• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
      • Trade and Investment
      • Administration and Human Resource Department
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ukaguzi wa Ndani
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

HALMASHAURI YA SIHA YAPONGEZWA KWA UKUSANYAJI BORA WA MAPATO

Posted on: June 17th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Kiseo Nzowa, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Siha kwa mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, hatua inayochochea kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uboreshaji wa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Nzowa alisema kuwa juhudi madhubuti zinazofanywa na viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo katika kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa ufanisi na uaminifu ni mfano bora unaopaswa kuigwa na halmashauri nyingine ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha, amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dkt. Haji Mnasi, kuendeleza juhudi hizo ili kuisaidia serikali kufanikisha ajenda ya maendeleo kwa wananchi wa Siha.

Katika hatua nyingine, Bw. Nzowa alitumia nafasi hiyo kuwasilisha taarifa rasmi ya kuhitimishwa kwa shughuli za Mabaraza ya Madiwani katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kilimanjaro, kufuatia ukomo wa muda wa uongozi wa Madiwani waliopo. Alitoa wito kwa madiwani hao kuhakikisha wanarejesha vitendea kazi walivyokabidhiwa na halmashauri katika kipindi chao cha utumishi, ili viweze kutumika kwenye awamu ijayo.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha imevuka lengo la  ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 100, ikifikia asilimia 114 katika mwaka wa fedha 2024/2025..

Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • ZOEZI LA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA MEI 16 HADI MEI 22 2025 KILIMANJARO May 15, 2025
  • MRADI WA BOOST April 01, 2023
  • Angalia Zote

Habari

  • KATIBU TAWALA MKOA WA KILIMANJARO ASISITIZA UTOAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANANCHI WILAYANI HAI

    June 18, 2025
  • HALMASHAURI YA SIHA YAPONGEZWA KWA UKUSANYAJI BORA WA MAPATO

    June 17, 2025
  • BASATA YAWANOA MAAFISA UTAMADUNI NA BIASHARA KILIMANJARO

    May 22, 2025
  • VIJANA NA WANAWAKE MSIKOPE BILA MALENGO

    May 15, 2025
  • Angalia Zote

Video

Kujisajili kwenye mfumo wa NeST - Hatua ya Awali
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Watumishi Portal

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na Kufuatilia malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    17 Barabara ya Florida

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: +255 (027) 2754236/7

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa