SEKTA YA KILIMO
Mazao ya kilimo yanayolimwa kwa wingi na wananchi ni pamoja na Kahawa, Ndizi, Mahindi, Mpunga, Maharage na Viazi Mviringo. Wananchi huendesha kilimo cha kutegemea mvua zaidi na pia kilimo cha umwagiliaji ambapo kuna jumla ya hekta 453,220 zinazofaa kwa kilimo na hekta 120,042 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Kati hekta 120,042 za umwagiliaji, hekta 85,252 ndizo zinazotumika sasa, ikiwa ni sawa na asilimia 71 ya eneo lote. Sehemu kubwa ya maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji yanapatikana katika Halmashauri za Wilaya za Moshi (37%), Hai (23%), na Same (23%).
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa