Tume ya taifa ya uchaguzi imejiandaa vizuri kuhakikisha kuwa kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura anapata fursa hiyo ili kutekeleza haki yake ya msingi.
Akizungumza mjini Moshi kwenye kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa uchaguzi wakimemo viongozi wa dini, asasi za kiaraia, viongozi wa vituo vya redio na waandishi wa habari katika mkoa wa Kilimanjaro, Mkurugenzi wa kitengo cha ukaguzi wa ndani wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Amos Ackim amesema kila mtu mwenye sifa ya kupiga kura atapata fursa ya kupiga kura bila kujali hali yake.
Bw.Ackim amefafanua kuwa tume imeandaa vifaa maalum vitakavyowezesha watu wenye mahitaji maalum hususan walemavu ili waweze kupiga kura ili wachague viongozi wanaowataka.
Mbali na hilo Bw. Ackim amewataka waandishi wa habari, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa makundi mbalimbali katika jamii watoe elimu kwa jamii ili wazingitie hali za watu wenye ulemavu siku ya kupiga kura.
Amefafanua kuwa ni wajibu wa kila mtu atakayekuwepo katika kituo cha kupigia kura kuhakikisha anatoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu wanapokuwa kwenye foleni za kupiga kura.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa