SEKTA YA UVUVI
Shughuli za uvuvi zinafanyika katika vyanzo mbalimbali vya maji kama vile maziwa, mabwawa ya asili, mito na mabwawa ya kuchimbwa majumbani. Shughuli kubwa za uvuvi hufanyika katika Bwawa la Nyumba ya Mungu, Mabwawa mengine yanayotumika ni Kalemawe, Ziwa Jipe, Ziwa Karamba, Ziwa Chala pamoja na Mto Pangani. Bwawa la Nyumba ya Mungu linazungukwa na halmashauri za wilaya tatu ambazo ni Moshi na Mwanga zilizopo mkoa wa Kilimanjaro na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro iliyopo mkoa wa Manyara.
Bwawa la Nyumba ya Mungu lina ukubwa wa kilomita za mraba 140 na lina uwezo wa kuzalisha tani za samaki 5,173 kwa mwaka (iwapo uvuvi endelevu utazingatiwa) ambazo zinazokadiriwa kuwa na wastani wa shilingi 36,211,000,000.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa