 

 

MALENGO:

 

i)                    Mwaka 2007/2008 wilaya ililenga kulima jumla ya hekta 68,120 za mazao ya chakula msimu wa masika, vuli na umwagiliaji na kuzalisha jumla ya tani 186,280 za chakula.

ii)                  Kuendeleza na kutunza hekta 12,655 za kahawa na kuzalisha tani 1,543.9

iii)                Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji

iv)                Kuongeza tija katika mazao ya chakula na biashara

v)                  Kuboresha afya ya mifugo

vi)                Kuwajengea uwezo wadau mbalilmbali wa sekta ya kilimo na mifugo

vii)              Kuboresha huduma za ugani

 

 

UTEKELEZAJI:

 

i)Jumla ya hekta 66,980 za mazao ya chakula zililimwa katika misimu ya masika, vuli na umwagiliaji na kuvuna tani 246,275 za chakula

 

ii)Jumla ya hekta 12,655 za kahawa ziliendelea kutunzwa na kuzalisha tani 2,568.9

 

iii) Ukarabati wa Mfereji mmoja ulikarabatiwa  kwa TSh. 20,000,000/= na kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta  120 hadi hekta 230. Kumekuwa na ongezeko la uzalishaji ndizi, kahawa na mbogamboga na hatimaye kipato na lishe bora.

 

iv) Miradi 2 ya ufugaji bora wa kuku yenye thamani ya TSh. 2,000,000 ilitekelezwa hivyo kuwa na ongezeko la mayai kutoka 70 hadi 95 kwa kuku kwa mwaka.

 

 • Miradi 7 ya kilimo bora cha mahindi, mpunga na maharage yenye thamani ya TSh.11,826,000/= ilitekelezwa. Kumekuwa na ongezeko la uzalishaji mahindi kutoka tani 1.5 hadi tani 3.5 kwa hekta na mpunga kutoka tani 4 hadi tani 6 kwa hekta.

 

 • Miradi 2 ya kilimo bora cha mboga mboa yenye thamani ya TSh. 2,070,000/= ilitekelezwa. Kumekuwa na ongezeko la uzalishaji mbogamboga kutoka tani 3 hadi tani 5 kwa hekta.

 

 • Mradi mmoja wa kilimo bora cha migomba wenye thamani ya TSh. 1,437,000 ulitekelezwa. Kumekuwepo ongezeko la ndizi kutoka tani 15 hadi tani 20 kwa hekta.

 

 • Miradi ya kilimo bora cha kahawa 6 yenye thamani ya TSh. 13,631,276/= ilitekelezwa.Uzalishaji wa kahawa umeongezeka kutoka tani 1,543.9 mwaka 2006/2007 hadi tani 2,568.9 mwaka 2007/2008.

 

v) Josho moja lenye thamani ya TSh. 9,550,724/= limejengwa.

 

vi) Pikipiki 4, baiskeli 20, vitendea kazi na shajala vilinunuliwa kwa wagani pamoja na mafunzo kwa wagani, vyama ushirika na kamati za miradi yalitolewa kwa gharama ya TSh. 64,060/729/= . Regista ya wakulima imetayarishwa na wakulima 26,200 walifikishiwa utaalam wa uzalishaji mazao mbalimbali na ufugaji.

 

vii) Mafunzo ya kilimo bora cha mazao mbalimbali na ufugaji bora yalitolewa kwa gharama ya TSh.77,430,967/=.

 

 • Pembejeo zenye ruzuku:

Mahitaji ya mbolea na mbegu kiwilaya yalikuwa tani 4,375 za mbolea na tani  366.5 za mbegu bora. Wilaya ilipata tani 824 za mbolea na tani  15.65 za mbegu zenye ruzuku na kuzisambaza kwa wakulima kupitia mawakala 28.

 

Mahitaji ya dawa za kuogesha mifugo aina mbalimbali yalikuwa lita 7,000. Wilaya ilipata lita 790 za dawa aina ya tikfix na kutumika kwenye majosho 4 na wafugaji 56 wanaotumia mabomba ya mikono.

 

 • Katika kupambana na viwavijeshi wilaya ilipatiwa lita 2,974 za dawa kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa na Ofisi Afya ya mimea Kanda ya Kaskazini.

 

 

Changamoto:

 • Kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi na pembejeo
 • Bei ndogo ya mazao kwa wakulima hususan kahawa
 • Magonjwa katika mazao mfano ubwiri mweupe katika alizeti
 • Mashambulizi ya viwavijeshi
 • Mafuriko
 • Chakula cha msaada cha kuuza kwa bei ya soko hakikunufaisha walengwa wengi kutokana na bei kuwa kubwa
 • Pembejeo zenye ruzuku zilizopatikana zilikuwa kidogo kulinga na mahitaji na zilichelewa kupatikana kwa mawakala wa wilaya

 

2.2.1.2 VIWANDA NA BIASHARA 2007/2008

 

VIWANDA

 

Katika utekelezaji wa MKUKUTA na Ilani ya Uchaguzi kama inavyotuelekeza katika ukurasa wa 36 Ibara ya 36, Wilaya ya Hai kwa mwaka wa 2007/2008 ilikuwa na malengo yafuatayo:

 1. Kuongeza viwanda vidogo vidogo kutoka kumi tano hadi ishirini
 2. kutambua eneo la mpango wa uanzishwaji wa viwanda (EPZ).

 

 

 

MAFANIKIO

1.      Vikundi ambavyo vimeanzia viwanda vidogo vidogo vya usindikaji vimeongezeka kutoka 15 hadi 20

2.      Katika kutambua eneo la mpango wa uanzishwaji wa viwanda (EPZ), Wilaya imetoa eneo lenye ukubwa wa hecta 463 sawa na ekari 1144 kwa ajili ya zoezi hili na tayari taratibu za mazungumzo zimeanza baina ya wakazi wa eneo husika ili wapewe fidia na kupisha mradi wa EPZ uanze rasmi. Pia EPZ makao makuu wameridhia mradi huo kuanzishwa Wilayani Hai kutokana na miundo mbinu iliyopo.

 

 

 

 

CHANGAMOTO

 1. Uhaba wa ardhi
 2. Ufinyu wa bajeti
 3. Kiwanda cha “Tanzania Machine Tools” kutofanya kazi yake sawa sawa na hivyo kuathiri soko la ajira.

 

 

BIASHARA

 

MALENGO

Katika kipindi cha 2007/2008 malengo yalikuwa kuongeza utambuzi wa wafanyabiashara na lesseni za biashara ili kuongeza mapato ya Halmashauri. Hali ya biashara katika Halmasahuri ya Wilaya ya Hai  ilikuwa kama ifuatavyo:-

 

 

 

KIPINDI

 

IDADI YA WAFANYA BIASHARA WALIOKUWEPO

 

LESENI MPYA ZILIZOTOLEWA WAFANYA BIASHARA (WAPYA)

2007/08

1198

81

 

MAFANIKIO

Kwa mwaka huu wafanyabiashara wameongezeka kufikia 1198, ongezeko hilo limwesababiswa na ongezeko la lesseni mpya 81

 

CHANGAMOTO

1.      Ufinyu wa bajeti.

2.      Wafanyabiashara wengi kutolipia lasseni zao za biashara kwa wakati.

3.      Katika mwaka  wa Fedha 2007/08 Halmashauri iligawanyika na kuwa Halmashauri mbili ya Siha na Hai hivyo kusababisha idadi ya wafanyabiashara kupungua toka 1766 hadi 1198. Punguo hilo limesababisha kupungua kwa mapato ya lesseni za biashara katika kitengo cha biashara.

 

2.2.1.3 MALIASIRI, MAZINGIRA NA ARDHI 2007/2008

Malengo:

Kwa mwaka wa 2007/2008 malengo katika Ardhi Maliasili na uhifadhi wa mazingira yalikuwa kama yalivyoonyeshwa hapo juu.

 

Bajeti:

SEKTA

2007 – 2008

 

H/SHAURI

RUZUKU

JML

Ardhi

10,998,734

-

10,998,734

Maliasili

20,200,970

-

20,200,970

 

Utekelezaji:

Utekelezaji ulikuwa kama ifuatavyo:-

 1. Elimu ya ufugaji Nyuki imetolewa kwa Vikundi 8, Chama cha Ushirika kimoja na Watu Binafsi.
 2. Doria 6 zimefanyika katika maeneo yenye Wanyama Pori.
 3. Halmashauri imeshiriki katika upandaji miti katika maeneo yaliyotengwa ya hifadhi
 4. Wananchi wameelimika kutumia Maliasili zilizopo ikiwemo Miti iliyopandwa katika maeneo yao [ Miti ya Kigeni na Asili ] , kwa kujengea na kuuza.
 5. Watu wanatumia asali  nta kujipatia kipato na matumizi mengineyo.
 6. Jumla ya miti 1,170,000 ilipandwa ambapo ni sawa na 78% ya 1,500,000 kwa mwaka kiwilaya kwa kuhusisha wadau mbalimbali.
 7. Watu Binafsi na Vikundi wanazalisha miche ya miti na matunda na kuuza.   Mche mmoja wa miti huuzwa kuanzia Tshs. 200/= hadi 2,000/=.

 

Mafanikio

  1. Kiwango cha ufugaji nyuki na uzalishaji mazao yake kimeongezeka.
  2. Kiwango cha ujangili kimepungua, taarifa za matukio ya wanyamapori wakali/waharibifu zinafika kwa wakati.
  3. Wananchi wameelimika kutumia maliasili zilizopo ikiwemo miti iliyopandwa katika maeneo yao kwa kujengea na kuuza.

 

 

Changamoto

 1. Uhaba wa watumishi,
 2. Uhaba wa vitendea kazi,
 3. Ufinyu wa Bajeti,
 4. Ukosefu wa ardhi huru kwa upimaji wa viwanja Mjini Hai.

 

2.2.1.4 USHIRIKA

MALENGO KWA MWAKA 2007/2008

 

·        Kuhamasisha wananchi kujiunga na vyama vya ushirika

·        Kuhamasisha wananchi kuanzisha vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS)

·        Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na ukaguzi wa mwisho katika vyama vya ushirika

·        Kutoa mafunzo kwa wanachama wa vyama vya ushirika

      

               BAJETI

Ili kufanikisha malengo haya, Halmashauri ya Wilaya ilitenga jumla ya Tshs:         9,683,830.00. toka DADPs na Tshs: 4,683,830.00 toka mapato ya ndani ya Hamashauri.

 

       UTEKELEZAJI

·         Elimu ya ushirika ilitolewa kwa wanachama 720 katika vyama vya ushirika 55.

·        Ukaguzi wa kawaida ulifanyika kwa vyama 5, na ukaguzi wa mwisho ulifanyika kwa vyama 26

·        Mikutano mikuu ya vyama vya Ushirika ilifanyika kwa vyama vyote 67

 

       MAFANIKIO

 

·        Hadi kufikia mwishoni mwaka 2007/2008 wanachama  2,079 waliongezeka, kutoka wanachama 25,804 hadi kufikia wanachama 27,883

·        Vyama vya ushirika wa Akiba na mikopo (SACCOS) viliongezeka toka vyama vya Akiba na mikopo (SACCOS) 20 hadi vyama 25  

·        Wanachama wa SACCOS waliongeza hisa zao kufikia  Tshs: 336,115,613.00, waliongeza akiba zao hadi kufikia            Tshs: 985,146,249.00, amana ziliongezeka kufikia                       Tshs: 288,945,873.00 na mikopo iliyotolewa kwa wanachama      Tshs: 1,334,823,331.00 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2.2.1.5 MASHAMBA MAKUBWA 2007/2008

MALENGO 2007/2008

 • Mashamba yote 18 yawe na wawekezaji
 • Wawekezaji waweze kufufua zao la kahawa
 • Kufanya vikao na wawekezaji ili kufanya marekebisho ya mikataba.

 

MAFANIKIO

·        Mashamba 17 yalikuwa na wawekezaji

·        Ongezeko la ajira kwa wananchi

·        Baadhi ya wawekezaji walianza kulipa kodi ya pango

CHANGAMOTO

 • Baadhi ya wawekezaji huwakodishia wananchi kwa ajili ya kilimo cha mahindi
 • Baadhi ya wawekezaji kutolipa kodi ya pango kwa vyama vya ushirika
 • Baadhi ya wawekezaji hulima mazao mengine badala ya kahawa.
 • Baadhi ya mikataba haikufuata taratibu na sheria za vyama vya ushirika

 

2.2.1.6 BARABARA 2007/2008

 

MALENGO YA  MATENGENEZO YA BARABARA KWA MWAKA WA FEDHA WA 2007/2008:-

Matengenezo  ya kawaida ya  (km.96 )

matengenezo ya  sehemu  korofi (km 22)

matengenezo ya muda maalum   (km 8)

kuimarisha madaraja na   makalvati

usimamizi na matengenezo ya gari la barabara,

radi wa Usafirishaji wa Serikali za Mitaa (Local Government Transport  Programme – (LGTP)

 

Katika mwaka wa fedha 2007/08 Halmashauri ya Wilaya ya Hai ilitarajia kutengeneza jumla ya km. 130 kwa gharama ya Tshs. 228,858,000/= kutoka mfuko wa barabara na Mradi wa Usafirishaji wa Serikali za Mitaa (Local Govt. Transport Programme – LGTP) na utekelezaji ulikuwa kama ifuatavyo:- Mfuko wa barabara zilitolewa kiasi cha Tshs. 185,350,000/= na kutumika kutengeneza km. 126 ambapo km. 96 ni matengenezo ya kawaida kwa TShs. 86,950,000/=, km. 8 ni matengenzo ya muda maalum  kwa TShs. 46,400,000/=, km. 22 ni matengenezo ya maeneo korofi kwa TShs. 25,2000,000/=, makalvati na  madaraja yalitengenezwa kwa TShs. 15,200,000/=, usimamizi na  matengenezo ya gari la barabara. TShs. 11,600,000/=.

 

 

Aidha zilitolewa TShs. 24,693,455/= kati ya makisio ya TShs. 43,508,000/= kutoka Mradi wa Usafirishaji wa Serikali za Mitaa (Local Government Transport  Programme – LGTP) na kutumika kutengeneza km. 1 kwa kuinua tuta la barabara ya Bomang’ome – Kikavu chini(eneo la Cheki Maji Kawaya), kwa TShs. 20,600,000/=, kutengeneza  makalvati vipande 14 ( 600 mm dia.x 14m.)  TShs. 420,000/= na kukusanya na kuandaa takwimu za barabara za Wilaya kwa TShs. 3,673,455/=

 

Mapato haya ni sawa na asilimia  55 ya kazi ya lengo lililokusudiwa (LGTP) na asilima 100 kwa mfuko wa barabara.

 

 

MAFANIKIO  KWA MWAKA 2007/2008

 

Halmashauri ya Wilaya ya Hai inapata mafanikio makubwa kwa kuboresha miundo mbinu mbalimbali kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya barabara kila mwaka (Road Fund) na vianzia mbali mbali na kufanya barabara nyingi kupitika wakati wote.

Barabara kupitika kwa wakati wote kumepunguza kero na adha ya usafiri na usafishaji wa mazao mbalimbali ya wananchi kutoka mashambani kwenda nyumbani na masoko mbalimbali ya ndani na nje ya Wilaya.

 

CHANGAMOTO

Halmashauri ya Hai inafanya juhudi kubwa ya kuendeleza kuboresha miundo mbinu lakini bado kuna baadhi ya wananchi wa korofi wanarudisha nyuma juhudi hizo kwa kupitisha maji barabarani wakati wanamwagilia mashamba yao,kufukia mifereji ya kuzuia/kutolea maji yasiende barabarani, wanaiba alama/samani za barabara, wanaweka matuta barabarani bila utaratibu wa kiutaalam, wanaharibu kingo za mito kwa kuchimba mawe na michanga hivyo kuhatarisha misingi ya madaraja, wanaswaga/kupitisha mifugo barabarani wakati wa kupeleka malishoni au kurudisha nyumbani.

 

 

 

2.2.2       UIMARISHAJI WA HUDUMA ZA JAMII

2.2.2.1 MAJI

UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI MWAKA 2007/08

Malengo:- 

-         Kupeleka huduma ya maji katika Kijiji cha Tindigani, Mtakuja,na Kwatito.

-         Kupeleka huduma  ya maji vijiji vitatu vya Kata  ya Machame Mashariki.

-         Kutoa elimu  juu ya sera ya maji ya Taifa.

-         Kuendesha kongamano la  utunzaji na usafi  wa mazingira katika mji wa Hai.

 

Skimu ya maji ya Kijiji cha Mtakuja.

Gharama za mradi: Mradi huu umegharimu Tshs. 84,000,000/= ambazo zimetolewa na Serikali kuu.

 

Utekelezaji: Kazi zilizotekelezwa katika mradi huu ni ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita 50,000 pamoja na ununuzi wa bomba na viungio umbali wa 1.2km.

 

Mafanikio: Utekekelezaji wa mradi umefikia asilimia 40.  Mradi utaendelea kujengwa kwa kutumia wataalam washauri wa Mradi wa Maji Safi na usafi wa mazingira.

 

Skimu ya Maji Lyamungo:

Gharama za mradi: Mradi huu umegharimu Tshs. 1.2 billion ambazo zimetolewa na Seriklai ya Ujerumani (KFW) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

 

Utekelezaji: Kazi zilizotekelezwa katika mradi huu ni ujenzi wa tawi la maji umbali wa 14km, Ujenzi wa vilula 8 na matanki mawili ya kuvunja msukumo wa maji.

 

Mafanikio: Kazi imekamilika na jumla ya wananchi 3500 na wanafunzi 260 wanapata huduma ya maji Safi na Salama.

 

Maadhimisho ya  wiki ya maji  ya taifa

Gharama: Maadhimisho ya wiki ya maji mwezi Machi  mwaka 2008  yamegharimu Tshs. 1,200,000/= ambazo zimetolewa na wadau wa maji.

 

Utekelezaji:

Sera ya maji imeelimisha katika vijijiji vitatu.

Kamati za maji zimeundwa katika vijiji viwili

Jumla ya wadau  sitini katika kata ya Hai Mjini wameelimishwa kuhusu utunzaji wa mazingira.

 

 

Mafanikio:

Uelewa wa sera ya maji ya Taifa na athari za uchafu wa mazingira.

 

Skimu ya maji ya Kijiji cha Tindigani

Gharama za Mradi:

Mradi huu umegharimu Tshs. 40,000,000/= ambazo zimetolewa na Serikali kuu

 

Utekelezaji:

Ununuzi wa bomba  umbali wa km 4.5, kuchimba mtaro na kufukia bomba  umbali wa km.4.5 pamoja na ujenzi wa vilula vitatu.

 

Mafanikio:  Jumla ya wananchi 1112 na wanafunzi 336 wanapata huduma ya maji safi na salama.

 

CHANGAMOTO

Kuwezesha upatikanaji wa huduma ya maji Safi na Salama katika umbali wa mita 400 kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2012 ambapo malengo ya MKUKUTA ni asilimia 65 na Milenia 74% (2015).

Kushirikisha wananchi ili kupinga kwa nguvu zote biashara ya vyuma chakavu kwani inasababisha kuibiwa kwa miundombinu ya miradi ya maji.

Kuelimisha wananchi ili kuondoa imani kuwa huduma ya maji ni bure.

Kushirikisha sekta nyingine za kijamii ili kuelimisha wananchi madhara ya uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.

 

MIKAKATI

Kukarabati skimu ya Maji Machame na kuanza ujenzi wa skimu ya Maji Mkalama chini ya mradi wa maji Hai District Water Supply Project awamu ya nne rudio la pili. Kushirikiana na wataalam washauri wa Miradi ya Maji na usafi wa mazingira (NRWSSP) watakaoteuliwa ili kuwezesha ujenzi wa mradi katika vijiji tisa vya ukanda wa chini wa Wilaya kuanzia mwezi Januari 2009.

Kuendelea kutoa elimu kuhusu sera ya maji ya Taifa (2002).

 

 

 

2.2.2.2 AFYA

Mwaka 2007/2008

Katika kipindi cha mwaka 2007/2008 idara iliidhinishiwa jumla ya Tsh. 1,731,521,294/= kati ya fedha hizo jumla ya Tshs. 1,003,411,912/= zilitumiwa kukamilisha kulipa mishahara ya watumishi na kiasi cha Tshs. 708,588,280/= matumizi ya kawaida. 

 

MIRADI YA MAENDELEO

Idara iliidhinishiwa kiasi cha Tsh. 19,521,102/= ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

 

Malengo:

 1. Kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi toka watoto 98/100,000 wanaozaliwa hai hadi watoto 97/100,000.
 2. Kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa kujenga Zahanati maeneo ambayo yalikuwa mbali na huduma hizo mfano Zahanati za Kikavu chini, Shirimgungani, Mbataketo, na Mtakuja.
 3. Kununua samani kwa ajili ya vituo 2 vya kutolea huduma.
 4. Ujenzi wa vyoo katika vituo 2 vya kutolea huduma.
 5. Ukarabati wa vituo 5 vya kutolea huduma ambavyo ni:-

-         Hospitali ya Wilaya ya Hai.

-         Kituo cha Afya Masama 

-         Kituo cha Afya Kisiki

-         Zahanati ya Weruweru.

-         Zahanati ya KIA

 

 

Utekelezaji:

 1. Vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi vimepungua toka 44/100,000 hadi 40/100,000 vya watoto waliozaliwa hai.
 2. Vifo vya watoto wachanga chini ya mwaka mmoja vimepungua toka vifo 93/1000 hadi 92/1,000.
 3. Ujenzi wa Zahanati ya Kikavu chini na Shirimgungani zimekamilika.
 4. Samani kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma zimenunuliwa.
 5. Ujenzi wa vyoo katika vituo 2 vya kutolea huduma zimekamilika.

 

Mafanikio:

 1. Kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma karibu na jamii.
 2. Hali ya usafi katika vituo vya kutolea huduma vimeboreka.

 

Changamoto:

 1. Wakina mama hasa jamii ya Kimasai hawapendi kujifungulia kwenye vituo vya huduma licha ya mahudhurio mazuri ya kliniki ya wajawazito.
 2. Mfumuko wa bei  umesababisha  kupanda bei kwa vitu.

 

MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Kwa mwaka wa 2007/2008 yafuatayo yalilengwa

 1. Kuwahamasisha wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuunda vikundi katika kata zao ili waweze kusaidiwa kwa urahisi.
 2. Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi umuhimu wa kupima Afya zao kwa hiari.
 3. Kuanzisha vituo 5 na vya upimaji wa hiari na kutibu magonjwa nyemelezi kwa waathirika wa UKIMWI na utoaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ambavyo ni Hospitali ya Wilaya ya Hai, Machame, Kisiki, Nkwansira, na Masama.
 4. Kujenga jengo la kutoa matibabu na malezi kwa waathirika wa UKIMWI.
 5. Jumla ya fedha zilizoidhinishwa na Halmashauri ni Tsh. 41,798,631.

 

Utekelezaji:

1.      Vikundi vya wanaoishi na virusi vya UKIMWI vimeundwa katika Kata zote 10 za Wilaya.

2.      Tulipima jumla ya watu 24,551 kati ya lengo la kupima watu 22,829 hivyo kuvuka lengo kwa 107.5%.

3.      Jengo limejengwa na kukamilika.

 

Mafanikio:

 1. Huduma za kusaidia wanaoishi na virusi vya UKIMWI zinapatikana kwa karibu.
 2. Wananchi wamekubali kupima afya zao kwa kiwango kikubwa ambapo maambukizi yamepungua kutoka 5% mpaka 2%.
 3. Wananchi wamepata huduma za matibabu na malezi kwa karibu.

 

Changamoto:

 1. Bado kuna baadhi ya wanaoishi na Virusi vya UKIMWI ambao hawataki kujiunga kwenye vikundi.
 2. Upungufu wa wataalam wa watoa ushauri nasaha.

 

Mkakati:

-         Kuendelea kutoa elimu ya faida za kujiunga na vikundi kwa wale bado.

-         Kushirikiana na wadau mbalimbali kuomba fedha za kutoa mafunzo kwa Wataalam wa Afya.

 

 

 

 

 

 

2.2.2.3            ELIMU

 

MALENGO, MAFANIKIO NA CHANGAMOTO 2007/2008

 

Kulingana na malengo ya MKUKUTA na ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005 kwa upande wa Elimu ililenga yafuatayo:-

 

 1. Uandikishaji wa watoto wote wenye umri wa miaka 7
 2. Kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliofaulu Elimu ya Sekondari wanajiunga kidato cha kwanza.
 3. Kuhakikisha kwamba watoto wote waliokosa Elimu ya Msingi wanasajiliwa
 4. Kuwapatia Elimu watoto wenye mahitaji maalum.

 

BAJETI YA IDARA YA ELIMU:

 

MAELEZO

2007/2008

YA KASMA

 

 

 

MAKISIO

MATUMIZI

PE & OC

5,377,819,935.00

5,412,608,344.74

MMEM CAP

211,635,000.00

197,846,956.00

MMEM DEV

528,106,020.00

-

 

 

Utekelezaji wa malengo kwa  Halmashauri ya Wilaya ya Hai:

 

Ø      Uandikishaji  wa wanafunzi:

Ø      Elimu ya Awali:

 Idadi ya wanafunzi waliandikishwa katika  madarasa ya Awali ni

                Wav: 2028        Was: 1875      Jml: 3903

 

 

Ø      Elimu ya Msingi.

Katika swala la uandikishaji,wa wanafunzi wa darasa la kwanza tumeandikisha watoto wote wenye wenye umri wa miaka 7 na kuondoa mlundikano wa waliozidi  umri wa miaka saba waliostahili kuandikishwa shule ya msingi kama inavyooneshwa  katika Jedwali lifuatalo.

 

 

Uandikishwaji  wa wanafunzi  darasa la I

 

MWAKA

WALIOATARAJIWA

WALIOANDIKISHWA

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

%

2007

3175

2739

5914

2766

2595

5361

90

2008

2657

2522

5179

2716

2475

5191

100

 

 

 

Ø      Ufaulu  wa wanafunzi na kujiunga na kidato cha kwanza

Ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka 2007/2008 ni kama unavyoonekana katika Jedwali

 

 

MWAKA

WALIOFANYA

WALIOFAULU

WALIOPATA NAFASI

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

%

WAV

WAS

JML

%

2007

2425

2399

4822

1083

1267

2350

48.73%

1083

1267

2350

100%

2008

2980

3092

6072

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 • Wanafunzi waliotegemewa kufanya mtihani mwaka 2008 ni  6151 wakiwemo

Wavulana 3038  Wasichana  3113.  Waliofanya mtihani ni 6072 sawa na  asilimia 98.7%.  Tunatarajia wanafunzi 5465 watakaofaulu ambao ni sawa na asilimia 90.

 

 

Ø                  Kusajiliwa kwa wanafunzi wote waliokosa Elimu ya Msingi:-

Kwa mwaka wa 2007/2008 wanafunzi walioandikishwa kwa mpango wa MEMKWA ni kama inavyoonekana katika Jedwali.

 

 

UANDIKISHAJI WA MEMKWA

 

MWAKA

WALIOANDIKISHWA

 

KUNDI RIKA I

KUNDI RIKA II

JUMLA 

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

2007

22

15

37

-

-

-

22

15

37

2008

22

11

33

 

 

 

 

 

 

 

 

MAFANIKIO: MWAKA  2007/ 2008

 

b.      Kumekuwa na ongezeko la miundo mbinu katika kupunguza msongamano wa wanafunzi – darasa I wanafunzi 40 – 50. Dawati  1 wanafunzi 2 – 3.

c.      Shule nyingi zimeboresha mazingira hasa uoteshaji wa miti ya kivuli, uzio (sawa na shule 68 kati ya shule 103) sawa na asilimia 66%.

d.      Walimu wamejiendeleza katika programu ya MUKA na waliobaki ni walimu daraja B/C ambao ni 35 kati ya walimu 539 sawa na asilimia 6.4

e.      Ujenzi wa visima vya kuvuna maji.  Hadi sasa vimejengwa visima  35 kati  ya vituo 103 sawa na asilimia 32%.

 

Changamoto katika Elimu ya Msingi 2007/2008

 

(i)                 Baadhi ya familia kuwaficha  baadhi ya watoto wenye kuhitaji Elimu maalum.

(ii)               Miundo mbinu kutokukamilika kwa wakati kutokana na mfumuko wa bei na kipato cha wananchi.

(iii)             Idadi ya watoto wanaoandikishwa na wanaomaliza kutofautiana hasa maeneo ya wafugaji.

(iv)              Ujenzi wa kituo kikuu cha Wilaya cha walimu kwa ajili ya kuendesha  mafunzo na semina mbalimbali.

(v)                Kutokana na eneo la shule kuwa finyu miundo mbinu mingine inashindikana kuwepo shuleni – mfano nyumba za walimu , maktaba, bwalo la chakula, viwanja vya michezo n.k.

(vi)              Ujenzi wa shule ya waalemavu ya Wilaya (Multipurpose Centre)

(vii)            Vituo vya Ufundi vina uhaba mkubwa wa vifaa na upungufu wa walimu wa fani za ufundi

               

 

ELIMU YA  SEKONDARI: 2007/2008

Wilaya ya Hai ina shule 40 za Sekondari zikiwemo 27  za Serikali na 13 binafsi. Shule za Serikali zina wanafunzi 8202 kati yao Wavulana 3746 na Wasichana 4456.

 

MALENGO

Mwaka 2007 na 2008 lengo ni kuongeza vyumba vya madarasa  26.

 

 

MAFANIKIO:2007/2008

 

 1. Shule 10 zimepata maeneo ya ujenzi
 2. Upatikanaji wa fedha za TASAF, LCDG na MMES umeongeza kasi ya ujenzi na upanuzi wa Sekondari  (TASAF Tshs. 336,546,541/= LGDG Tshs 44,000,000/=na MMES  Tshs,. 170,000,000/=).   Fedha kutoka mfuko wa TASAF umejenge vyumba 39 vya madarasa.

 

CHANGAMOTO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI 2007/2008

 

 1. upungufu wa majengo ya utawala katika shule za sekondari 19
 2. upungufu wa nyumba za walimu katika shule 12
 3. upungufu wa maabara katika shule za Sekondari 23
 4. Upungufu wa mabwalo katika shule za sekondari 24
 5. Upungufu wa maktaba katika shule za Sekondari 25
 6. Baadhi ya wananchi kutochangia mipango ya Elimu ya Sekondari ambayo inasababishwa na kipato duni
 7. Mfumuko wa bei za vifaa vya ujenzi
 8. Upungufu wa walimu
 9. Maeneo ya kujenga miundo mbinu ya sekondari yamekuwa haba kutokana na ufinyu wa ardhi.

 

 

2.2.3 UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI 2007/2008

Kwa mwaka 2007/2008 vikao vya ngazi ya Wilaya vilifanyika kwa asilimia 100,  ngazi ya Kata (WDC), asilimia 77.5, mikutano mikuu ya vijiji na asilimia 55.4, vikao vya Halmashauri za vijiji asilimia 69 na mikutano ya vitongoji asilimia 51, kama inavyoonekana katika Jedwali.

 

JEDWALI

NA

MKUTANO/VIKAO

VILIVYOTARAJIWA

VILIVYOFANYIKA

ASILIMIA

1

Mikutano ya Halmashauri

4

4

100

2

Vikao vya Maendeleo ya Kata (WDC)

40

31

77.5

3

Mikutano mikuu ya Vijiji

220

122

55.4

4

Vikao vya serekali ya Vijiji

660

456

69

5

Vikao vya Vitongoji

3084

1573

51

 

 

 

 

 

2.2.3.1            MAENDELEO YA JAMII (JINSIA, WATOTO NA RUSHWA)

 

 

JINSIA NA WATOTO

Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Ibara ya 17.1 ambayo ni kuelekeza nguvu katika kuwezesha wananchi ili waweze kujiajiri mijini na vijijini, kulikuwa na malengo yafuatayo kwa mwaka 2007/2008 kwa upande wa jinsia na watoto:

 

MALENGO

Kwa kipindi cha mwaka 2007/2008 malengo yalikuwa kuendelea kufanya utambuzi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kutekeleza sera ya jinsia na kuendelea kuwezesha makundi ya wajasiriamali kutoka vikundi tisini hadi 180 ifikapo mwaka 2008

 

MAFANIKIO

(i)                 Wilaya imefanikiwa kupata takwimu za watoto waishio katika mazingiara magumu na hatarishi kutoka kata zote kumi. Jumla ya watoto hao ni 7,392.Me 3873 na Ke 3509. Uhamasishaji wa kuandaa mipango ya kuwezesha watoto hao umefanyika katika vijiji vyote 55 na kila kijiji kimefungua akaunti kwa ajiri ya kuwawezesha watoto hao kutokana na taratibu walizojiwekea wenyewe.

(ii)                Vikundi vimeongezeka kwa lengo la kuunganisha nguvu na kujikwamua kiuchumi kutoka tisini hadi 228 hivyo kuvuka lengo tulilojiwekea

(iii)             Halmashauri inatekeleza sera ya jinsia kila wakati inapofanya zoezi la kuajiri watumishi.

CHANGAMOTO

 

(i)                 Kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika mazingira magumu na ufinyu wa rasilimali (fedha)  bado nguvu kubwa inahitajika ili kupunguza umaskini  uliokithiri miongoni mwa jamii.

(ii)               Idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi inabadilika mara kwa mara kwa sababu ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa UKIMWI, madawa ya kulevya na wazazi wenye vipato duni.

(iii)             Idadi watu wanaotakiwa kusaidiwa ni kubwa ukilinganisha na ufinyu wa bajeti iliyopo.

 

MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

MALENGO

(i)                 Kufanya mikutano na wananchi kuwaelimisha juu mapambano dhidi ya rushwa.

(ii)               Kuendelea kuanzisha klabu za wapinga rushwa shuleni.

 

MAFANIKIO

(i)                 Katika kupambana na rushwa, Halmashauri imeteua Afisa ambaye anashughulika na masuala yote yanayohusiana na rushwa.

(ii)               Halmashauri kwa kushirikiana na TAKUKURU imeendelea kuanzisha klabu za wapinga Rushwa  na kuzuia madawa ya kulevya katika shule za Sekondari ili kuwaelimisha vijana kutojihusisha katika vitendo vya Rushwa na madawa ya kulevya.

(iii)             Taasisi ya kupambana na kuzuia  Rushwa imeendelea kufanya  Mikutano na Wananchi kwa minajiri ya kuwaelewesha haki zao za kimsingi, na namna wananchi wanavyotakiwa kutoa taarifa pale ambapo wanahisi kuwepo na mianya au dalili za rushwa.

(iv)              Aidha Zabuni zote zinazotolewa katika kutekeleza Miradi mbali mbali   zimeendelea kupitishwa ngazi husika na kubandikwa kwenye mbao za matangazo ili kuwa na uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji wa pamoja.

 

CHANGAMOTO

1.Elimu zaidi juu ya Rushwa inahitajika kwakuwa wananchi wana uelewa mdogo juu ya aina mbalimbali za rushwa.

2.Wanachi bado wanahofu ya kutoa taarifa sahii juu rushwa kwa kuhofia usalama wao na kukosa baadhi ya haki fulani katika jamii

 

 

 

3.0 MWELEKEO NA MPANGO WA BAJETI 2008/2009 KATIKA                  UTEKELEZAJI WA MKUKUTA NA ILANI YA UCHAGUZI 2005

 

3.1 UKUAJI WA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI WA KIPATO

3.1.1 MWELEKEO KATIKA SEKTA YA KILIMO/MIFUGO 2008/2009

 

Katika wilaya ya Hai kuna hekta 46,506 zinazofaa kwa kilimo. Wilaya ina watu 183,712 ambao wanahitaji tani 50,291.16 za wanga na tani 5,029.11 za utomwili. Uzalishaji ulikuwa tani 80,550 za wanga na 7,500 za utomwili mwaka 2007/2008. Kutakuwepo ziada ya chakula 2008/2009. Wakulima wanaendelea kushauriwa kuhifadhi chakula na kutokuuza nje ya nchi.

 

Idara ya Kilimo/Mifugo imekasimiwa TSh. 455,250,000/=  kwa matumizi ya kawaida na mishahara na TSh. 500,689,374/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo, kujenga uwezo wa wadau mbalimbali na shughuli za ugani.

 

MALENGO:

 

Mwaka 2008/2009 wilaya imelenga kulima jumla ya hekta 68,120 za mazao ya chakula msimu wa masika, vuli na umwagiliaji na kuzalisha jumla ya tani 186,280 za chakula. Wilaya itahitaji tani 7,800 za aina mbalimbali za mbolea na tani 803 za mbegu bora ya mahindi. Mahitaji ya dawa za kuogesha mifugo aina mbalimbali ni lita 7,000.

 

i)                    Kuendeleza na kutunza hekta 12,655 za kahawa na kuzalisha tani 2,600

ii)                  Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa gharama ya TSh. 110,879,750/=

iii)                Kufufua zao la kahawa kwa gharama  Tsh. 4,000,000

iii)        Kuongeza tija katika mazao ya chakula kwa gharama TSh.16,080,000

iv)        Kuboresha afya na uzalishaji mifugo kwa gharama ya TSh. 125,011,723/=

iv)                Kuwajengea uwezo wadau mbalilmbali wa sekta ya kilimo na mifugo kwa

            gharama ya TSh. 166,911,752

vi)        Kuboresha huduma za ugani kwa gharama ya TSh. 66,814,224/=

 

UTEKELEZAJI:

 • Wilaya ilipata lita 250 za dawa aina ya Cypermethrin  ambayo itatumika kwenye majosho 5 na  kwa wafugaji wenye mabomba

 

 

 

3.1.2 VIWANDA NA BIASHARA

MWELEKEO WA VIWANDA 2008/2009

 1. Kuhakikisha kuwa Kamati Endeshaji iliyoundwa Wilayani kuhusiana na mpango wa EPZ inapata mafunzo ya uzoefu nchi jirani hususan Kenya Athiriver.
 2. Pia kuhakikisha kuwa wananchi waliopo katika eneo linalotegemewa kuanzisha mradi wanapata fidia, kama EPZ makao makuu watawezesha fedha kama walivyoahidi.
 3. Kuendeleza viwanda vidogo vidogo vilivyoanzishwa na vikundi vya kiuchumi ili viweze kukuza kipato na kuinuka kiuchumi.

 

MWELEKEO WA BISHARA 2008/2009

 1. Kuendelea kutambua wafanyabiashara walioko Wilayani hai.
 2. Kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ili waanzishe viwanda vidogo vidogo vya usindikaji
 3. Kuwaunganisha wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali za kifedha ili waweze kuwezeshwa

 

3.1.3 MALIASILI, MAZINGIRA NA ARDHI

MWELEKEO

Mwenendo na mwelekeo wa kufanikisha malengo na makusudio ya 2008/2009 ni kama ifuatavyo:

 

 1. Kuboresha ikama kwa kuajiri ama kuhamishia watumishi/wataalam katika Wilaya nyingine.  Sekta zinazohusika zaidi ni Misitu, Nyuki, Ardhi, Uvuvi na Wanyamapori.
 2. Ununuzi wa vyombo za usafiri kama pikipiki, gari na vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi za kitalam na kuboresha ofisi.
 3. Bajeti iongezwe kuwezesha na kukuza ufanisi wa kitaalam kutekeleza malengo.
 4. Kutafuta maeneo ya kufidia toka jamii inayozunguka Mji wa Hai ili kuboresha na kukuza Mji.

 

3.1.4 USHIRIKA

MALENGO KWA MWAKA 2008/2009

 

·        Kuendesha mafunzo ya awali ya uhasibu kwa SACCOS 40

·        Kuendesha mafunzo ya mbinu ya kutafuta masoko kwa SACCOS 40

·        Kuendesha mafunzo kwa vyama vya msingi 65 juu ya urekebishaji wa sheria ndogondogo(Bylaws) kulingana na sheriaya ya vyama vya vyama  ushirika ya mwaka 2003.

·        Ukaguzi wa kawaida kwa vyama vya ushirika 6

·        Ukaguzi wa mwisho katika vyama 65

         

Kwa mwaka wa fedha 2008/2009  Halmashauri imeomba kibali  ili kuajiri maafisa Ushirika wawili.

 

 

3.1.5 MWELEKEO MASHAMBA MAKUBWA 2008/2009

 

MALENGO 2008/2009

 • Mashamba yote 18 yawe na wawekezaji
 • Wawekezaji waweze kufufua zao la kahawa
 • Kufanya vikao na wawekezaji ili kufanya marekebisho ya mikataba

 

 

MPANGO WA BAADAYE

 • Kupitia upya mikataba hiyo na kufanya marekebisho

 

3.1.6 MWELEKEO WA BARABARA 2008/2009

 

Kwa mwaka wa fedha 2008/09 Halmashauri ya Wilaya ya Hai inatarajia kupata

Tshs. 359,600,000/= kutoka mfuko wa barabara na Mradi wa Usafirishaji wa Serikali za Mitaa (LGTP) kwa ajili ya  kuimarisha  km. 218.6 za barabara za Wilaya.  Kati ya fedha hizo kiasi cha Tshs. 243,600,000/= zitatoka mfuko wa barabara (Road Fund) kwa ajili ya matengenezo ya  km. 189.6 ambapo kati ya kilometa hizo km. 170.6 zitafanyiwa matengenezo ya kawaida kwa Tshs. 127,970,000/=, km. 14 zitafanyiwa matengenezo ya maeneo korofi kwa TShs. 22,700,000/=, km. 5 zitafanyiwa  matengenezo ya muda maalum kwa Tshs. 60,000,000/=,  ujenzi wa makalvati zitatumika Tshs. 15,000,000/= na kwa ajili ya usimamizi na matengenezo ya gari la barabara zitatumika

TShs. 18,000,000/=.

 

Pia Halmashauri ya Wilaya inatarajia kupokea na kutumia Tshs. 116,000,000/= kutoka Local Government Transport Programme (LGTP) kwa ajili ya matengenezo km. 29 za maeneo korofi za barabara mbalimbali  za Wilaya ya Hai na kujenga  makalvati yenye kipenyo cha ( 600 mm.x  168 m.) au line 24  zenye urefu wa  mita 7 kila moja.

 

MIKAKATI

Viongozi wa ngazi zote wahamasishe wananchi/wadau ili waweze kuelewa kuwa barabara ni sehemu ya mali yao na waweze kuitunza na kama ikitokea uharibufu wowote ule watoe taarifa haraka kwa uongozi wa juu ili tatizo hilo litatuliwe mapema iwezekanavyo.

Halmashauri ya Wilaya ya Hai kwa kutumia kitengo chake cha sheria itatunga sheria ndogo (BY LAW) kwa ajili ya utunzaji wa barabara za Wilaya

 

3.2 UIMARISHAJI WA HUDUMA ZA JAMII

 

3.2.1 UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI MWAKA 2008/09

Malengo:

Kupeleka huduma ya maji katika vijiji sita vya kata ya Machame Kaskazini.

 

Kuanza kwa mradi wa  maji safi na usafi wa mazingira  katika vijiji tisa vya ukanda wa chini wa Wilaya ya Hai.

 

Kuboresha huduma ya maji katika vijiji saba  vya mradi wa maji Losaa Kia.

 

Skimu  ya maji Machame

Gharama za Mradi

Mradi huu utagharimu EURO 2.1 million  ambazo ni sawa na Tshs. Billion 4  za Tanzania . ambazo zimetolewa na Serikali ya ujerumani ( KFW) kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania

 

Utekelezaj:

Kazi ya mradi imeanza mwezi  Julai 2008.  Ujenzi wa vyanzo  vitatu vya maji umefikia  asilimia 50.

 

Matarajio:  Mradi  ukikamilika jumla ya vijiji sita vitapata maji safi na salama

 

Mradi wa maji safi na usafi wa mazingira (NRWSSP)

 

Gharama za Mradi:

Gharama za mradi ni Tshs. 380,892,000/= ambazo zitatolewa na benki ya dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

 

Utekelezaj:

Mchakato wa kumpata  mkandarasi mshauri wa mradi  umefanyika na  watashindanishwa wawili baada ya kupata kibali  cha benki ya dunia.

 

Matarajio:

 Utekelezaji rasmi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Januari 2009.

 

Skimu ya maji ya kijiji cha Sanya station.

Gharama za mradi: Mradi huu umegharimu Tshs. 42,530,000/= ambazo zimetolewa na Serikali kuu.

 

Utekelezaji: Ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita 50,000 na  ujenzi umefikia asilimia 50.  Kazi ya ujenzi inaendelea.

 

Skimu ya maji katika vijiji vya Mudio, Nkwansira, Nguni, Isuki, Mungushi na Mborenyi.

 

Gharama za mradi: Gharama za ununuzi wa bomba na viungio vyenye  urefu wa 4.050km ni Tshs. 22,447,000/=.

 

Utekelezaji: Kazi ya ulazaji bomba  umbali wa km 4.050 inaendelea.

 

Matarajio:  Kazi hiyo ikikamilika  idadi ya wananchi 9,000 watapata huduma ya maji safi na salama.

 

3.2.2 MWELEKEO WA AFYA 2008/2009

Katika kipindi cha mwaka 2008/2009 Wilaya imeomba jumla ya Tshs.2,455,246,807.80 kati ya hizo Tshs. 1,223,351,908.80 zitatumika kulipia mishahara ya watumishi wa Sekta ya afya. Fedha hizo ni sawa na ongezeko la asilimia 50.28 katika bajeti ya mwaka 2007/2008.  na Tsh. 1,195,894,899 kwa matumizi ya kawaida. Fedha zilizoombwa zitatumika kuendeshea shughuli 144 kama ilivyoanishwa kwenye mpango kabambe wa afya wa Halmashauri.

 

 

MIRADI YA MAENDELEO

Idara iliidhinishiwa kiasi cha Tsh. 36,000,000/= ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

Malengo:

 1. kukarabati tanuru la kuchomea taka  Hospitali ya Wilaya.
 2. Kukarabati vituo 5 vya kutolea huduma.
 3. Kujenga chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya.
 4. Kupunguza matukio ya magonjwa yasiyoambukiza kuto 3% - 2% ifikapo mwaka 2009.

 

Mkakati:

1.      Kukamilisha chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Wilaya.

2.      Kujenga chumba cha upasuaji na X-ray Hospitali ya Wilaya.

3.      Kupatikana kwa gari maalumu la kubebea wagonjwa wa hospitali ya Wilaya.

4.      Kufanya ukaguzi wa kila kaya ili kuhakikisha kuwa na choo cha kudumu.

 

3.2.3 MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Mwelekeo 2008/2009:

Katika mwaka wa Fedha 2008/2009 jumla ya Tshs 59,309,000.00 zimeidhinishwa toka Hazina kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbali mbali za UKIMWI zikiwa ni:-

 1. Kutoa mafunzo kwa Wataalam kwa watoa Ushauri nasaha katika Kata 10.
 2. Kutoa mafunzo kwa watoa huduma za kifua kikuuu katika Kata 10 juu ya upimaji wa hiari.
 3. Kukagua vituo vya upimaji hiari katika Wilaya.

 

Mkakati:

Idara itahakikisha malengo yaliyopangwa yatatekelezwa kikamilifu na kuendelea na uhamasishaji wa wananchi kuhusu upimaji wa hiari wa Afya zao.

 

3.2.4 ELIMU MWELEKEO WA BAJETI KWA MWAKA WA 2008/2009

Katika mwelekeo wa bajeti kwa mwaka wa 2008/2009 fedha zilizoteidhinishwa kutoka hazina ni kama ifuatavyo ; CDG Tsh 110,000,000/= Ujenzi MMEM TSh 24,430,000/= na Matumizi ya kawaida Tsh 408,078,000/=. 

 

Halmashauri inayo mkakati wa kuongeza vyumba vya madarasa kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2009.  Pia tunao mkakati wa kuhakikisha kwamba shule zote zenye upungufu wa madarasa na matundu ya vyoo yanajengwa.

 

MWELEKEO WA BAJETI YA IDARA YA ELIMU 2008/2009:

 

MAELEZO

2008/2009

YA KASMA

 

 

MAKISIO

PE & OC

5,278,186,835.00

MMEM CAP

226,000,000.00

MMEM DEV

24,430,000.00

 

 

 

 

ELIMU YA UFUNDI:

 

Wilaya ina Kituo 1 kipya kinachotarajiwa kuanza mwaka 2009 Januari.              

 

 

      3.3 UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI

       .MWELEKEO NA MPANGO  2008/2009

Kwa mwaka  2008/2009,  tunatarajia vikao na mikutano yote ya kisheria ifanyike kwa mujibu wa ratiba, kwani hadi mwezi Septemba 2008, vikao na mikutano iliyotakiwa kufanyika imefanyika kwa mujibu wa ratiba, katika ngazi za Kata na Vijiji.

 

-Halmashauri imeweka mpango madhubuti wa kuwalipa wenyeviti wa vijiji na vitongoji posho zao kwa wakati na imeshalipa kiasi cha shilingi 22,000,000/- ili kuwahamasisha viongozi hao kufanya kazi zao vizuri hasa uitishwaji wa vikao katika maeneo yao.

 

 -Kiasi cha Tshs 7,581,740.00 kitatolewa toka katika ruzuku ya kujenga uwezo kwa ajili ya kukuza demokrasia katika Ngazi za Vijiji na Kata kwa kutoa mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji & Vitongoji, Watendaji wa Vijiji na Kata, [CBG] kati ya jumla ya Tshs 37,906,700.00 zilizoidhinishwa 2008/2009, kiasi hiki ni asilimia 28% ukilinganisha na Tshs 5,079,232.00 kati ya Tshs 25,396,160.00 ambacho kilikuwa  20% ya fedha zilizoidhinishwa mwaka 2007/2008.

 

3.3.1 MAENDELEO YA JAMII (JINSIA, WATOTO NA RUSHWA)

Wilaya itaendelea kukuza sera ya jinsia na watoto kama inavyotekelezwa na Halmashauri. Wilaya itaendelea kupambana na Rushwa kwa kushirikiana na TAKUKURU kama ilivyokuwa inafanya kwa miaka ya nyuma.

 

 

3. 4 UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI

MWELEKEO WA BAJETI 2008/2009

Bajeti kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumikwa mwaka 2008/2009 katika ngazi ya Halmashauri ni shilingi 17,752,000/=.

 

Malengo

Malengo ya idara ni haya yafuatayo:-

1.      kuendelea kuwajengea uwezo viongozi wa vijiji ili kutekeleza sera za Maendeleo ya Jamii.

 

2.      Kuendelea kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu kwa kushirikiana na mashirika mbalimbaliyanayotoa misaada kwa makundi hayo.

 

3.      Kuendelea kutoa mikopo kwa vikundi ili kuwawezesha kiuchumi na kuongeza kipato chao.

 

4.      Kuhuisha takwimu za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

 

5.      Kuratibu shughuli mbalimbali zinazofanywa  na mashirika yasiyo ya kiserikali ndani ya wilaya  kwa lengo la kupunguza umasikini na kuongeza pato la wananchi.

 

Tunatarajia kutekeleza malengo haya ili kuweza kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kujiajiri wenyewe ili kujiongezea kipato na kuondokana na dhana tegemezi. Hii itasaidia kuondokana na umaskini unaoikabili jamii.

 

4.0 HITIMISHO

Hayo hapo juu ndiyo yaliyofanywa na wilaya katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya  mwaka 2005.