RUWASA Wilaya ya Mwanga imeelekezwa kuweka ulinzi madhubuti katika Matanki yote yakufadhia maji pamoja na kutunza miundombinu ya maji.
Ameyasema hayo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Kivisini leo Aprili 7, 2024 wilayani Mwanga.
Ndugu Mzava amesema maji ni muhimu kwa kila kiumbe hai hivyo usalama wa wananchi wanaotumia maji unatakiwa kupewa kipaumbele kwa kuhakikisha maji yanakua salama nyakati zote na kudhibiti uharibifu wa miuondombinu ya maji inayofanywa na wananchi wakorofi.
Aidha, Ndg. Mnzava amependezwa na mchakato wa manunuzi katika mradi huo kufanyika katika mfumo wa NeST hivyo, amewataka Wakurugenzi wote nchini kuwajengea uwezo watumishi wao juu ya matumizi ya mfumo huo pia Kamati ya Ulinzi na Usalama za Wilaya zipatiwe mafunzo kwa lengo la kuwezesha katika ufuatiliaji.
Naye Meneja RUWASA Wilaya ya Mwanga mhandisi Christina Kessy amesema chanzo kikuu cha maji cha mradi huu ni kutoka katika kisima kirefu kilichopo kijiji cha Kivisini chenye uwezo wa kuzalisha lita 27,000 kwa saa.
Ameendelea kusema ujenzi wa mradi huu umehusisha, ujenzi wa tanki la kukusanyia maji lita 75,00, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 22, ujenzi wa birika la kunyweshea mifupo, ununuzi na uwekaji wa pampu mpya, ujenzi wa mtandao wa bomba urefu m. 18.577 km.
Mhandisi Christina amesema mradi umekamilika kwa asilimia mia na unaenda kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji masaa 24 kwa wananchi wapatao 1539 katika vijiji viwili vya
Kwamnyange na Kivisini na umegharamu kiasi cha Tshs. Milioni 553,635,637.00.
Kwa upande wa wananchi wa vijiji hivyo viwili wamesema mradi huo umetatua changamoto walizokuwa wanakabiliana nazo za magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa maji safi na salama hapo awali iliwalazimu kuchota maji katika makorongo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa