Serikali hapa nchini imepiga marufuku uuzaji na usafirishaji wa mazao ya nafaka katika nje ya nchi bila kuwa na kibali cha serikali na kuagiza kamati za mikoa kusimamia kikamilifu agizo hilo .
Marufuku hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muuungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kasim majaliwa alipokuwa akiwahutubia waumini wa dini ya kiislam na wananchi kwa ujumlakwenye baraza la Iidd lilifanyika kitaifa mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo alilakwa kama mgeni rasmi katika ibada hiyo.
Waziri Mkuu majaliwa amesema serikali imechukua hatua hiyo ili kuliepusha taifa na upungufu wa chakula kutokana na mahitaji makubwa ya chakula waliyonayo wananchi kabla ya chakula kusafirishwa kwenda nchi jirani.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya nafaka kuomba vibali vya kusafirisha nje ya nchi bidhaa ambazo zimeshaongezwa thamani ili waweze kupata faida zaidi.
Akitoa mfano wa zao la mahindi Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa nivema wafanyabiashara wakasafirisha unga wa mahindi baadala ya kusafirisha mahindi ghafi kwani kwa kufanya hivyo wanapoteza faida katika biashara hiyo na kuhamishia nje ya nchi fursa za ajira kwa watanzani.
Mhe majaliwa alitoa mfano wa maroli kumi na moja yanayoshikiliwa na jeshi lapolisi Mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kujaribu kusafirisha mahindi nje ya nchi amesema iwe mwisho kwani mtu au kikundi chochote kitakachojihusishs na usafirishaji wa mazo ya nafaka nje ya nchi kinyume na sheria mazao hayo pamoja na vyombo vya usafiri vitakavyotumika vitaaifishwa.
Kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya Mhe. Waziri Mkuu amesema serikali inatambua na kuthamini ushirikiano unaotolewa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) pamoja na madhehebu ya mengine ya dini katika kuunga mkono juhudi za seriali kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya.
Kuhusu viashiria vya uvunjifu amani katika baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo wilaya za Kibiti na Rufiji mkoani Pwani, Mhe. Majaliwa amesema serikali inaendelea kuwasaka, kuwakamata na kuwapeleleza wahusika wote wa vitendo hivyo na watakapoabainika kuhusika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Awali akiwasilisha taarifa ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikh Salum Abeid amesema waislamu nchini wanaunga mkoano juhudi za serikali ya wamu ya tano katika vita dhidi ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
Sheikh Salum Abeid amesema waislamu wanatambua na kuthamini nia njema ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kuzirejesha mali zote za baraza hilo zilizoporwa kinyemela na watu wachache kwa njia za kuwarubuni baadhi ya viongozi wa baraza hilo.
Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania amewataka waislamu nchini na wananchi wote kuwa na mienendo mema ili amani iliyopo nchini iendelee kudumu.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa