Viongozi wa Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro wameelekezwa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali ya awamu ya sita.
Amewataka kutumia mbao za matangazo, mikutano na mitandao ya kijamii na redio za ndani kwa jili ya kufikisha taarofa kwa wananchi wote.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu ameyasema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika Novemba 6, 2023 katika ukumi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Mhe. Babu amezitaka Halmashauri zote pamoja na Mamlaka ya Mapato TRA kuhakikisha wanakusanya mapato ya Serikali kwa kuzingatia sheria na taratibu zaukusanyaji wa mapato pia amezitaka halmashauri za Mkoa kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato wa vyanzo vilovyopo.
Vilevile, Babu amesema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na mvua kubwa zinazoendelea kipindi hichi amewataka Wakuu wa Wilaya kuwasihi wananchi wanaoishi maeneo ya bondeni kuondoka katika maeneo hayo lengo ni kuepuka athari zinazosababishwa na mvua.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda amesema kuwa ushirikiano ulipo kati ya viongozi na wadau ndani ya Mkoa umewezesha watendaji kufanya majukumu yao kwa bidii, na kwa kuzingatia misingi ya Utawala bora, Sera, Sheria, Mikakati, Miongozi pamoja na Mipangokazi.
Akiwasilisha taarifa ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) Eng.Innocent Logodisha amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/23 pamoja na robo ya kwanza kwa mwaka 2023/24 Mamlaka ilifanikiwa Kusimamia na kukamilisha utekelezaji wa Mradi wa Majisafi wa Miwaleni na Ujenzi wa Mtandao wa majitaka “Kata ya Korongoni na Longuo A hatua hizo zimepelekea kuunga jumla ya wateja wapya 3,241 kwenye huduma ya majisafi na wateja wapya 313 wameungwa kwenye mtandao wa majitaka na kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka Shilingi Milioni 970 kwa mwezi na hadi Shilingi Bilioni 1.
Naye Mwakilishi wa NaCONGO Mkoa wa Kilimanjaro Bi.Asifiwe James Malya amesema kwa mwaka 2022/2023 Mkoa umekua Jumla ya Mashirika yaliyohakikiwa 188, Mashirika yanayofanya kazi jumla ni 104 na Mashirika yasiyofanyakazi 84. Aidha, katika utekelezaji wa afua mbalimbali katika sekta ya Ngos jumla ya watu 32,291,751 waliweza kunufaika katika uwezeshwaji kiuchumji, Mazingira pamoja na msaada wa kisheria.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa