Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amesema sera ya uwekezaji kwenye viwanda ni moja kati ya suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana hapa nchini.
Akiongea na wananchi wa mji wa Moshi katika uzinduzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika eneo la gereza la Karanga Rais Magufuli amesema kiwanda hicho ni miongoni mwa mifano ya viwanda vinavyowanufaisha vijana katika kupata ajira.
Aidha Rais Magufuli amesema kiwanda hicho kitatoa ajira za moja kwa moja kwa vijana wapatao elfu tatau ambao kiwanda kitawaajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali katika uzalishaji wa bidhaa hizo zitikanazo na ngozi za mifugo.
Rais Magufuli ameongeza kuwa mnyororo wa fursa za ajira kutokana na kiwanda hicho utaenda mbali kwani wafanyabiashara za vyakula yaani mama lishe na baba lishe watapa soko la biashara kwa kuwauzia vyakula wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Ameongeza kuwa wafugaji wa mifugo wataongeza thamani ya mifugo yao kwani wataweza kuuza nyama na ngozi za mifugo na hatimaye kuongeza vipata vyao.
Mbali na makundi hayo, Rais Magufuli amesema uzalishaji wa bidhaa katika kiwanda hicho ambacho kina uwezo wa kuzalisha jozi za viatu milioni mbili kwa mwaka utachochea ajira kwa watu watakaofanya kazi za usambazaji na uuzaji wa bidhaa za zitakazolalishwa kiwandani hapo.
Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga kinazalisha viatu, mikanda, mikoba, majaketi na pochi mbalimbali kwa kutumia malighafi za ngozi za mifugo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa