• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Internal Audit
      • Kitengo cha Sheria
      • Procument and Supply
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

TPC Waanza Msimu Mpya wa Uzalishaji

Posted on: June 11th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Dkt Anna Mgwhira ameupongeza uwongozi wa kiwanda cha Sukari TPC kwa kuanza uzalishaji wa Sukari katika msimu wa 2020/2021ambapo wanatarajia kuzalisha takribani tani elfu 93 za sukari licha ya kukabiliwa na changamoto ya mafuriko ambayo imeathiri uzalishaji wa miwa katika mashamba kiwanda hicho


Akizungumza katika ghafla ya uzinduzi wa msimu huo Dkt. Mgwhira amesema hatua hiyo itasaidia kuwaondolea adha walaji kulanguliwa  kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kuagiza sukari  kutoka nje ya nchi na kuiuza kwa wananchi kwa bei ghali.


Aidha Dkt.Mgwhira amewataka wafanyabiashara kuwa waadilifu kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazotolewa na bodi ya Sukari ikiwemo ukomo wa bei elekezi ifikapo juni 30/ 2020 kwani kuanzia kipindi hizo sukari itakayozalishwa ndani ya nchi itatosha kukidhi mahitaji ya wananchi.


Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Utawala wa kiwanda cha TPC Bw. Jaffary Ally amesema uzalishaji wa sukari umeshaanza rasmi ambapo wanatarajia kuzalisha  kwa ziada ikilinganishwa na msimu uliopita kwa kuzalisha takribani tani 93,000 kutoka tani 89,000 walizozalisha msimu uliopita ili kutatua changamoto ya uhaba  wa sukari hapa nchini.



Bw. Ally amesebainisha changamoto kubwa waliyonayo kwa Sasa ni mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika ambapo maji yamefurika mashambani na kuharibu miwa iliyokuwa shamabani pamoja na miundombinu  ikiwemo na barabara na reli zinazotumika kusafirisha miwa kutoka mashambani hadi kiwandani .


Aidha Bw. Ally amewataka wasambazaji wa Sukari kufuata taratibu za usajili zinazotolewa na Serikali kupitia Bodi ya Sukari  ikiwemo kutofungasha sukari kwenye mifuko yenye ujazo wowote ambayo haina nembo ya mzalishaji kwani ni kinyume cha sheria na kunahatarisha afya za walaji.



Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • Angalia Zote

Habari

  • Waziri Aweso Avunja Mkataba na Mkandarasi wa Mradi Mkubwa wa Maji

    December 25, 2020
  • Serikali Yarudisha Mali za Ushirika

    November 12, 2020
  • Rais Magufuli: Viwanda Suluhisho la Ajira

    October 22, 2020
  • Rais Magufuli Asikitishwa Mradi wa Maji Kuchelewa

    October 20, 2020
  • Angalia Zote

Video

Tamasha la Upimaji VVU Mkoa wa Kilimanjaro
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Fomu ya Opras

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Manispaa ya Moshi
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Florida Street

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: 027 2758248/027 2751

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa