Halmashauri yaWilaya ya Mwanga imeagizwa kutenga siku maalumu kujadili hoja 47 za Mkaguzi wa Mkuu wa Hesabu wa Nje za Mwaka 2013 hadi 2019.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Stephen Kagaigai alipohudhuria kikako cha Baraza Maalumu la Madiwani lililoketi kwa ajili ya kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Mhe.Kagaigai alitoa maelekezo hayo baada ya taarifa iliyo kwenye makabrasha kuwa na idadi kubwa ya hoja za miaka iliyopita ambazo hazijajibiwa.
Aidha, Katibu Tawala Mkoawa Kilimanjaro Dr. Seif Shekalaghe ambaye naye alialikwa kwenye kikao hicho amepongeza michango na hojazilizokuwa zikitolewa na Madiwani wa Halmashauri hiyo na aliwashauri kutoa maazimio katika kila hoja watakayojadili.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bw. Zephrin Lubuva amemshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa kuhudhuria na kumuahidi kufanyia kazi kwa wakati maelekezo na maagizo aliyoyatoa kwenye kikao hicho.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa