Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira amesema uhamisho wa aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Lyamungo, Mwalimu Adrian Maro ulilenga kuimarisha utendaji na uwajibikaji katika kusimamia elimu katika na si vinginevyo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dkt. Mghwira amesma uhamisho huo uliotekelezwa na Katibu Tawalawa wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Khatib Kazungu ulizingatia mapendekezo ya tume iliyochunguza malalamiko kutoka kwa baadhi ya waalimu wa shule ya sekondari Lyamungo dhidi ya Mwalimu Adrian Maro .
Miongoni mwa mambo yaliyobainika baada ya uchunguzi wa tume hiyo ni pamoja na uwezo mzuri wa mwalimu Maro katika kusimamia shule ya sekondari Kimochi ya kutwa yenye kidato cha kwanza hadi cha nne jambo ambalo lilipelekea wasimamizi wake wa kazi kumbadlishia majukumu na kumpa kazi ya kusimamia shule ya sekondari Lyamungo ambayo ni ya bweni yenye kidato cha tano na sita.
Aidha Mhe Mghwira alibainisha kuwa tume imegundua uwezo mdogo wa kiutendaji wa Mwalimu Maro katika kusimamia shule ya bweni nyenye kidato cha tano na cha sita hali iliyosababisha wasimimizi wake wa kazi kumpungizia ukubwa wa kazi kwa kumpa usimamizi wa shule ya kutwa kama ya awali.
Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo ambayo yameonesha udhaifu wa kiutendaji kwa Mwalimu Maro ni kufanya teuzi bila kufuata taratibu na miongozo na kutowapa barua waalimu ambao amewateua kwa kuwapa majuku.
Mbali na hilo Mhe. Dkt, Mghwira amesema Mwalimu Maro alishindwa kudhibiti jaribio la mgomo wa wanafunzi lililotokea tarehe 24/02/2020 jambo ambalo ni ishara ya kutomudu nidhamu kwa waanafunzi.
Kuhusu fedha za ukarabati wa shule kongwe unaotekelezwa na serikali ya awamu ya tano, Mhe. Dkt. Mghwira amesema shule ya sekondari Lyamungo si shule pekee iliyopata fedha za utekelezaji wa miradi hiyo katika mkoa wa Kilimanjaro, hivyo basi si sahihi kuhusisha uhamisho wa mkuu wa shule na kuletwa fedha za utekelezaji wa mradi huo.
Amebanisha kuwa tangu mwaka 2017 halmashauri za mkoa wa Kilimanjaro zimekua zikipokea fedha za kukarabati wa shule kongwe ndani ya mkoa.
Mhe. Dkt. Mghwira amefafanua kwamba Halmashauri ya wilaya Same imepokea kiasi cha milioni 91,6927,960 kwa ajili ya ukarabati wa shule ya sekondari Same,
Katika Manispaa ya Moshi shule ya ufundi moshi imepokea Shilingi bilion 2.8 na shule ya sekondari Mawenzi imepokea shilingi milioni 750,332,637. Katika halmashauri ya Moshi shule ya sekondari Langasani ilipokea shilingi milioni 121,600,000, shule ya sekondari Umbwe imepokea shilingi milioni 969,669,148 , shule ya sekondari Ashira imepokea shilingi milioni 851,955,447.50 na shule ya sekondari Weruweru imepokea shilingi milioni 749,179,604.
Katika Halmashauri ya wilaya ya Hai shule ya sekondari Lyamungo imepokea kiasi cha shilingi milioni 799,443,156 kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa muongozo wa matumizi ya fedha hizo uatolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI ) ambao unatakiwa kusimamiwa na mamlaka zote katika usimamizi wa fedha.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa