Sekta binafsi Mkoani Kilimanjaro zimeelekezwa kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi pamoja na kuweka mikakati bora ya namna ya kutatua changamoto za waajiriwa wao kwa wakati ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima ambayo hupunguza ufanisi wa kazi na kurudisha nyuma maendeleo.
Hayo yamesemwa leo Mei 1, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu katika siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo Kimkoa yameadhimishwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.
Mhe. Babu amewaelekeza Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi kuendelea kuwatembelea na kufanya vikao kazi na wanachama wao katika maeneo yao ya kazi ili kujua changamoto wanazokabiliwa nazo na kuzitatua kwa wakati.
Aidha, uongozi wa Serikali ya Mkoa inaenda kushughulikia changamoto wanayokutana nayo wafanyakazi ya kutokupewa ushirikiano mzuri katika ofisi ya kazi mkoa pindi wanapopeleka malalamiko yao ya mfanyakazi mmoja mmoja au kupitia chama cha wafanyakazi.
Hata hivyo Mhe. Babu ameendelea kukemea suala la mmomonyoko wa maadili unaoendelea kwa sasa katika jamii zetu kwa ukatili na ulawiti unaofanywa kwa watoto na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kusema kila mmoja anajukumu la kukemea na kuchukua hatua katika kutoa elimu.
Mratibu wa TUKTA Bw. Kanuti Magashi akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema kuna baadhi ya taasisi binafsi wamekua wakitoa mikataba yamuda mfupi katika kazi ambazo ni endelevu jambo ambalo limefanya wafanyakazi kutochangai katika mifuko ya hifadhi ya jamii hii inapelekea maumivu kwa watumishi hao mara wanapofika ukomo wakazi au kupatwa na majanga kazini na kutokwenda kazini.
Aidha, Bw. Kanuti ameomba kama itawezekana suala la kikokotoo liangaliwe tena kwa mtumishi kwani bado linawaumiza ikiwezekana mara baada ya kustaafu mtumishi apewe mafao yake yote.
Hata hivyo ametoa shukrani kwa taasisi mbalimbali ambazo zimekua mstari wa mbele katika kushughulikia changamoto za wafanyakazi ndani ya mkoa.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa