Seksheni hii ina lengo la kuziwezesha Seksheni nyingine kutimiza majukumu yake, kutoa utaalamu na huduma mbalimbali zinazohusiana na usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala kwenye Sekretarieti ya Mkoa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Utawala na Rasilimali watu:
•kuratibu masuala ya Mahusiano na Ustawi wa Wafanyakazi ikiwa na pamoja na masuala ya Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni
•kuratibu maandalizi, utekelezaji, usimamizi na tathimini ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja kwenye Sekretarieti ya Mkoa
•kutoa huduma za Masijala, Ofisi na utunzaji na usimamizi wa kumbukumbu
•kutoa huduma za Kihitifaki/Itifaki katika Mkoa
•kuratibu huduma za Ulinzi, Usafi na utunzaji Ofisi, majengo na maeneo/viwanja vya ofisi na huduma za Usafiri
•Kutoa huduma za ujumla za uangalizi wa vifaa vya ofisi na majengo
•Kuratibu utekelezaji wa jukumu la kuimarisha Nidhamu ikijumuisha utoaji wa elimu ya kuzuia Rushwa.
•Kuratibu utekelezaji wa masuala mtambuka kama Jinsia, Ulemavu, HIV/AIDS kwenye Sekretarieti ya Mkoa
•Kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma – Tume/Sekretarieti ya Ajira juu ya masuala yote yanayohusiana na Ajira na Uteuzi wa watumishi.
•Kushauri juu ya ufanisi wa kitaasisi wa Sekretarieti ya Mkoa
•Kusimamia hatua/Mchakato wa kuwathibitisha na kuwapandisha vyeo/madaraja watumishi wa Mkoa
•Kuwezesha mafunzo ya rasilimaliwatu na maendeleo (taaluma, weledi, kuboresha ujuzi) kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa
•Kuwezesha programu za mafunzo elekezi kwa waajiriwa/watumishi wapya
•Kusimamia Mpango wa Rasilimaliwatu kwa ajili ya kujua upatikanaji na mahitaji ya wataalamu kwenye Sekretarieti ya Mkoa
•Kusimamia mishahara na kushauri juu ya kusimamia mfumo/orodha ya malipo ya mshahara
•Kusimamia utekelezaji wa mfumo wa wazi wa mapitio na upimaji wa utendaji wa kazi (OPRAS)
•Kushughulikia na kuhuisha taarifa za watumishi kama Likizo za mwaka, likizo za uzazi na matibab, ruhusa za mafunzo/masomo na watumishi kuondoka kazini
•Kuratibu upatikanaji wa mafao ya watumishi (malipo ya pensheni n.k) na madai mengineyo
•Kushughulikia upatikanaji wa huduma zinazohusiana na watumishi kuondoka kwenye utumishi (kustaafu, kujiuzulu n.k)
•Kuratibu kamati ndogo ya Ajira na Uteuzi ya Mkoa
•Kusimamia masuala ya kinidhamu
•Kuratibu na kushughulikia malalamiko na mashitaka
•Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya masuala yanayohusu rasilimaliwatu
•Kusimamia upatikanaji wa huduma za Habari, Elimu na Mawasiliano kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa
•kuratibu utekelezaji wa sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na sheria nyingine zinazohusiana na Utawala na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa