Majukumu ya kitengo cha Fedha na Uhasibu yamegawanyika kwenye nyanja zifuatazo:
Usimamizi wa Mishahara:
Kuandaa na kuidhinisha malipo ya Mishahara
kuandaa na kutunza orodha ya watumishi wanaolipwa mishahara
Kuwezesha makato mbalimbali kutoka mishahara ya watumishi na kuyawasilishan mamlaka husika
Kuwezesha Malipo:
Kuandaa na kuingiza malipo kwenye mtandao wa malipo
Kuchukua hundi zamalipo kutoka Hazina ndogo
Kupeleka fedha tasilimu na hundi benki
Kutayarisha taarifa za mwezi za malipo
Kuwalipa watumishi fedha taslimu au hundi na kuwalipa watoa huduma kwa hundi
Kutunza daftari la hesabu
Hesabu za Mwisho wa Mwaka:
Kutayarisha Makadirio ya bajeti na kudhibiti matumizi
Kuandaa taarifa ya matumizi ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali
Kujibu hoja zote na maoni ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Kuandaa taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Ukusanyaji Mapato:
Kukusanya Mapato
Kusimamia mapato kwa mujibu wa sheria na miongozo
Ukaguzi wa Awali:
Kuhakiki nyaraka za malipo kama zimezingatia taratibu za malipo ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa
Kuhakikisha kama sheria, kanuni na miongozo na nyaraka za fedha kama zimezingatiwa
Kuhakikisha malipo yatakayofanyika hayavuki bajeti ya kasma husika
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa