Mapambano dhidi ya rushwa katika mkoa wa Kilimanjaro yamesaidia kuokoa fedha za umma kiasi cha shilingi milioni themanini na sita laki tatu na elfu hamsini na mia tatu kumi na tatu katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017.
Akiongea wakati wa kupokea mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira amesema mafanikio hayo yametokana na kuongezeka kwa uelewa wa wananchi juu ya athari za rushwa pamoja na faida za kupambana na rushwa.
Mhe. Mghwira ameongeza kuwa hadi kufikia Mwezi Juni, 2017, taarifa za rushwa 247 zimepokewa kupitia vyanzo mbalimbali vya kiuchunguzi.
Ameongeza kuwa miongoni mwa taarifa hizo, taarifa 247 zimeonekana kuwa na uhusiano na rushwa, na taarifa hizo taarifa 21 zipo katika hatua mbalimbali kwa ajili ya kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Aidha Mhe. Mghwira ameongeza kuwa jumla ya kesi 29 zimefikishwa mahakamani na kesi 4 zimehukumiwa ambapo kesi 25 zinaendelea Mahakamani huku jumla ya taarifa 168 zikiwa katika hatua za awali za uchunguzi.
Mkoa wa Kilimanjaro umepokea mwenge wa uhuru kutoka Mkoa wa Manyara tarehe 15/09/2017 ambapo unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri zote na hatimaye kukabidhiwa mkoa wa Tanga tarehe 22/09/2017.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa