Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kwenye Mkoa wa Kilimanjaro
Kujenga mazingira rafiki ya kiutendaji kwa Walimu ili kuakikisha haki za walimu hao zinatekelezwa.
Akitoa kauli hiyo wakati akizindua kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za kiutumishi kwa Walimu iliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari WeruWeru leo Machi 11, 2025 Mhe.Babu amesisitiza umuhimu wa Walimu katika Jamii na Taifa kwa ujumla katika kuhakikisha ukuaji wa sekta ya Elimu Nchini na hivyo wanapaswa kuheshimiwa na kupatiwa Haki zao za Msingi.
"Asitokee Kiongozi yeyote ndani ya Mkoa,kuwafokea Walimu,kuwazalilisha kuwakakalipia mbele za watu au kuwabeza kwa namna yeyote ile kwani mwalimu ni mtu Mhimu sana katika Jamii"alisema Rc.Babu
Aidha, amewasihi Walimu kupitia umoja wao kuendelea kutekeleza wajibu huku akisema serikali itaendelea kutatua changamoto za kiutumishi kwani inatambua mchango mkubwa wa Walimu katika jamii na Taifa kwa Ujumla.
Awali akizungumza Makamu Rais wa Chama cha Walimu Nchini Suleiman Ikomba ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia kuwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa walimu katika kuwapatia mafunzo mbalimbali ya kiutumishi uku akieleza kuwa kuwepo kwa kliniki hii itasaidia kutatua changamoto za Kiutumishi kwa Walimu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Uzinduzi wa kliniki hiyo ulienda samabamba na ugawaji wa vifaa mbalimbali kwa Waalimu walemavu,pamoja na Uzinduzi wa Gari la Chama Cha Waalimu Wilaya ya Moshi CWT hafla iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa Nurdin Babu.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa