| KUTUHUSU | ANUANI ZETU |      
   
Rudi nyumbani
............................................................................................................................................................................................................... ..............................................................................................................................................................................................................
     
 
     
MAELEZO MAFUPI KUHUSU MKOA WA KILIMANJARO
 
Mkoa wa Kilimanjaro uko Kaskazini Mashariki mwa Tanzania Bara. Mkoa unapakana na Jamhuri ya Kenya upande wa Kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa Kusini Mashariki, Mkoa wa Arusha upande wa Mashariki na Mkoa wa Manyara upande wa Kusini Magharibi.
 
Mkoa una eneo lenye Kilometa za mraba 13,209 ambazo zimegawanyika kwa matumizi ya ardhi kama ifuatavyo;-
 
Jedwali na 1: Mgawanyo wa eneo la Mkoa kwa matumizi ya Ardhi:
MATUMIZI ENEO (km. mraba) ASILIMIA(%)
Ardhi inayofaa Kilimo 6,433 48.7
Hifadhi ya wanyama 3,051 23.1
Mbuga za Malisho 2,018 15.3
Misitu 1,403 10.6
Maji 304 2.3
Jumla 13,209 100%
 
Mkoa una wilaya 6 za utawala ambazo ni Hai, Siha, Rombo, Moshi, Mwanga na Same ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo;-
 
Jedwali na 2: Mgawanyo wa Utawala:
Wilaya Idadi ya Tarafa Idadi ya Kata Idadi ya Vijiji
Same 6 25 83
Mwanga 5 16 60
Hai 3 10 55
Siha 1 4 30
Rombo 5 20 60
Moshi 4 31 145
Manispaa 2 15 Mitaa 60
Jumla 26 121 433
Mitaa 60
 
IDADI YA WATU KWA MUJIBU WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012
 
Mkoa una jumla ya watu wapatao 1,640,087 (Kwa mujibu wa Sensa ya 2012). Kati yake wanaume ni 793,140 na Wanawake ni 846,947. Makisio ya mwaka 2006 mkoa una watu 1,466,052 katika mgawanyiko kiwilaya. Kama jedwali linavyoonyesha kwa sensa ya 2012 na makisio ya mwaka 2006, BONYEZA HAPA
 
HALI YA SIASA
 
(A) VYAMA
 
Mkoa umeimarika katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Aidha, katika mkoa vipo vyama vipatavyo 9, navyo ni CCM, CHADEMA, TLP, NCCR Mageuzi, CUF, UDP, Demokrasia Makini. Democratic Party na PPT.
 
 
(B) RUSHWA
 
Katika Mkoa wa Kilimanjaro suala la Rushwa linaendelea kupigwa vita katika taasisi za Serikali na maeneo mbalimbali yanayotoa huduma kwa wananchi. Jumla ya taarifa 113 zimepokelewa na Taasisi ya kuzua rushwa (TAKURU) na kufanyiwa uchunguzi.
 
TAKURU Mkoani Kilmanjaro inafanya juhudi kutoa elimu kwa umma. Kwa kipindi cha Januari hadi aprili, 2007 mafunzo yametolewa kwa polisi, Waaendaji wa Kata pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari. Vile vile katika mikuano iliyoshirikisha wananchi takribani 1,415.
     
 
   
 
MAAFA
 
Katika kipindi cha mwaka 2006/2007 kumekuepo na maafa mbalimbali yaliyotokea katika Mkoa wa Kilimanjaro. Maafa hayo yalisababishwa na upeopo mkali mafuriko, moto, ajali za barabara na maporomoko ya ardhi. Maafa haya yalitokea Wilaya ya Moshi, Wilaya ya Same, Wilaya ya Hai, Wilaya ya Mwanga na Manispaa ya Moshi.
 
 
UHARIBIFU ULIOTOKANA NA MAAFA :
 
(A) MAFURIKO :
 
Jumla ya hekta 690.6 za mazao ya mahindi, maharage, nyanya, tikitimaji, hoho vyenye thamani ya shs.141,465,000 ziliharibiwa katika Wilaya ya Moshi, Wilayani Same watu 130 waliathrika na mafuriko, ekari 80 za mahindi ziliharibiwa katika Kata ya Ndugu, uharibifu ulikuwa na thamani ya shs.28,340,000/= Shirika la CARITAS lililoko Same lilitoa msaada wa chakula tani 3.2 kwa wananchi walioathrika.
 
(B) UPEPO MKALI
 
Wilaya tatu ambazo ni Hai, Same na Mwanga zilikubwa na upeopo mkali katika kipindi cha mwezi Februari mwaka 2007, ambapo nyumba za watu binafsi majengo ya shule za sekondari na chuo cha ufundi, mifugo na miti viliharibika. Uharibifu huu katika wilaya ya Hai ulikadiriwa kugharimu hasara ya shilingi 340,834,600/=.
 
 
(C) MATUKIO YA MOTO :
 
Yamekuwepo matukio ya moto katika mkoa wa Kilimanjaro hususani katika Manispaa ya Modhi na Modhi Vijijini. Usiku wa tarehe 24/3/2007 moto uloizuka kwenye eneo la soko kuu na kuunguza vibanda 81 vya wajasiriamali mbalimbali wa Mjini Moshi, hata hivyo moto uloizimwa na kikosi cha zimamoto wakisaidiana na zima moto toka TPC. Yamekuwepo pia matukio ya moto katika kiwanda cha sukari TPC. Matukio hayo yamesababisha hasara kubwa kwa kiwanda hicho. Uchunguzi wa kubaini chanzo cha motgo na sababu za matukio hayo yanayojirudia rudia unaendelea kufanywa na vyombo husika.
 
MWELEKEO WA MKOA
 
Mkoa wa Kilimanjaro umelenga kufanya kazi zenye matokeo kwa walengwa na kuwa Taasisi inayoongoza kwa kuzisaidia na kuzijengea uwezo Serikali za Mitaa kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi na waeja wengine.

 
MAJUKUMU YA MKOA
 
  1. Kuratibu na kusimamia utekelezaji Sera zilizoainishwa na Wizara/Sekta mbalimbali za Serikali.
  2. Kusimamia utawala bora kwa H/Wilaya na jamii
  3. Kufuatilia na Kutathmini miradi ya maendeleo ya H/Wilaya na Mkoa kwa ujumla
  4. Kutoa ushauri kwa sekta na miradi husika ikiwa ni pamoja na kutafuta wawekezaji ili kuinua uchumi wa wananchi na mkoa kwa ujumla.
 
 
MASUALA YA UTUMISHI
 
Watumishi walioajiriwa katika utumishi wa umma na mashirika mbalimbali hapa mkoani yanaendelea kutoa huduma nzuri kwa wadau mbalimbali. Hata hivyo kuna upungufu wa wafanyakazia katika Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro. Watumishi wanaotakiwa ni 800 kwa sasa watumishi waliopo ni 652. Watumishi wapatao 33 wamepata ajira mpya, hadi sasa kuna nafasi zilizowazi 123 ambazo zinahitaji kujazwa. Kati ya hizo nafasi sita (6) zimachwa wazi kutokana na kustaafu kwa mujibu wa sheria.
 
 
 
CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WATUMISHI:
 
Sekta ya Afya hapa mkoani ndiyo yenye uhitaji wa watumishi wengi. Nafasi ziliztangazwa lakini kumekuwa na shida ya kupata watumishi wenye sifa zinazohitajika. Kwa mfano kupata Madaktari Bingwa, wataalamu kama vile Mpima Ardhi (Land Surveyor), Manasheira wa Sekretariet ya Mkoa na Senior Medical Officers ya mkoa.
 
Kwa taarifa zaidi za kisekta tembelea sekta husika kwa kubonyeza viunganishi vilivyoko kwenye ukurasa wa nyumbani BONYEZA HAPA
 
    Rudi juu
.........................................................................................................................................................................................................................................................................................
 
COPYRIGHT© OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, S.L.P 3070, SIMU: 027 2752184/54236-7, FAX: 027-2753248. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.