RC-BABU ATOA AGIZO IFIKAPO JANUARI 11,2025 SHULE ZOTE ZIWE ZIMEKAMILIKA
Baadhi ya wakazi katika wilaya ya Hai na Siha Mkoani Kilimanjaro wameishukuru serikali ya awamu ya Sita kwa kusikia kilio chao cha ubovu wa miundombinu ya Elimu katika maeneo Yao na kuwarahisishia watoto wao kupunguza mwendo mrefu wa kufuata elimu
Wakitoa kauli zao kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema hakika kwa sasa ni faraja kwani ujenzi wa miundombinu hiyo unaendelea na hivyo watoto wao wataondokana na changamoto walizokuwa wanakumbana nazo
Aidha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu ametoa agizo na kuwasisitiza wakuu wa wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kuwa ifikapo 13 Januari 2025 ,Shule hizo zianze kupokea wanafunzi na watoto wote walio chaguliwa kuendelea na masomo waripoti shuleni
"Wanafunzi wote walio chaguliwa kuendelea na masomo natoa agizo wanatakiwa waripoti katika maeneo Yao waliyopangiwa sitaki kusikia sababu yoyote ya mtoto kutoendelea na masomo labda kama ametangulia mbele za haki
Sasa Wakurugenzi natoa maelekezo ikifika tarehe 11 mwezi januari ujenzi madarasa uwe umekamilika ntatuma watu wangu kimyakimya wanipigie picha na kama hamjamaliza tutaelewana vibaya" Amesema Babu
Hata hivyo amewapongeza wananchi katika kuunga mkono ujenzı wa shule hizo ikiwemo uchimbaji msingi
Sambamba na hayo Mkuu wa Shule ya Msingi ya Saboku wilayani Siha Bwn.Lomnyaki Lukumai amesema shule hiyo imepokea shilingi milioni 47.3 kwa ajili ya vyumba 4 vya madarasa ,Matundu 16 ya vyoo,miundombinu ya maji safi na taka pamoja na mfumo wa kunawa mkono na leather tank
"Tarehe 18julai 2024 shule imepokea milioni 113.6 kupitia mradi wa boost kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 4 na vyoo matundu 6 tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha hizo ambazo zinaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule hii"Amesema Lukumai
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Msingi Msamadi wa wilaya ya Hai Mwl.Bariki Mlay amesema shule hiyo ilipokea Tshs.351,500,000.00 tarehe 18/6/2024 Kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa BOOST Awamu ya pili 2023/2024
"Fedha hizi zimepokelewa Kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule mpya inayojumuisha ujenzi wa madarasa 7 ya Msingi,choo Cha wanafunzi wa Msingi matundu 14,madarasa 2 ya awali ya mfano na choo Cha matundu 6,uwanja wa michezo Kwa wanafunzi wa Awali na Jengo la Utawala"Amesema Mlay
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa