• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
      • Trade and Investment
      • Administration and Human Resource Department
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ukaguzi wa Ndani
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

RC-BABU ATOA AGIZO IFIKAPO JANUARI 11,2025 SHULE ZOTE ZIWE ZIMEKAMILIKA

Posted on: January 20th, 2025

RC-BABU ATOA AGIZO IFIKAPO JANUARI 11,2025 SHULE ZOTE  ZIWE  ZIMEKAMILIKA

Baadhi ya wakazi katika wilaya ya Hai na Siha Mkoani Kilimanjaro wameishukuru serikali ya awamu ya Sita kwa kusikia kilio chao cha ubovu  wa miundombinu ya Elimu katika maeneo Yao na kuwarahisishia watoto wao kupunguza mwendo mrefu wa kufuata elimu

Wakitoa kauli zao kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema hakika kwa sasa ni faraja kwani ujenzi wa miundombinu hiyo unaendelea na hivyo watoto wao wataondokana na changamoto walizokuwa wanakumbana nazo

Aidha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu ametoa agizo na kuwasisitiza wakuu wa wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kuwa ifikapo 13 Januari 2025 ,Shule hizo zianze kupokea wanafunzi na watoto wote walio chaguliwa kuendelea na masomo waripoti shuleni

"Wanafunzi wote walio chaguliwa kuendelea na masomo natoa agizo wanatakiwa waripoti katika maeneo Yao waliyopangiwa sitaki kusikia sababu yoyote ya mtoto kutoendelea na masomo labda kama ametangulia mbele za haki 

Sasa Wakurugenzi natoa maelekezo ikifika tarehe 11 mwezi januari  ujenzi madarasa uwe umekamilika ntatuma watu wangu kimyakimya  wanipigie picha na kama hamjamaliza tutaelewana vibaya" Amesema Babu

Hata hivyo amewapongeza wananchi  katika kuunga mkono ujenzı wa shule hizo ikiwemo uchimbaji msingi

Sambamba na hayo Mkuu wa Shule ya Msingi ya Saboku wilayani Siha Bwn.Lomnyaki Lukumai amesema shule hiyo imepokea shilingi milioni 47.3 kwa ajili ya vyumba 4 vya madarasa ,Matundu 16 ya vyoo,miundombinu ya maji safi na taka pamoja na mfumo wa kunawa mkono na leather tank

"Tarehe 18julai 2024 shule imepokea milioni 113.6 kupitia mradi wa boost kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 4 na vyoo matundu 6 tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha hizo ambazo zinaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule hii"Amesema Lukumai

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Msingi Msamadi wa wilaya ya Hai Mwl.Bariki Mlay amesema shule hiyo ilipokea Tshs.351,500,000.00 tarehe 18/6/2024 Kwa ajili ya utekelezaji wa mradi  wa BOOST Awamu ya pili 2023/2024

"Fedha hizi zimepokelewa Kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule mpya inayojumuisha ujenzi wa madarasa 7 ya Msingi,choo Cha wanafunzi wa Msingi matundu 14,madarasa 2 ya awali ya mfano na choo Cha matundu 6,uwanja wa michezo Kwa wanafunzi wa Awali na Jengo la Utawala"Amesema Mlay

Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • ZOEZI LA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA MEI 16 HADI MEI 22 2025 KILIMANJARO May 15, 2025
  • MRADI WA BOOST April 01, 2023
  • Angalia Zote

Habari

  • VIJANA NA WANAWAKE MSIKOPE BILA MALENGO

    May 15, 2025
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi kumsindikiza aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya katika safari yake ya mwisho.

    May 13, 2025
  • Mwili wa Hayati Cleopa D. Msuya waagwa katika viwanja vya CD Msuya wilayani Mwanga

    May 12, 2025
  • SERIKALI KUTENGA BILIONI 7 KUTEKELEZA UJENZI WA BARABARA YA MABOGINI - KAHE

    May 04, 2025
  • Angalia Zote

Video

Kujisajili kwenye mfumo wa NeST - Hatua ya Awali
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Watumishi Portal

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na Kufuatilia malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    17 Barabara ya Florida

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: +255 (027) 2754236/7

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa