Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu ametoa wito kwa Viongozi wa Kimila Mkoani hapa kushirikiana na Serikali kupinga mmomonyoko wa maadili na kudumisha mila na desturi nzuri katika Jamii.
Amesema hayo Desemba 14, 2024 wakati akihutubia Mamia ya Wananchi kwenye Hafla ya Kusimikwa kwa Mangi wa Machame ambaye ni Kiongozi wa Mila Jamii ya Wachaga katika kijiji cha Wari Kata ya Machame ambapo amebainisha kuwepo kwa mmomonyoko wa Maadili kwa baadhi ya jamii zilizopo Mkoani hapa na hivyo kuwaasa viongozi hao kushirikiana na Serikali kukomesha wimbi la uhalifu na tabia zingine zinazopelekea mmomonyoko wa Maadili katika jamii ikiwemo suala la na Ulawiti,ubakaji na mimba kwa wanafunzi.
" Katika miezi miwili iliyopita Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro amefanya kazi kubwa sana, tumewafunga watu 30,wengine tumewafunga Maisha na wengine Miaka 30 kwa tabia Mbaya wanazozifanya kwa Watoto wetu" alisema Rc. Babu.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Kiseo Nzowa amesema kuwa serikali ya Mkoa na Watumishi wake itashirikiana vyema na Kiongozi Mpya wa Jamii hiyo kutatua kero za Wananchi ili kuleta Maendeleo na ustawi katika jamii.
Kwa upande wake Ndg.Gilbet Shangana Mangi mpya aliyesimikwa kuongoza jamii hiyo amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuthamini maendeleo ya Mila na desturi za jamii katika kuendeleza na kulinda amani ya Nchi.
Aidha amekiri kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kulinda maadili katika Jamii hiyo, kutunza Mazingira pamoja na Mila na desturi za Taifa letu.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa