Sunday 18th, May 2025
@kijiji cha Mkalama kata ya Rundugai wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wananchi mkoani humu kuendelea kuuenzi, kuudumisha na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kutowapa nafasi baadhi ya watu wenye chokochoko ya kutaka kutia maneno ya chuki kuhusu Muungano.
Babu alitoa kauli hiyo Aprili 26, 2025 alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Mkalama kata ya Rundugai wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo maadhimisho hayo yalifanyika kimkoa kwa kupanda miti 15000 katika eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na badae kuzungumza na wananchi.
Alisema kuwa, muungano huo umepelekea Wananchi kutoka Tanzania bara kwenda Zanzibar kifua mbele huku wengine wakitoka Zanzabar kuja Tanzania bara kifua mbele ambalo yote hayo yamechangiwa na uwepo wa muungano huo.
“Watanzania bara wengi wapo Zanzibar wanapata elimu na wapo Wazanzibar wanapata elimu kwenye vyuo vikuu na vyuo vingine kwa uhuru na upendo mkubwa kwa sababu ya tunu ya muungano wetu hivyo Wanakilimanjaro tunawajibu wa kuendelea kuulinda muungano” alisema Babu.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa, viongozi wameweza kuwaweka wananchi pamoja na kuhakikisha dosari za muungano zilizokuwa zinasemwa zimetatuliwa ambapo kwa sasa zimebaki tatu ambapo nazo zinafanyiwa kazi.
Alisena kuwa, Watanzania wanayo kazi ya kuendelea kuulinda Muungano na kutowapa nafasi baadhi ya watu wenye chokochoko za kutaka kutia maneno yao ya chuki kuhusu muungano na kuwataka kuulinda kwa nguvu zao zao.
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, katibu Tawala wa Mkoa, Yusufu Nzowa amesema tukio hili la Muungano ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar hivyo wananchi waendelee kuudumisha Kwa kulinda Amani ya nchi yetu.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa