Majukumu ya Kitengo Cha Ukaguzi wa Ndani yamegawanyika kama ifuatavyo;-
1.Kuandaa na kutekeleza Mipango Mkakati ya Ukaguzi.
2.Kukagua na kutoa Taarifa juu ya udhibiti sahihi wa Nyaraka uhifadhi na matumizi ya Rasilimali za Sekretariet ya Mkoa.
3.Kukagua na kutoa Taarifa juu ya utekelezaji wa taratibu za Uendeshaji zilizowekwa katika Sheria mbalimbali za Nchi au Kanuni au Maagizo yoyote kwa Udhibiti wa Matumizi ya Mali, Madeni na Rasilimali zilizopo katika Usimamizi wa Sekretarieti ya Mkoa.
4.Kukagua na kutoa taarifa juu ya uainishaji na mgawanyo sahihi wa Hesabu za Mapato na Matumizi.
5.Kutengeneza taratibu za Ukaguzi Ili kuwezesha kufuata Viwango vya Kitaifa na Kimataifa vilivyoainishwa na Taasisi zinazotambulika Kisheria (NBAA, IIA,IFAC etc).
6.Kukagua na kuripoti juu ya uaminifu na uadilifu wa Kifedha, namna ya uendeshaji na kuandaa Taarifa mbalimbali.
7.Kukagua na kuripoti juu ya Mifumo inayotumika kulinda Mali na kuthibitisha uwepo wa Mali hizo.
8.Kukagua na kuripoti utendakazi au Programu ili kuhakikisha kama matokeo yanaendana na malengo yaliyokusudiwa.
9.Kukagua na kutoa Taarifa juu ya Mtizamo wa Menejimenti kwenye Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani na kusaidia Usimamizi katika utekelezaji wa Mapendekezo yaliyotolewa na Taarifa na ufuatiliaji wa utekelezaji iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
10.Kukagua na kutoa ripoti juu ya utoshelevu wa Vidhibiti vilivyoundwa kwenye mifumo ya TEHAMA iliyopo Sekretarieti ya Mkoa.
11.Kufanya Ukaguzi wa Ufanisi katika Tathmini ya Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa