Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri zilizopatwa na athari za mafuriko mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwafikishia misaada ya kibinadamu wananchi wote waliokumbwa na athari za mafuriko kwa haaraka na uadilifu.
Akiongea kwa nyakati tofauti akiwa kwenye vijiji vilivyoathirika na mafuriko katika wilaya za Moshi, Siha, Hai na Mwanga, Katibu Tawala wa Mkoa wa kilimanjaro Dkt. Khatibu Kazungu amewaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha wanaifikisha misaada hiyo kwa walengwa na kwa wakati bila kuchelewa .
Aidha Dkt. Kazungu amezitaka halmashauri hizo kuendelea kukusanya taarifa zikiwemo takwimu sahihi za uharibifu wa mali za wananchi zikiwemo nyumba, akiba za vya kula pamoja na idadi ya heka za mashamba zilizoharibiwa na mafuriko zikiwa na mazao.
Dkt. Kazungu alifanya ziara katika vijiji vyote vilivyoathirika na mafuriko katika wilaya za Mwanga,Moshi,Hai na Siha ili kuwapa pole wananchi waliopatwa na maafa hayo pamoja na kujionea madhara yaliyosababishwa na mafuriko kwa wananchi.
Dkt. Kazungu amewahakikishia wananchi wote waliopatwa na athari za mafuriko kuwa watulivu kwani serikali yao ipo pamoja nao na kuwathibitishia kuwa itahakikisha kila kaya iliyokumbwa na athari za mafuriko itapatiwa misaada ya kibinadamu itakayokidhi mahitaji muhimu ya kiutu.
Mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Kilimanjaro zimeleta madhara katika ambapo kaya zaidi ya elfu moja zimekosa makazi huku zaidi ya ekari elfu moja zilizokuwa na mazao zikiharibiwa kabisa.
Wadau kadhaa wa maendeleo wameshatoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa waathirika na kumkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira.Misaada iliyotolewa ni pamoja na vyakula, magodoro na vyandarua.
Katibu Tawala wa Mkoa ameshaikabidhi misaada hiyo kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri zilizokumbwa na mafuriko na kuwaagiza waifikishe kwa waathirika wa mafuriko mapema iwezekanavyo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa