Vijana Mkoani Kilimanjaro wamehimizwa kushiriki katika kilimo cha kahawa kwani kinamanufaa na kuacha fikra potofu kwamba zao hilo halina faida na lifaa kulimwa na wazee pekee.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Lole kata ya Mwika kaskazini Wilayani Moshi, baada ya kutembelea kiwanda cha kubangua kahawa kinachomilikiwa na kikundi cha Amkeni Coffee Group Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Amour Hamad Amour amewataka vijana kuunda vikundi vya kujihusisha na shughuli za kilimo hususan kilimo cha zao la kahawa.
Aidha Bw. Amour ameeleza kufurahishwa kwake na hatua zilichukuliwa na kikundi cha Aamkeni Cofee Group kwa kuungana wakiwa mchangnyiko wa wanawake na wanaume na kujishughulisha pamoja katika shughuli za kilimo,kununua na kubangua kahawa kwa pamoja.
Kuhusu kuunga mkono juhudi za serikali katika kuanzisha viwanda Bw. Amour amesema kikundi hicho ni mfano wa kuigwa kwani kuanzisha kiwanda kidogo cha kubangua kahawa ni mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye uwezo wa kuziongezea thamani malighafi na kuwa bidhaa kamili tayari kwa kuingizwa sokoni.
Awali akimkaribisha Kiongozi huyo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba ameleza kuwa moja kati ya malengo ya kuufikisha Mwenge wa Uhuru katika kiwanda hicho ni kumtaka aone juhudi za wananchi hao ili aweze kuwatia moyo na kutoa hamasa kwa wananchi wengine kuiga mfano mzuri wa kikundi hicho.
Mbali na hilo Mhe. Warioba alimueleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazokabili juhudi za serikali wilayani moshi katika kuimarisha kilimo cha kahawa ni vijana kukimbia zao hilo kwa mawazo kuwa kilimo cha zao hilo hakina faida.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa