Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema mwenge wa uhuru umekimbizwa kilomita 895, umekagua miradi 52 yenye thamani ya Bilion 84. Ameyasema hayo Julai 5,2025 wakati akiukabidhi Mwenge wa Uhuru 2025 katika kijiji cha Kingori kata Malula wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Amesema katika mkoa huu, miradi 22 ilizinduliwa, 20 iliwekwa mawe ya msingi na miradi 10 ilitembelewa na Mwenge wa Uhuru na yote imeridhiwa.
Amesema Mwenge huo, ulipita kwenye miradi ya kijamii 9 ikiwa ni hatua ya kuonyesha ushirikiano wa wawekezaji binafsi na serikali ya mkoa. Aidha amesema katika kubiliana na mabadiliko ya tabia nchi, mkoa wa Kilimanjaro umetoa mitungi 370 yenye thamani milioni zaidi 18.4 kwa wananchi wa maeneo mbalimbali.
Amesema katika kipindi cha siku saba watu waliopima VVU ni 1,801 walikutwa 12 sawa na asilimia 0.67, Damu salama ilipatikana unit 177, waliopima malaria 812 na hakuna aliyepatikana na ugonjwa huo.
Amesema mkoa umekuwa ukitoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya rushwa, na kesi zilizoripotiwa 401, zilizokutwa na viashiria vya rushwa ni 201, zilizotolewa hukumu 20.
Amesema mkoa huo haukubaki nyuma kwenye suala la madawa ya kulevya na jeshi la polisi liliwakamata watuhumiwa 555 waliokamatwa 232 kesi zinazoendelea mahakamani 126 na kesi zilizohukumu ni 106.
Akiaga mkoa wa Kilimanjaro, Ismail Ally Ussi amesema miradi yote imetekelezwa kwa ubunifu ufanisi mkubwa na imeakisi thamani ya miradi.
Aidha amewapongeza wakuu wa wilaya wote waliopo mkoani humo kwa jitihada wanazofanya katika kusaidia miradi ya maendeleo.
"Mimi ningeambiwa nishauri, ningeshauri wakuu wa wilaya hawa wasiondoke hapa wamsaidie Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kusimamia maendeleo ya wananchi,nimeridhishwa na utendaji kazi wao kila mahali nilipofika tulikuta mambo yameeleweka hakika hawa ni viongozi,"amesema.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa