Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (MB) nchini,amesema serikali umewekeza Mradi Mkubwa wa kimkakati ambao haujawai kuwepo katika wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
"Mradi huu unahitaji Mafundi wa kurekebisha koki kuingiza maji Kwenye nyumba za watu , Mafundi hao watapata ujuzi kutoka kwenye shule ya ufundi na chuo Cha ufundi" Amesema Mhagama
Ameyasema hayo Januari 7,2025 katika ziara yake alipotembelea na kukagua Mradi wa Afya wilayani Rombo katika kata ya Kalamfua mokala mkoani hapa
Aidha amesema wilaya hiyo imepokea Kwa miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya Sita Bilioni 82 yakuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Afya ,Elimu,Maji ,na Umeme
"Katika wilaya hii tayari tumeanza kujenga chuo Cha veta pamoja na Shule ya ufundi wa Umeme hivyo Mhe.Rais Dakt.Samia suluhu Hassan ameanza kutengeneza ajira Kwa vijana kupitia sekta ya Umeme ili kutatua tatizo la ajira Kwa vijana"
Hata hivyo amesema mpango wa serikali ni kufungamanisha soko la Mamsera na hololo na Miradi mikubwa ambayo Sasa wameamua uletwe, na umwagiliaji kwenye kilimo Cha kisasa Cha ndizi kwenye halmashauri hiyo na katika wilaya ya Rombo
"Vitu hivyo vikifungamanishwa vizuri vitasaidia kuifanya zai la ndizi liwe la kibiashara Zaidi liongeze mapato Kwa wananchi pia na uchumi katika wilaya"Amesema Mhagama
Sambamba na hayo Baadhi ya Wananchi wilayani humo wameishukuru serikali ya awamu ya Sita kwa kuendelea kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya Afya
"Naishukuru serikali ya Rais Samia suluhu Hassan Kwa Yale yote anayoifanya katika wilaya yetu ,ametuletea kituo Cha Afya katika kata yetu ya Kalamfua mokala na ametutengenezea na wodi ya wazazi" Amesema Romania Laswai
"Serikali ya awamu ya Sita imetuletea kituo Cha Afya kwani tulikuwa hatuna kituo Cha Afya Kwa Sasa hivi tunapata huduma nzuri ,tunapokelewa vizuri na wahudumu wa kituo hichi wamama wajawazito wanajifungua salama kwani tumetengenezewa pamoja na wodi ya wazazi"Amesema Efgenia Bimng'anya
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa