Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Bw. Ismail Ali Ussi amesema Serikali kupitia Wizara ya afya imeendelea kuboresha mazingira rafiki kwa watumishi wa afya lengo kutoa huduma bora kwa wanachi.
Ameyasema hayo leo Julai 2,2025 wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika katika hospitali ya wilaya ya Rombo kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya Watumishi hospitalini hapo.
Alisema kuwa, serikali imeendelea kujenga hospitali katika maeneo mbalimbali kwa ngazi tofauti ambapo kwa mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa mikoa ambayo imebarikiwa kupata huduma za afya katika maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa, kukamilika kwa nyumba hizo pamoja na madaktari kuhamia itasaidia wananchi kupatiwa huduma muda wote na kupunguza changamoto ya Afya kwa wananchi.
Aidha amewataka, Madaktari hao ambao wataishi katika nyumba hizo kuhakikisha wanafanya uadilifu na uaminifu katika kutoa huduma kwa wananchi.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo, Dkt. Fortunatus Anthony alisema kuwa, kutokana na umbali na uhaba wa nyumba za Watumishi katika eneo la Hospitali hiyo umepelekea Watumishi kuwa na wakati mgumu kufika hospitali na kutoa huduma kwa wagonjwa kwa wakati.
Dkt. Fortunatus alisema kuwa, serikali ilitoa fedha milioni 120 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Watumishi ya familia mbili kwa moja.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha Watumishi kuishi karibu na eneo la kazi na wananchi kuendelea kupata huduma kwa masaa 24, na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma mbalimbali katika hospitali.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa