Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Ekiakim Mnzava ameonyesha kuridhishwa na upandwaji wa miti pamoja na Utunzaji katika shamba la Miti la Rongai lilipo Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambalo linasimamiwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS)
Kiongozi huyo amesema Mwenge umekuta kitu cha tofauti miti imepandwa , imetunzwa na inakuwa na hilo ndio jambo ambalo wanalifanya Nchi nzima kuhakikisha miti inayo pandwa inatunzwa vizuri na sio kupanda miti na kuitelekeza na kama wapo watu wanataka kujifunza upandaji wa Miti wafike Rombo ili kuweza kuona jinsi gani wanavyo tunza miti waliyoiotesha.
Mnzava ameayasema hayo April 05,2024 wakati Mwenge wa Uhuru ulipo tembelea, kukagua , kupanda miti Shamba la miti pamoja na Uzinduzi wa Kitalu cha miti.
Akitoa taarifa ya Shamba la Miti Rongai kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge ,Mhifadhi wa Shamba la miti Rongai Joel Naasi amesema Shamba hilo lina Bustani ya miche yenye uwezo wa kukuza miche laki sita ambapo Bustani hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha miche inayo pandwa kwenye shamba lao ,kugawa kwa jamii na Taasisi za Umma na Binafsi.
Naasi amesema kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 Miche 26,900 imegawanywa kwa ajili ya utunzaji wa Mazingira , pamoja na kuoakoa vyanzo vya Maji.
Naasi amesema mafanikio yaliyopatikana hadi sasa ni Wananchi, Taasisi za Serikali na Binafsi kushiriki katika Kampeni za Utunzaji wa Mazingira na Vyanzo vya Maji ambapo Miti zaidi ya 4,000 imepandwa katika vyanyo vya Maji kwa Mwaka wa Fedha 20223/2024 katika kipindi cha Mvua za Vuli.
Kauli Mbiu Mwaka huu inasema “Tunza Mazingira,na shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa endelevu”.
Mwisho.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa