Watumishi wa umma katika mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kutotomia tatizo la ugonjwa korona kama njia ya kukiuka sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Hayo yamesmwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Renatus Msangira alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wakati alipoahirisha kikao kilichoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa sekretatieti ya mkoa kupata elimu muhimu ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa korona.
Msangira ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro amesisistiza kuwa ni kosa kwa mtumishi wa umma kutofika kazini au kutotimiza majukumu yake kama mtumishi wa umma kwa kubaki nyumbani au kuendelea na shughuli zake binafsi kwa kusingizia ugonjwa au kujifanya anajikinga na korona.
Kwa upande wake Afisa Afya wa mkoa wa kilimanjaro Bw. Jonas Mcharo amewaelimisha watumishi wa umma juu ya namna bora ya kutoa huduma kwa wananchi huku wakichukua tahadhari ili waepuke maambukizi ya ugonjwa wa korona.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Credianus Mgimba amewataka watumishi wa umma kutopata taharuki wala kuwa waoga badala yake waendelee kutoa huduma kwa wananchi huku wakichukua tahadhari dhidi ya ugojnjwa wa korona na wanapoona mmoja wao ana dalili za ugonjwa huo basi watoe taarifa mapema ili aweze kupatiwa huduma na hatua zichukuliwe asiambukize wengine
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa