Serikali na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wamepiga hatua nzuri katika kupambana na ugonjwa wa UKIMWI . Akizungumza baada ya kupokea mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira amesema kiwango cha maambukizi kimeshuka kutoka 3.8 kwa mujibu wa utafiti wa viashiria vya UKIMWI wa 2011/12 na kufikia asimilimia 2.6 kwa mujibu wa utafiti wa viashiria hivyo wa 2017.
Takwimu hizo ziufanya mkoa wa kilimanjo kuwa na miongon mwa mikoa yenye kiwango cha chini cha maabukizi ikilinganishwa na takwimu za kitaifa ambazo ni asilimia 5.
Aidha Mhe. Mghwira meongeza kuwa mkoa umeweka mkakati wa kuhakikisha kiwango cha maambukizi kinaendelea kupungua kwa kuendelea kutoa elimu ya afya kwa wananchi hususani kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Ameongeza kuwa mkoa umejipanga kuendela kuwahamasisha wananchi kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa hiyari,kuacha tabia hatarishi na kuhakikisha watu wote waliogundulika kuaathirika na virusi vya UKIMWI wanaanza matumizi ya dawa za kufubaza virusi hivyo mapema iwezekanavyo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa