Serikali mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imefankiwa kuokoa kiasi cha shilingi 266,551,507 katika kipindi kilichoanzia Januari hadi Mei 2021.
Akiongea wakati wa kuupokea Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Kiliamanjaro Mhe. Stephen Kagaigai amesema mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya serikali na wananchi wa mkoa wa Kilianjaro katika vita dhidi ya rushwa.
Mhe. Kagaigai amefafanua kuwa kiasi chashilingi 218,269,856 zilirejeshwa kwa wahusika na shilingi 48,281,651 zilirejeshwa serikalini.
Aidha Mhe. Kagaigai ameongeza kuwa katika kipindi kilichoanzia mwezi Julai 2020 haadi Aprili 2021 jumla ya taarifa 774 ziliwasilishwa TAKUKURU ambapo baada ya uchunguzi taarifa 46 zimebainika kuwa zinahusiana na rushwa na taarifa 368 zimegundulika hazihusiani na rushwa.
Kuhusu kesi mpya zilizopo mahakamani, Mhe. Kagaigai amesema jumla ya kesi mpya 15 zimefunguliwa huku kesi 12 zikiwa zimeshahuhumiwa ambapo serikali ilishinda kesi 8 na kushindwa kesi 4.
Mwenge wa Uhuru unatajia kutembelea jumla ya miradi 44 katika mkoa wa kilimanjaro kuanzia tarehe 5/06/2021 hadi tarehe 9/06/2021.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa