Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi nchini, ambapo shule ya msingi Kwaktau iliyopo katika Wilaya ya Rombo imepata neema ya ujenzi na ukarabati mkubwa wa miundombinu ya elimu.
Akisoma taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa Mbio wa Mwenge Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwaktau Filemoni Nyaki amesema kukamilika kwa mradi huu kutaleta manufaa makubwa kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji na kuimarisha mahudhurio ya wanafunzi kwa kupunguza changamoto za utoro.
Ameendelea kusema kuwa Mradi huo umehusisha ujenzi wa vyumba saba vya madarasa ya elimu Msingi, mawili ya awali ya Elimu na matundu 16 ya vyoo pamoja na kichomea taka vyanye gharama ya Milioni 315.5 hatua inayolenga kuongeza mazingira bora na salama kwa wanafunzi kujifunza. Hali hiyo ni baada ya shule hiyo kukumbwa na changamoto ya miundombinu chakavu kwa muda mrefu, hali iliyokuwa ikikwamisha maendeleo ya elimu kwa watoto wa eneo hilo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndg. Ismail Ussi, ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo, aliipongeza serikali kwa juhudi za dhati za kuinua elimu, huku akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Mhe. Raymond Mangwala, kwa kusimamia kwa karibu ujenzi huo na kuhakikisha ubora unazingatiwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Mhe. Raymond Mangwala, alisema kuwa shule hiyo ilikuwa katika hali ya uchakavu mkubwa wa madarasa, vyoo na miundombinu mingine muhimu, hali iliyosababisha usumbufu kwa walimu na wanafunzi. Alieleza kuwa kukamilika kwa mradi huu kutabadilisha kabisa taswira ya shule hiyo na kuinua kiwango cha ufauliu.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa