Halmashauri Mkoani Kilimanjaro zimepewa mwezi mmoja kuteketeza dawa zilizoisha muda wake.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai aliyasema hayo Wilayani Moshi katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani cha kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mhe. Kagaigai amesema hoja ya dawa kuisha muda wake wamatumizi imejitokeza katika kila Halmashauri hivyo inaonyesha wakati wa ununuzi wa dawa hizo hapakuwa na mipango thabiti, ameendelea kusema vibali na taratibu zote zinazohusika kwa ajili ya kuteketeza dawa hizo zifanyike haraka iwezekanavyo.
'' Halmashauri yoyote ambayo inadawa zilizoisha muda wake taratibu zifanyike dawa hizo ziwe zimeteketezwa, Katibu tawala mkoa naomba ushughulikie suala hilo'' alisema Kagaigai
Aidha, Mhe. Kagaigai amemuelekeza Katibu Tawala Mkoa baada ya mwezi mmoja kuleta taarifa ya Halmashauri ambazo hazitakuwa zimefanya zoezi la uteketezaji wa dawa zilizoisha muda wake.
Vilevile Mhe. Kagaigai ameendelea kuwahimiza Waheshimiwa Madiwan kuwa tayari kusikiliza kero za wananchi wao na kuzitatua kwa wakati kwa kushirikiana na watendaji wa kata zao.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa