Wananchi wanaoishi jirani na Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) wamehakikishiwa kuwa hifadhi hiyo ni salama kwa wananchi walioruhusiwa kuingia ndani ya msitu wa kifadhi kwa aliji ya kujipatia mahitaji mbalimbali ikiwemo kuokota kuni na kukata majani kwa ajili ya malisho ya mifugo.
Akijibu hoja za baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ubetu ambacho ni moja ya vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo wilayani Rombo Kaimu Mkuu wa hifadhi hiyo Charles Ngendo (pichani) amewahakikishia wananchi hao kuwa hawatopata madhara yoyote endapo wataingia ndani ya hifadhi hiyo bila kukiuka sheria na taratibu za hifadhi.
Aidha Ngendo aliwataka viongozi wa vijiji vinavyozunguka msitu wa hifadhi watumie kamati za mazingira za vijiji husika kuratibu namna ya kusimamia wanawake wanaoingia hifadhini kutafuta mahitaji waingie kwa usalama bila ya kupata bughudha yoyote.
Kuhusu utaratibu wa kuruhusu wanawake pekee kuingia ndani ya hifadhi Ngendo alisema huo ni utaratibu uliowekwa baada ya kufikiwa maamuzi ya kulinda hifadhi yalifanywa na Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa (RCC) hivyo hauwezi kukiukwa.
Awali mwananchi wa kijiji cha Ubetu aliyejitambulisha kwa jina la Mama Silayo amedai kuwa baadhi ya wanawake wamekuwa wakichapwa kwa fimbo na baadhi askari wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro wanapokutwa ndani ya hifadhi wakiokota kuni.
Ngendo alimtaka Mama silayo awasilishe malalamiko pamoja na ushahidi katika utaratibu rasmi ikiwa ni pamoja na kuonana na uongozi wa hifadhi mapema iwezekanavyo ili uongozi huo uweze kuchukua hatua kwa mtumishi aliyetenda kitendo hicho.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amewataka wanawake wanaongia ndani ya hifadhi kuwa waaminifu na waadilifu wapoingia ndani hifadhi kwa kuhakikisha kuwa hawavunji sheria na kanuni za hifadhi.
Kuhusu utoaji wa taarifa amewataka watoe taarifa sahihi na si za kudanganya ili kuisaidia serikali kutenda haki.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa