Mkuu wa Mkoa wa Kimanjaro Mhe. Anna Mghwira amezipiga marufuku halmashauri zote mkoani Kilimanjaro kuwatoza tozo yeyote wafanyabiashara ndogondogo ndani ya mkoa.
Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara katika soko la Hedaru Mhe. Mghwira amesema si sahihi na kinyume na maelekezo ya serikali kuwatoza wafanyabiashara ndogondogo kwani maelekezo ya serikali ni kila mjasiliamali mdogo kuwa na kitambulisho cha mjasilia mali na asitozwe tena .
Mhe. Mghwira amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamesema kuwa mbali na kumiliki vitambulisho vya mjasiliamali wasafirishaji wa mazao wamekuwa wakiwachangisha wafanyabiashara kulipia ushuru wa kuingiza mazao sokoni.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa tozo za ushuru wa kuingiza gari ndani ya soko au kupisha mzigo wa mazao barabarani zinatakiwa kulipwa na msafirishaji na si jukumu la mkulima au mjasiliamali mdogo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa