Watumishi wa serikali katika mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutumia vizuri simu za mkononi na mitandao ya kijamii ili isiwe chanzo cha kupoteza muda wa kuwatumikia wananchi.
Akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Siha, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira amewataka watumishi kutopoteza muda kwa kutumia simu za mkononi kufanya shughuli na mawasiliano binafsi ambazo hazina uhusianona kazi.
Aidha Mhe. Mghwira amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia utu na maslahi ya umma huku kila mtumishi mmoja akitakiwa kutambua na kuzingatia umuhimu wa mtumishi mwinginie.
Kuhusu matumizi sahihi ya mali za umma Mhe. Mghwira mewataka watumishi hao kufanyakazi kwa uaminifu na uadilifu.
Mhe. Mghwira amewakumbusha watumishi kufanya kazi kwa kujali afya zao ikiwa ni pamoja na kupanga vizuri ratiba zao za kazi ili kuwa na muda wa kupumzika baada ya saa za kazi.
Kuhusu huduma za afya Mhe. Mghwira amewataka watumishi wa umma na viongozi kuwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF).
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Siha Mhe.Frank Tarimo amemuhakikishia Mhe. Mkuu wa Mkoa kuwa wataendelea kuweka mikakati endelevu ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi katika wilaya hiyo wanakuwa na kadi za Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa