FEDHA NA HESABU
   
Rudi nyumbani
................................................................................................................................. ................................................................................................................................. .................................................................................................................................
         
 
UTANGULIZI
 
 
Bi. Regina Mutagurwa
Mhasibu Mkuu
 
Mkoa wa Kilimanjaro mpaka kuishia mwezi Septemba, 2008 una jumla ya Vyama vya Ushirika 424, vilivyochanga, jumla ya Hisa zenye thamani ya Tshs. 2,757,015,699/=. Miongoni mwa vyama hivyo vya ushirika vya Msingi ni 421, vilivyochanga jumla ya Hisa zenye thamani ya Tshs. 2,148,975,454/=.
 
Katika idadi hiyo ya Vyama vya Ushirika “SACCOS” ni 204 na zilizochanga jumla ya Hisa zenye thamani ya Tshs. 1,973,612,959/= na Akiba zilizowekwa zenye thamani ya Tshs. 7,677,202,429.45. Kuna Vyama Vikuu vya Ushirika viwili (2) ambavyo ni “Kilimanjaro Native Co-operative Union (1984 ) Ltd” (KNCU 1984) Ltd. na VUASU (1984) Ltd.” . Aidha Mkoa una Benki ya Ushirika iitwayo “Kilimanjaro Co-operative Bank Ltd (KCBL), zenye jumla ya Hisa zenye thamani ya Tshs. 608,940,245/=.
 
1.0 Malengo ya mwaka:
 
(i) Uhamasishaji wananchi ili kuelewa na kuona umuhimu wa kujiunga na kuanzisha vyama vya ushirika 35 vya aina mbali mbali zikiwemo “SACCOS” katika maeneo ambayo hayana vyama vya ushirika.
 
(ii) Ufufuaji wa vyama sinzia 66 , uimarishaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika 312.
 
(iii) Ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika 378 mkoa wa Kilimanjaro.
 
•  Ufuatiliaji na utatuzi wa migogoro ya Vyama vya ushirika 81.
 
1.1 Utekelezaji:
 
(i) Kumekuwepo na ongezeko la vyama vya ushirika hasa “SACCOS” kutoka vilivyokuwepo 2005/2006 vyama vya Ushirika 356 hadi kufikia 378.
 
(ii) Ongezeko la Vyama vya Ushirika ni 22, “SACCOS” zikiwa ni 19 na vyama aina nyingine ya ushirika ni 3.
 
(iii) Vyama vya Ushirika vilivyokaguliwa ni 136 kati ya lengo la 378.
 
(iv) Migogoro 27 ya vyama vya ushirika imesuluhishwa.
 
Mafanikio:
 
(i) Wananchi waliojiunga na SACCOS wameweza kupata mikopo na kuongeza kipato.
 
(ii) Wananchi wamejenga imani na vyama vyao na kuongeza mitaji baada ya kukaguliwa.
 
•  Changamoto:
 
•  Ukosefu wa elimu endelevu ya ushirika unakwamisha uwezo wa wananchi kujijenga kiuchumi. Wanachama/wanaushirika wanahitajika kupatiwa elimu ya ushirika na Biashara ili kuviwezesha vyama hivyo kujiendesha kibiashara na kujijengea uwezo wa kiuchumi kwa lengo la kujitegemea.
 
•  Wanachama waanzilishi wa vyama kutotaka kuingiza wanachama wapya.
 
•  Malengo ya mwaka 2007/2008:
 
•  Uhamasihsji na uandikishaji wa vyama vya ushirika na hasa “SACCOS” kufuatia mpango wa serikali wa uwezeshaji wananchi kiuchumi.
 
•  Mafanikio:
 
•  Ongezeko ni kutoka vyama vya ushirika 378 msimu 2006/2007 hadi kufikia vyama vya ushirika 403 na hivyo kuwa na ongezeko la Vyama vya Ushirika 25 – “SACCOS” zikiwa ni 19 na vyama aina nyingine vya ushirika ni 6.
 
•  Changamoto:
 
Maeneo mengi ambayo Vyama vya Ushirika vimeanzishwa ni kufuatia kuitikia wito wa serikali kuhusiana na uhamasihsaji wa serikali wa uwezeshaji wananchi kiuchumi.
 
(ii) Vyama hivyo vinahitajika kuwa na usimamizi na uendeshaji mzuri chini ya wananchi waliopata elimu ya ujasiriamali, biashara na ushirika ili kuendana na sera ya ushirika yenye lengo la uimarishaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika.
 
(iii) Ongezeko la Vyama vya Ushirika katika mkoa wa Kilimanjaro haliwiani na idadi ya Maofisa ushirika/wakaguzi wenye wajibu wa kusimamia na kukagua vyama vya ushirika.
 
(iv) Idadi ya maofisa ushirika/wakaguzi walio kazini katika kipindi hicho ni 27 na Ikama za Halmashauri za wilaya na Manispaa zimeonyesha kuwa na upungufu wa Maofisa Ushirika 9 tu.
 
•  Malengo ya mwaka 2008/2009:
 
•  Kuendelea na uhamasishaji, uandikishaji, usimamizi na ukaguzi wa vyama vya ushirika kwa vile vilivyopo na vinavyofanya kazi.
 
•  Kushauri uimarishaji wa mitaji katika Vyama vya Ushirika kwa lengo la kujiendesha kibiashara na kujitegemea.
 
•  Mafanikio.
 
•  Kwa kushirikiana na Idara ya Ushirika katika baadhi ya Halmashauri za wilaya kuna “NGOs” na kampuni zilizojitokeza kufanya shughuli na baadhi ya “SACCOS” kwa makubaliano maalum.
 
•  “NGOs” na kampuni zilizokubaliana na baadhi ya “SACCOS” wamekubali kusaidia mafunzo kwa wajumbe wa bodi, watendaji wa vyama hivyo na wanachama kwa kutoa elimu ya ujasiriamlai, utunzaji wa vitabu vya hesabu na utoaji wa taarifa za hesabu za ushirika. (Kuwajengea uwezo wa kiuendeshaji).
 
•  Baadhi ya NGOs na kampuni wanawasaidia maofisa ushirika/wakaguzi kuwafikisha vyamani kwa ajili ya ukaguzi katika baadhi ya Vyama vya Ushirika hasa “SACCOS”, chache zilizokaguliwa.
 
•  Changamoto:
 
•  Vyama vya Ushirika vya aina mbalimbali na hasa “SACCOs” zimefanikiwa kupata mikopo mingi kutoka kwenye vyombo vya fedha.
 
•  Udhibiti na ukaguzi wa vyama vya ushirika (hasa “SACCOS”) unahitajika sana ili kuzuia ubadhirifu na wizi katika vyama vya ushairika.
 
•  Uchache wa maofisa ushirika/wakaguzi kunasababisha kutokufanyika kazi ya usimamizi na ukaguzsi aidha kwa wakati au kutokufanyika kabisa kwa muda. Jambo hili limepelekea baadhi ya Vyama vya Ushirika hasa “SACCOS” kujiingiza katika ubadhirifu wa fedha hizo na hivyo kusababisha migogoro na kutokuelewana miongoni mwa wanachama.
 
•  Upatikanaji wa vyombo vya usafiri vya kuwawezesha maofisa ushirika/wakaguzi kufika vyamani kwa wakati.
 
BONYEZA HAPA kuona hali ya Uanchama katika Vyama vya Ushirika kuishia Agosti 2008
 
4.0 Vyama Vikuu vya Ushirika na Benki;
 
4.1 Mkoa wa Kilimanjaro una jumla ya Vyama vya ushirika 424, miongoni mwa vyama hivyo, vyama vya Ushirika vya msingi ni 421 na vyama vikuu vya ushirika ni viwili (2) ambavyo ni “Kilimanjaro Native Co-operative Unuion (l984) Ltd. KNCU (l984) Ltd) na VUASU (1984)Ltd. Aidha mkoa una Benki ya ushirika iitwayo “Kilimanjaro Co-operative Bank Ltd (KCBL).
 
•  Malengo:
 
•  Kutoa elimu kwa wanachama wao juu ya kilimo cha zao la kahawa – kilimo bora tangu shambani, kuvuna hadi uuzaji.
 
•  Kutoa elimu ya biashara na ushirika kwa vyama wanachama wao kwa kuzingatia sheria ya ushirika.
 
•  kutafuta masoko bora na kuuza kahawa katika hali ya ubora na kwa bei nzuri kwa manufaa ya mkulima.
 
•  Kutoa huduma ya fedha za kukopesha wanachama; kukuza mitaji; kuendeleza kilimo, ununuzi wa pembejeo za kilimo na ununuzi wa mazao.
 
•  Kuunganisha nguvu, mitaji na kuwa na sauti moja ya ushirika. Kuanzisha na kuendesha miradi na biashara kwa njia ya ushirika.
 
•  Kutoa na kuendesha huduma za kijamii kwa wanachama wao kwa kadri ya uwezo wa kila chama kikuu cha ushirika.
 
4.3 Mafainikio :
 
(i) Vyama vikuu vya ushirika vyote vitatu (3) vinakaguliwa na kusoma hesabu zao kwa wanachama wao kila mwaka.
 
 
(ii) KNCU (1984) Ltd, ina mradi wa Utalii HAKI na wanasomesha watoto wa wanachama wao kupitia baadhi ya vyama vya ushirika wanachama wao.
 
(iii) KNCU (1984) Ltd. wamesaidia baadhi ya vyama wanachama wao “CPA” (Kiwanda cha kati cha kusindika kahawa) kwa ajili ya kutoa ubora wa juu na ubora unaofanana kwa vyama vyote vya ushirika wanachama wake.
 
(iv) “KCBL” msimu wa 2006/2007 ilifanikiwa kuzalisha ziada ya Tshs. 61,496,686/= ambazo wanachama wake waliazimia kuongeza thamani ya Hisa zao ili kukuza mtajiwa benki yao.
 
(v) “KCBL” imeanzisha huduma ya “WESTERN UNION MONEY TRANSFER”.
 
(vi) Benki ya ushirika kwa kushirikiana na baadhi ya vyama vya ushirika vya msingi vya kahawa vimeanzisha utaratibu wa ‘MFUMO WA STAKABADHI YA MAZAO GHALANI”.
 
4.4 Changamoto:
 
(i) KNCU (1984) Ltd inahitaji kujipanga upya na kuainisha umuhimu wake (provide justification), kwa vyama ambavyo kwa sasa vinafanya biashara nje ya utaratibu wa KNCU.
 
(ii) KNCU (1984) Ltd inahitaji kutafuta njia za kupanua mtaji wake na kupunguza utegemezi wa mikopo ya Benki za Biashara kwa asilimia mia moja (100%) katika kuendesha biashara zake na hasa wakati wa ununuzi wa kahawa.
 
(iii) Vyama vikuu vyote vitatu vinahitajika kuwa makini na waangalifu wanapoingia kwenye mikataba na watumishi, mabenki na kwingineko na baada ya hapo kuheshimu mikataba hiyo.
•  Vyama vikuu vya ushirika vyote vitatu vinalazimika kuweka utaratibu wa kuimarisha mitaji yao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanachama wao kulipia hisa zaidi, sambamba na kujongeza thamani ya Hisa.
•  Vyama vikuu vya ushirika vyote vitatu vinalazimika kujenga tabia ya kulipa madeni yao ndani ya vipindi vya mikatana na kuweka utaratibu wa kulipa madeni ya nyuma.
•  Vyama vikuu vya ushirika vyote vitatu vinalazimika kuimarisha safu zao za uongozi na utendaji pia.
 
(iv) Katika mfumo huu wa uchumi wa soko, vyama vikuuvya ushirika vyote vitatu vina nafasi ya kutumia utaratibu wa “STAKABADHI YA MAZAO GHALANI” kwa manufaa ya wanachama wao.
 
5.0 Mpango wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mkoa wa Kilimanjaro
 
5.1 Malengo ya Mpango 2006/2007 :
 
Lengo kuu la Serikali ni kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi katika sekta zote na kuongeza fursa za ajira kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wajasiriamali na hasa wale wadogo ambao ndiyo walengwa wa kuomba fedha hizo ambazo zitaongeza mitaji yao kwa kupitia Vyama vyao vya Ushirika wa Akiba na Mikopo – “SACCOs”, au vikundi vyao vya Kiuchumi na hata mtu mmoja mmoja.
•  Kuwawezesha wananchi wengi zaidi kushiriki na kunufaika na miradi yao ya kiuchumi kwa lengo la kuongeza kipato na kupunguza umaskini.
 
5.2 Utekelezaji :
 
Katika msimu 2006/2007 Benki za CRDB na NMB ndizo benki pekee zilizotoa mikopo katika kipindi hicho kama ifuatavyo:-
•  CRDB Bank walitoa mikopo kwenye SACCOS 3 yenye thamani ya Tshs. 507,990,000/=.
•  NMB walitoa mikopo kwa wajasiria mali 288 yenye thamani ya Tshs. 272,900,000/=.
 
Taarifa ya utekelezaji wa mpango hadi Juni 2008:
 
•  PRIDE Tanzania Ltd. – tawi la Moshi.
•  Mgawo wao wa Tshs. 100/= umepelekwa Singida kwa makosa.
 
•  Mwanga Community Bank:
•  Fedha ilitolewa kwa SACCOS 2 na wajasiriamali 131 zenye thamani ya Tshs. 67,67,750,000/=
 
•  KCBL – Moshi:
•  Fedha ilitolewa kwa vikundi vya kiuchumi 22 - thamani yake ni Tshs. 174,490,000/=. KCBL mpaka kipindi hicho marejesho yalikuwa Tshs. 4,503,167/=.
 
•  CRDB Bank:
- Fedha iliyotolewa kipindi hicho ni kwa SACCOS 13, zenye thamani ya Tshs. 2,432,305,000/=.
 
•  UCHUMI COMMERCIAL Bank:
- Fedha imetolewa kwa watu binafsi 11 zenye thamani ya Tshs. 73,054,600/=.
 
(ii) Jumla ya mikopo iliyotolewa ni TShs.2,123,865,000'/- kwenye “SACCOs” na vikundi kwa jumla 11 kwa wilaya zote ndani ya M koa.
 
(c) Kumekuwa na ongezeko la vikundi vya kiuchumi vinavyotambulika pia “SACCOs” zilizosajiliwa na kuanza kuendeshwa kibiashara. “SACCOs” zilizokuwepo nyingi zimeimarishwa na kuongeza wanachama na kupanua wigo wa huduma zake. Kwa mfano idadi ya “SACCOs” zilizoandikishwa ziliongezeka kutoka 171 Juni, 2006 hadi kufikia 192 kufikia Desemba, 2007.
 
5.3 Changamoto zilizojitokeza :
 
Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, kulikuwa pia na changamoto zilizojitokeza katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mpango huu. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na:
 
(i) Ngazi ya Mkoa imekuwa Mratibu Mkuu wa Mpango huu bila kufanyiwa maandalizi wala kushirikishwa katika mafunzo ambayo ngazi ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa ilipata.
 
(ii) Kuchelewa kuwa na uelewa wa pamoja juu ya dhana nzima ya mpango wa uwezeshaji ambao ungewafanya viongozi kuwa na lugha moja kuanzia ngazi ya mtaa/kijiji,kata tarafa, wilaya, mkoa na taifa.
 
5.4 Malengo ya mpango 2007/2008:
 
Kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. Kuongeza fursa za ajira kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wajasiriamali hasa wale wadogo.
 
•  Kuwawezesha wananchi wengi kuwa karibu na kutumia huduma za mabenki, kujiunga kwenye vikundi vya kiuchumi na “SACCOS” zinazojiendesha kibiashara.
 
5.5 Mafanikio ya mpango:
 
Mpango huu umeweza kufufua miradi ya uzalishaji ya binafsi na vikundi iliyokuwa imelegalega, mfano wa kilimo cha mpunga Moshi Vijijini na Same – Ndungu, ambayo walichukua mikopo yao kutoka “CRDB”. Wajasiriamali wapatao 509 kupitia NMB walipata mikopo yenye thamani ya Tshs. 599,977,306/=.
 
•  SACCOS sita zilipata mikopo yao kupitia “CRDB Bank” yenye thamani ya Tshs. 1,149,000,000/= SACCOS 38 ziliandikishwa katika kipindi hicho.
 
Ongezeko la vikundi vya kiuchumi vinavyotambulika pia “SACCOS” zilizosajiliwa na kuendeshwa kibiashara. Baadhi ya “SACCOS” zimeimarishwa kiuchumi na kuendelea kuongeza wanachama na kupanua wigo wa huduma zao. Idadi ya “SACCOS” zilizokuwepo hadi Desemba 2007 ni 192 na kuongezeka hadi kufikia 204 kuishia Septemba, 2008.
 
5.6 Changamoto zilizojitokeza:
 
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na:-
 
•  Kutokuwepo na bajeti mahususi kwa ajili ya utekelezaji wa mpango tangu mwaka wa fedha 2006/07 na 2007/08 kaitka ngazi zote yaani Halmashauri za wilaya na ngazi ya mkoa.
 
•  Kufuatia uhamasishaji mkubwa uliofanyika mwitikio wa wananchi kujiunga katika vikundi na “SACCOS” umekuwa mkubwa kiasi ambacho kumesababisha fedha iliyotolewa na serikali kama amana kwenye mabenki husika kilikuwa ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji, hali iliyopelekea wajasiriamali wengi kukosa mikopo.
 
 
•  Ongezeko la Vyama vya Ushirika umepelekea uchache wa Maofisa Ushirika/wakauguzi kwa ajili ya usimamizi na ukaguzi wa vyama vya ushairika na hasa “SACCOS”
 
5.7 Mwelekezo/Matarajio 2008/2009 :
 
Kuwawezesha wananchi kupata mikopo ili kukuza mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi ya uzalishaji mali ili kukuza ajira na kupambana na umaskini na uwezeshaji huu ni kwa njia ya mikopo nafuu. “SACCOS” zina nafasi ya kuwafikia wananchi wengi zaidi Vijijini na Mijini.
 
Malengo:
 
Kuwawezesha wananchi kushiriki kimailifu katika shughuli za kiuchumi kuongeza fursa za ajira kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wajasiriamali hasa wale wadogo
 
5.8 Utekelezaji 2008/2009:
 
(i) Uzalishaji umeongezeka katika mazao ya nafaka; mahindi, mpunga (lower Moshi na Ndugu), zao la Tangawizi, pia katika uvuvi kwa wavuvi wa Bwawa la Nyumba ya Mungu.
 
(ii) Ongezeko la Vyama vya Ushirika limeendelea kujitokeza mpaka kuishia Septemba, 2008 kuna maombi ya vyama vinavyotarajiwa kuandikishwa 16 (kumi na sita) na kati ya idadi hiyo “SACCOS” ni 11. Katika vikundi vya kiuchumi kuna ongezeko la usindikaji na ukaushaji wa vyakula.
 
BONYEZA HAPA kuona mikopo uliokwisha kutolewa na mabenki mpaka kuishia septemba 2008
 
5.10 Changamoto:
 
(a) Ili kuepusha migogoro, wizi na ubadhirifu wa fedha kwenye “SACCOs” na vikundi vilivyokopeshwa fedha hizo, udhibiti wa ndani na ukaguzi wa mara kwa mara unahitajika.
 
(b) Uwezo wa Maofisa Ushirika/Wakaguzi kufanya kazi hiyo kwa wakati na kila wanapohitajika bado ni mdogo kwa sasa, kufuatia uchache wao kwa kila Halmashauri ikilinganishwa na idadi ya vyama vya ushirika vilivyoko.
 
(c) “SACCOs” ndiyo Asasi/Vyombo pekee vyenye uwezo wa kuwafikia na kuwahudumia wanachama na wananchi waliowengi na hivyo upo umuhimu wa kuvisaidia na kuviimarisha vyama hivi vya ushirika, ili viweze kutoa huduma inayotarajiwa.
 
6.0. Umiliki wa Mashamba:
 
6.1 Malengo 2006/2007:
 
Usimamizi na uendeshaji wa mashamba umeendelea kuwa chini ya Vyama vya Ushirika vya Msingi vilivyomilikishwa na kupata wawekezaji kwenye mashamba yote 41.
 
6.2 Mafanikio 2006/2007:
 
Mashamba 26 kati ya mashamba 41 yamekuwa yanajiendesha kwa kuridhisha kufuatia kujengeka mahusiano mazuri kati ya wamiliki na wawekezaji. Sehemu kubwa ya mashamba hayo yako wilaya Moshi.
 
6.3 Changamoto :
 
(i) Katika kipindi hiki jambo lililojitokeza ni kuwa, imebainika mikataba mingi iliyoingiwa kati ya wamiliki/wenye mashamba na wawekezaji iliandaliwa na mawakili wa wawekezaji na hivyo inawanufaisha zaidi wawekezaji kufuatia lugha na baadhi ya vipengile kuvibana vyama vya ushirika .
 
( ii) Serikali imeona upo umuhimu wa kuingilia kati migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kati ya wamiliki na wawekezaji.
 
( iii) Kumejitokeza ukiukaji mkubwa wa mikataba kati ya wamiliki na wawekezaji.
 
(iv) Sheria ya Ushirika Namba 20 ya mwaka 2003 na ile ya ardhi hazikuzingatiwa na hivyo kuwa sehemu ya migogo iliyojitokeza.
 
6.4 Malengo 2007/2008:
 
(i) Serikali ya mkoa kufanya utafiti kupitia kamati ya mashamba ya mkoa kwa kutembelea mashamba yote.
 
6.5 Mafanikio :
 
Hadi kufikia mwezi Aprili 2008 asilimia 100 sawa na mashamba 41 yalikuwa yamepata wawekezaji. Katika baadhi ya mashamba kuna maeneo ya ardhi yasiyowekezwa yenye jumla ya eka 3,275.20.
 
Hata hivyo hali ya maendeleo ya uwekezaji ni kama ifutavyo:-
Uwekezaji zaidi ya asilimia 76 -100
•  Tchibo Estate Ltd.
•  African Plantation Kilimanjaro Ltd.
•  Block and Boacha Ltd..
•  Otaru Manufacturing Trading Co. Ltd.
•  Blue Mountain Coffee Farm Ltd
•  Mufindi Tea and Coffee Co. Ltd.
 
Uwekezaji asilimia 75 – (51 – 75%);
•  N. G. Emanuel & Sons Co. Ltd
•  Ocean Link Shipping Services Ltd.
•  Tier Life (T) Ltd.
•  Shira Farming Co. Ltd.
•  Lyamungo Primary Co-operative Society Ltd.
•  Tudeley Estate Ltd
•  DekkerBruins
•  Mkomari & Godbless Farm Enterprises.
 
Uwekezaji chini ya asilimia 50 – 0 (0-50%) ;
 
•  Theo Trading Co. Ltd.
•  Africado Company Ltd
•  Bourbon Coffee Estate Ltd.
•  Sam Food Products Ltd.
•  Hai West Coffee and Fresh Farm Ltd.
•  Sheteco Ltd.
•  Fiona Ltd
•  Mufindi Tea and Coffee Co. Ltd/Dhiru Chauhan
•  Vasso Agroventure Ltd
 
Hata hivyo, azma ya Serikali ya mashamba hayo kuleta maendeleo kwa wananchi haijatimia kikamilifu kwa kuwa ni mashamba machache kati ya hayo ndiyo yanaendeshwa vizuri. Yaliyobaki yamegubikwa na migogoro mbalimbali inayotokana na:-
 
•  Kuingia mikataba mibovu na wawekezaji au kuingia mikataba na wawekezaji ambao siyo waaminifu.
•  Uongozi wa Ushirika na ubia ambao ni dhaifu.
•  Kukosa mitaji ya kutosha ya kuwekeza kwenye mashamba.
•  Kuwa na matatizo ya mgawanyo wa mapato kutokana na watendaji na viongozi dhaifu au wasio waadilifuwa baadhi ya vyama vya ushirika.
•  Baadhi ya sehemu za mashamba kuvamiwa na wananchi kwa shughuli zao za kilimo cha kawaida.
•  Baadhi kuwa kwenye matatizo ya mgawanyo wa maji ya kumwagilia kwakutozingatia taratibu za HATI miliki za maji.
 
6.6 Changamoto zinazohusiana na mashamba ni;
 
•  Kufanya rejea ya mikataba iliyopo na kuhakikisha inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.
•  Kufanya tathmini ya jumla na kuweka njia bora za undeshaji wa mashamba hayo,
•  Kuimarisha ubia na uongozi wa Vyama vya Ushirika wahusika na mashamba hayo.
•  Kuangalia uwezekano wa kuwa na chombo cha jumla cha uratibu na usimamizi wa mashamba hayo.
 
6.7 Malengo 2008/2009:
 
Kufanya utekelezaji wa maazimio ya serikao ya mkoa kupitia kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichoketi tarehe 9 Mei, 2008.
 
6.8 Mafanikio 2008/2009:
 
(i) Serikali ya Mkoa imekwisha sambaza taarifa ya mashamba kwenye wilaya zenye mashamba hayo yaani Siha, Hai, na Moshi tayari kwa utekelezaji.
 
(ii) Kamati ya Mashamba ya Mkoa imeanza kufanya ufuatiliaji kwenye Halmashauri za wilaya za Siha, Hai na Moshi kusaidia utatuzi wa baadhi ya migogoro kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
 
6.9 Changamoto:
 
•  Kufanya rejea ya mikataba iliyopo na kuhakikisha inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.
•  Kufanya tathmini ya jumla na kuweka njia bora za undeshaji wa mashamba hayo,
•  Kuimarisha ubia na uongozi wa Vyama vya Ushirika wahusika na mashamba hayo.
•  Kuangalia uwezekano wa kuwa na chombo cha jumla cha uratibu na usimamizi wa mashamba hayo.
         
Rudi juu   Rudi juu   Rudi juu
 
.........................................................................................................................................................................................................................................................................................
 
COPYRIGHT© OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, S.L.P 3070, SIMU: 027 2752184/54236-7, FAX: 027-2753248. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA.