Halmashauri mkoani Kilimanjaro zimehimizwa kusimamia kwa weledi zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza na mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa shule za sekondari.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha tarehe 13.01.2022 kilichojumuisha viongozi wa Chama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Makatibu Tawala Wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai ameyasema zoezi hili ni muhimu kwa ustawi wa taifa hivyo lisimamawe kwa umakini.
Aidha, Mhe. Kagaigai amesema kwa mwaka 2022 wanafunzi wapya wa awali walioandikishwa hadi sasa kufikia 15,135 ambapo jumla ya wavulana ni 7,559 na wasichana 7,576 sawa na silimia 50 ya maoteo ya kuandikisha Watoto 30,47. Kwa upande wa elimu ya msingi darasa la kwanza jumla ya wanafunzi walioandikishwa hadi sasa ni 17,525 ambapo wavulana 8,747 na wasichana 8,778 sawa na asilimia 58 ya lengo la uandikishaji ambapo maoteo ni kuandikishwa wanafunzi 30,039.
Kwa upande wa elimu ya sekondari jumla ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni 30,710 ambapo wavulana 15,011 na wasichana 15,699. Amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanaripoti shuleni mapema ili kuendelea na masomo yao kwa wakati. Hata hivyo ameendelea kuweka msisitizo kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wote waliotimizia umri wa kuanza shule za awali na darasa la kwanza kwa muhula wa masomo 2022 kuhakikisha waandikishwa bila kisingizio chochote maana elimu hii haina malipo ya ada.
‘‘ ni jukumu letu sote kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanaripoti shuleni mapema kwa kuzingatia muda ili waweze kuendelea na masomo yao pamoja na kuhakikisha tunaweka msisitizo kwa wazazi na walezi kuandikisha wanafunzi wote waliotimiza umri wa kuanza shule za awali na darasa la kwanza kwa muhula wa masomo mwaka 2022’’.
Mbali na maelekezo hayo Mhe. Kagaigai ametoa shukrani zake za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuboresha miundombinu ya Elimu kupitia fedha za UVIKO-19. Ambapo kwa sekta ya elimu pekee mkoani Kilimanjaro ilifanikiwa kupata jumla ya shilingi Bilioni sita na milioni arobaini (6,040,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 276, vituo shikizi 18 na mabweni 2.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa