• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
      • Trade and Investment
      • Administration and Human Resource Department
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ukaguzi wa Ndani
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

MAJALIWA ATAKA MIKAKATI ZAIDI MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWENYE MAGEREZA.

Posted on: August 30th, 2025

MAJALIWA ATAKA MIKAKATI ZAIDI MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWENYE MAGEREZA, Asema Rais Dkt. Samia ameonesha njia kwenye matumizi ya nishati safi.

Alipongeza Jeshi la Magereza kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo matumizi ya nishati safi.


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati zihakikishe kuwa magereza yote nchini yanaunganishwa na mifumo ya nishati safi ifikapo mwaka 2027.

Amesema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itasaidia kuboresha huduma kwa wafungwa, kulinda afya za watumishi na wakazi wa magereza pamoja na kuhifadhi mazingira.


ametoa wito huo leo Jumamosi (Agosti 30, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Magereza nchini. Uzinduzi huo umefanyika kwa niaba ya magereza yote nchini.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa uzinduzi huo ni utekelezaji wa mkakati wa kuhama kutoka nishati zisizosafi na kuhamia katika matumizi ya Nishati Safi ya kupikia. “Rais wetu Dkt. Samia anatambulika Afrika na duniani kwa ujumla kwa hamasa yake ya matumizi ya nishati safi, hatua hii mmeonesha kwa vitendo kwamba mnamuunga mkono”


“Takwimu zinaonyesha kuwa gereza moja linaweza kutumia zaidi ya tani 100 za mkaa kwa mwaka, zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60. Kupitia nishati safi, gharama hizi zitapungua kwa zaidi ya asilimia 50.”


Amesisitiza kuwa hatua hiyo ni ya kupongeza kwa kuwa inaunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha jamii yote inatumia nishati hiyo na hivyo kwa kiasi kikubwa kuondoa madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyo safi.


Ameongeza kuwa tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa moshi wa kuni na mkaa una kemikali hatarishi zinazoweza kusababisha magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama vile nimonia, kikohozi sugu na pumu. “Kwa kupunguza matumizi ya nishati hizo, Jeshi la Magereza linachangia moja kwa moja katika kuboresha hali ya hewa ndani ya magereza, kuongeza tija ya kazi kwa watumishi na kuhakikisha ustawi wa wafungwa.”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Sekta binafsi kuongeza ubunifu na uwekezaji katika teknolojia nafuu na salama za kupikia, ili kuharakisha upatikanaji wa suluhisho bora kwa wananchi wengi zaidi.


“Pia Wizara ya Fedha na Viwanda na Biashara hakikisheni mnaweka mizania rafiki ya kisera, kodi na mifumo kwenye uwekezaji wa Nishati Safi ya kupikia. Kadhalika Kila Taasisi, Kila Jamii, na Kila Mwananchi ana jukumu katika matumizi ya nishati safi. Tuchukue hatua leo, kwa manufaa ya kesho ya watoto wetu na vizazi vijavyo”.


Naye, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo amesema kuwa mradi huo uliozinduliwa utasaidia sana katika utunzaji wa mazingira na wapishi katika magereza nchini. “Jeshi letu la magereza limefanikiwa kutekeleza kwa asilimia 100 matumizi ya nishati safi kwenye magereza”.


Naye, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Jeremiah Katungu amesema kuwa kwa miongo mingi Jeshi la Magereza limekuwa likitumia kuni kama nishati ya kupikia na mahitaji ya kuni yalikuwa ni wastani wa mita za ujazo 91,391.25 kwa mwaka.


Amesema kuwa hadi kufikia Desemba 2024 Magereza yote nchini yalikuwa yameshaanza kutumia nishati safi ya kupikia kwa ajili ya chakula cha wafungwa na mahabusu. “Mpaka sasa vyanzo vya nishati mbadala vinayotumika katika magereza ni Gesi Vunde (BIOGAS), Mkaa Mbadala (Briquettes), Kuni Poa na Gesi Asilia (NATURAL GAS).”


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amesema kuwa Wakala wa Nishati vijijini walisaini mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 35.2 kwa ajili ya utoaji ruzuku ya kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa magereza yote Tanzania.


“Sisi REA tunatoa shilingi bilioni 26.5 sawa na asilimia 75.4 na Jeshi la Magereza linachangia shilingi bilioni 8.6  sawa na asilimia 24.6”


Amesema fedha hizo zitatumika kujenga miundombinu 126 ya biogas na majiko banifi 377, ujenzi wa miundombinu 64 ya LPG na majiko banifu 256, usambazaji wa mitungi ya gesi 15, 126 ya kilo 15, ununuzi wa mashine 61 za kutengenezea mkaa mbadala kwa kambi 22 za Jeshi la Magereza pamoja na kusambaza makaa ya mawe tani 865 na majiko banifu 344.


Akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Msimamizi wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Utunzaji wa Mazingira kutoka Jeshi la Magereza SACP Daimu Mmolosha amesema lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha kunakuwa na chanzo zaidi ya  kimoja cha nishati ili kuepukana na matumizi ya kuni ma mkaa.

Mwisho

Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • ZOEZI LA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA MEI 16 HADI MEI 22 2025 KILIMANJARO May 15, 2025
  • MRADI WA BOOST April 01, 2023
  • Angalia Zote

Habari

  • MAJALIWA ATAKA MIKAKATI ZAIDI MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWENYE MAGEREZA.

    August 30, 2025
  • STENDI YA NGANGAMFUMUNI KUANZA KAZI APRILI, 2026

    August 28, 2025
  • KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO KILIMANJARO

    August 26, 2025
  • RC ATOA SIKU 14 MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KIJIJI CHA RUVU MARWA SAME

    August 21, 2025
  • Angalia Zote

Video

Kujisajili kwenye mfumo wa NeST - Hatua ya Awali
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Watumishi Portal

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na Kufuatilia malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    17 Barabara ya Florida

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: +255 (027) 2754236/7

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa