Halmashauri ya wilaya Same mkoani Kilimanjaro imetakiwa kukamilisha ujenzi wa soko la kazndo ya barabara ili kuwaewzesha wananchi hususan wakulima na wafanyabiashara ndogondogo kunufaika na mradi huo.
Akiongea na wananchi baada ya kukagua mradi huo wa ujenzi wa soko kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi amesema wameridhishwa na taarifa zilizowasilishwa kuhusu gharama za mradi huo kwani zinaendana na thamani ya fedha.
Awali akiwasilisha taarifa ya mdari huo kwa kiongozi wa mbio za mwenge, fundi sanifu wa mradi huo Bi. Magreth Mkenda amesema mradi huo unaotekelezwa kwa kugharamiwa na wananchi, halmashauri na shirika la UNDC utagharamu kiasi cha Tsh.2,737,239,321 hadi kukamilika.
Mradi huo unatajiwa kutoa fursa za kibiashara kwa wajasiliamali wasiopungua 250 na ajira za kudumu kwa watumishi 10.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa