Malengo
Idara hii itafanya shughuli zifuatazo:-
i)Kuratibu usimamizi wa elimu ya awali, msingi, sekondari, watu wazima, elimu isiyo rasmi na mafunzo ya ufundi stadi
ii)Kutambua na kuratibu upangaji wa walimu katika shule za awali, msingi na sekondari katika Mkoa kwa kushirikiana na TAMISEMI.
iii)Kuratibu utekelezaji wa Mitaala na viwango vya elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
iv)Kusimamia mitihani ya shule za msingi, shule za sekondari na vyuo vya ualimu vilivyopo Mkoani kwa kushirikiana na NECTA.
v)Kusimamia utoaji wa mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia shuleni.
vi)Kuratibu wa upatikanaji wa mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
vii)Kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima na elimu isiyo rasmi katika Mkoa
viii)Kuratibu na kusimamia uibuaji wa vipaji na maendeleo yao.
ix)Kuanzisha na kudumisha kanzidata ya elimu na ukuzaji ujuzi wa katika Mkoa.
x)Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa ripoti za mapendekezo yanayotokana na ukaguzi wa shule.
xi)Kuratibu mipango ya maendeleo ya utamaduni na michezo shuleni; na
xii)Kuratibu shughuli za sanaa na michezo katika Mkoa.
Idara hiyo itaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia atakuwa Afisa Elimu
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa