| KILIMO | UMWAGILIAJI | MIFUGO |  
   
Rudi nyumbani
................................................................................................................................. ................................................................................................................................. .................................................................................................................................
         
 
UTANGULIZI
 
 
Bi. H. MKAMBA
Afisa Kilimo - Sekretarieti ya Mkoa
 
 
Kilimo huchangia zaidi ya asilimia 60 ya Pato la Mkoa (RGDP). Zaidi ya asilimia 75 ya wananchi huishi vijijini wakitegemea kilimo kwa mahitaji yote ya maisha yao.
 
Eneo linalofaa kwa kilimo ni km mraba 6433 , sawa na hekta 643,300. Eneo linalolimwa kwa mwaka ni karibu hekta 400,000. Matumizi ya ardhi mkoani ni kama ifuatavyo.
 
BONYEZA HAPA kuona matumizi ya ardhi
 
 
Zao la Ndizi
 
Ndizi ni chakula kikuu kwa wakazi wa mkoa huu. Zao hili hulimwa pamoja na kahawa. Zipo aina nyingi zenye majina ya kienyeji kwa kupika, kutengeneza pombe ya kienyeji na kula mbivu. Ingawa zao hili limelimwa mkoani kwa muda mrefu uzalishaji kwa ujumla ni mdogo, wastani wa tani 12 kwa hekta ukilinganisha na uzalishaji katika utafiti ambao ni tani 40 – 70 kwa hekta. Tatizo kubwa ni aina zilizopo, ukame, wadudu, magonjwa na kutozingatia kanuni za utunzaji. Mkoa una zaidi ya hekta 70,000 za migomba. Aina mpya za migomba zikiwepo pazi, williams na grandnine zenye uzalishaji mkubwa na soko zimeshaanza kuingizwa mkoani na zinaendelea vizuri.
 
Maharagwe
 
Maharagwe hulimwa zaidi mchanganyiko na mahindi na ni zao muhimu kabisa linalowapatia protini wananchi wengi. Pamoja na hayo uzalishaji wake ni wa chini usiotosheleza mahitaji ya protini ya mkoa. Mahitaji ya protini husaidiwa na protini kutokana na wanyama.
 
 
Katani
 
Zao la katani au mkonge linalimwa katika mashamba makubwa maeneo ya tambarare za Mwana na Same. Wilayani Same zao la mkonge limelimwa tangu mwaka 1960 katika mashamba makubwa yaliyokuwa yanamilikiwa na Mamlaka ya Mkonge na Karimje Jivanjee LtdJ. Kuna mashamba mawili makubwa:-
 
•  Shamba la Ndungu - Ha 1084  
•  Shamba la Makanya - Ha 2400
 
Mashamba yote mawili yameuzwa kwa wawekezaji. Kwa sasa shamba la Ndungu linamilikiwa na Lupindo Investment Ltd. alilolinunua toka kwa Mamlaka ya Mkonge Tanzania mwaka 1998. Malengo ya mwekezaji ni kupanda upya hekta 180 kila mwaka.
 
Shamba la Makanya lilinunuliwa na Mohamed Enteprises Ltd. toka kwa Karimjee Jivanjee mwaka 1998 na ana lengo la kupanda hekta 100 kila mwaka.
 
Wilayani Mwanga zao linalimwa eneo la Kisangara. Mmiliki wa shamba hili ni Mohamed
Enteprises Ltd. ambaye alilinunua toka kwa
Mkoa umegawanyika katika kanda 4 za kilimo, zikiwepo ukanda wa mlimani, juu, kati na chini/tambarare. Kanda hizo hutofautiana kwa mwinuko unaosababisha utofauti katika hali ya hewa, aina/rutuba ya udongo, aina ya mazao, na hata idadi ya watu kwa eneo.
 
BONYEZA HAPA kuona kanda za kilimo
 
Shughuli za Kilimo Mkoani kimegawanyika katika sehemu kuu tatu:-

•  kilimo cha umwagiliaji ambacho hufanyika mwaka mzima kufuatana na upatikanaji maji lakini zaidi Julai hadi Septemba.

•  kilimo cha vuli ambacho ni muhimu (“main cropping season”) kwa Wilaya za Rombo,Mwanga na Same hufanyika Oktoba hadi Februari;

•  klimo cha masika ambacho ni muhimu (“main cropping season”) kwa Wilaya za Hai, Siha na Moshi, hufanyika Machi hadi Agosti;

Asilimia 80 ya kilimo mkoani hutegemea mvua.
 
Mifumo ya Kilimo (Farming Sytems) zipo 3 kutokana na mwinuko ambao huchangia katika utofauti wa hali ya hewa na udongo. Ukanda wa juu na kati kuna mfumo wa kilimo cha kahawa mchanganyiko na migomba pamoja na ufugaji wa ndani. Sehemu ya chini ya kanda ya kati na ya juu ya ukanda wa tambarare kuna kilimo mchanganyiko wa nafaka na mazao aina ya mikunde na ufugaji wa ndani au nje. Ukanda wa tambarare kuna ufugaji wa kuchunga pamoja na mashamba makubwa ya katani, miwa na kilimo cha umwagiliaji.
 
Udongo ni wa volkaniki na kwa sehemu kubwa una rutuba ila kutokana na mwinuko, mvua nyingi na kilimo kisichozingatia utaalamu rutuba inapungua kutokana na mmomonyoko wa ardhi na mimea kuvuna madini ardhini bila kurudisha “nutrient mining”.
 
Mazao yanayolimwa ni ya chakula na biashara yakiwepo ndizi, mahindi, mpunga, mtama, ulezi, ngano, viazi, mhogo, alizeti, kartamu, mikunde, mboga, matunda, viungo, maua, kahawa, pamba, miwa, katani, shayiri, mlonge na artemisia.
 
Mazao ya chakula
 

Mazao muhimu ya chakula ni mahindi,mpunga, ndizi na maharagwe.

 
Mahindi
 
Mahindi ni zao kuu la nafaka linalolimwa ukanda wa kati na chini. Zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro hutumia mahindi kwa chakula. Uzalishaji wake ni kuanzia tani 3.5 hadi pungufu ya tani 1 kwa hekta kutegemea na hali ya hewa na matumizi ya pembejeo. Aina za mbegu zinazotumika ni chotara, (>50%), mchanganyiko (40%) na kienyeji (10%).
 
Mpunga
 
Zao hili hulimwa kwa umwagiliaji mwaka mzima. Zipo skimu mbili za kisasa za umwagiliaji (Mradi wa Umwagiliaji wa Lower Moshi (1100ha) na Mradi wa Umwagiliaji Ndungu (680 ha). Kwa sababu ya ubora wa miundo mbinu na matumizi ya teknologia uzalishaji umeongezeka kutoka tani 2.0 kwa hekta (kabla ya Mradi) hadi wastani wa tani 6.5/ha sasa. Uwezekano wa kuzalisha hadi tani 10 kwa hekta upo. Teknolojia hiyo imeigwa nje ya eneo la mradi ambapo uzalishaji umefikia tani 4.5 kwa hekta. Uzalishaji wa mpunga kwa mwaka mzima unawezesha kusiwepo na mfumuko wa bei kwa mazao ya chakula (hasa nafaka).
 
Tatizo kubwa la uzalishaji zao hili ni idadi ndogo ya mimea kwa eneo na matumizi ya mbegu za kienyeji.
 
Mazao ya Biashara
 
Mazao makuu ya biashara ni kahawa, pamba,miwa, katani, maua na shayiri. Zaidi ya asilimia 70 ya kahawa na pamba hulimwa na wakulima wadogo, ambapo katani, miwa shayiri na maua hulimwa katika mashamba makubwa na wakulima wakubwa (large scale farms).
 
Kahawa
 
Kahawa ni uti wa mgongo wa maendeleo ya kiuchumi Mkoani Kilimanjaro. Miaka ya nyuma mkoa ulizalisha asilimia 30 – 36 ya kahawa yote ya Tanzania. Mkoa unakisiwa kuwa na hekta 76000 za kahawa. Uzalishaji umekuwa ukipanda na kushuka na katika miaka ya 90 ulishuka toka tani 20586 (ya maganda “parchment”) mwaka 1995/96 hadi kiwango cha chini kabisa cha tani 4600 mwaka 1997/98. Katika jitihada za kufufua zao hili uzalishaji ulipanda hadi tani 11325, lakini kushuka tena hadi tani 3495 msimu 2007/08 kutokana na ukame wa miaka 9 mfulilizo.
 
BONYEZA HAPA kusoma zaidi juu ya kahawa
 
Pamba
 
Pamba ni zao la pili kwa umuhimu linalolimwa na wakulima wadogo. Zao hili hulimwa katika ukanda wa tambarare. Zipo hekta 15867 zinazofaa kwa kilimo cha pamba katika wilaya za Moshi, Mwanga na Same. Kama ilivyo kwa mazao mengine uzalishaji umekuwa ukipungua mwaka hadi mwaka kutoka tani 360 mwaka 1995/96 hadi tani 4 mwaka 2000/01. Uzalishaji umeongezeka kutoka tani 4 mwaka 2000/01 hadi tani 209 mwaka 2006/07 kutokana na jitihada mbalimbali za Bodi ya Pamba na Halmashauri za Wilaya. Tatizo kubwa ni upatikanaji wa soko la uhakika na upatikanaji wa pembejeo.Mkoa umepewa lengo la kuzalisha tani 563 ifikapo mwaka 2010.
 
Miwa
 
Miwa inazalishwa katika shamba kubwa linalomilikiwa na kiwanda cha TPC Ltd. (TPC – Tanganyika Planting Company) lililoko kata ya TPC, wilaya ya Moshi. TPC Ltd. kwa sasa inamilikiwa na mwekezaji M/S Sukari Investment Co. Ltd. ambayo ni ya Mauritius kwa asilimia 75 na asilimia 25 inamilikiwa na Serikali ya Tanzania.
 
Kiwanda cha Sukari TPC kilibinafsishwa kuanzia tarehe 24/03/2000. Wakati wa ubinafsishaji kampuni ya Sukari Investment kwenye mkataba walionyesha watawekeza dola za kimarekani milioni 30 katika kipindi cha miaka mitano. Lengo lilikuwa kuzalisha sukari kiasi cha tani 72,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2005.
 
Kampuni hii imekuwa na jitihada kubwa na uzalishaji sukari umeendelea kukua toka tani 42,003 mwaka 2000/01 wakati wa ubinafsishaji hadi tani 60,503 mwaka 2006/07. Mkoa ulipewa lengo la kuzalisha tani 80,000 ifikapo mwaka 2010. BONYEZA HAPA kusoma hali ya uzalishaji hadi sasa.
 
Uwekezaji katika mashamba na ufungaji mitambo mipya ya kiwanda umefikia dola za kimarekani milioni 69. Pamoja na kuongeza uzalishaji wa sukari, ajira kwa wananchi imeongezeka. Hivi sasa kiwanda kinaajiri wafanyakazi 2,254 wa kudumu na vibarua 1,060.
 
Karimjee Jivanjee Agricultural Ltd. mwaka 1998. Shamba lina eneo la hekta 2,000 . Mwekezaji ana lengo la kupanda upya asilimia 10 ya shamba kwa mwaka.
 
Wakulima wadogo bado hawajahamasika au kuwezeshwa vya kutosha kuweza kuzalisha zao hili japo wawekezaji wako tayari kununua na kusafirisha hadi kiwandani.
 
Shayiri
 
Zao la shayiri linazalishwa na wawekezaji wakubwa wenye mkataba na kampuni ya Bia Tanzania huko West Kilimanjaro. Shayiri hutumika kuzalisha bia na mabaki yake ni chakula cha mifugo. Uzalishaji kwa miaka mitano iliyopita ni kama inavyooneshwa kwenye kiunganishi hiki: BONYEZA HAPA
 
Mazao yasiyo ya asili (Non-traditional crops)
 
Mkoa umekuwa ukihimiza wakulima kulima mazao mengine ya thamani kubwa kwa lengo la kumwongezea mkulima kipato. Mazao hayo ni kama inavyonyesha kwenye kiunganishi hiki: BONYEZA HAPA
 
Mazao mengine yanayohamasishwa ni pamojana rosell, soya, paprika, jatropha, aloevera na karanga miti (macadamia nuts). Changamoto katika mazaohaya yasiyo ya kawaida ni uzalishaji mdogo na ukosefu wa soko la uhakika.
 
Jitihada zinaelekezwa katika kuongeza wingi wa mazao kwa kuhamasisha wakulima wengi zaidi walime mazao hayo kushawishi sekta binafsi kuanzisha viwanda vya kusindika mazao na kutafuta masoko. Kituo cha uwekezaji mkoani kinahamasisha wakulima ili wawekeze katika usindikaji kwa maana ya kuongeza thamani.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Rudi juu   Rudi juu     Rudi juu
.........................................................................................................................................................................................................................................................................................
 
Matatizo Katika Kilimo Malengo ya Kilimo kwa Msimu wa Mwakan2008/09 Kilimo cha Umwagiliaji
Fursa Zilizopo za Kuboresha Kilimo Ununuzi wa Mazao Ramani za Udongo
Mkakati wa Kuboresha Kilimo Upatikanaji & Usambazaji wa Pembejeo za Ruzuku Huduma za Ugani
Utekelezaji wa Malengo ya Kilimo 2007/08 Athari za Mafuriko 2007/08 Miradi ya Kilimo
 
.........................................................................................................................................................................................................................................................................................
 
COPYRIGHT© OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, S.L.P 3070, SIMU: 027 2752184/54236-7, FAX: 027-2753248. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.