Baadhi ya wakazi katika wilaya ya Hai na Siha Mkoani Kilimanjaro wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kusikia kilio chao cha ubovu wa miundombinu ya Barabara ya Bomang'ombe -Kikavuchini na kutopitika kwa daraja Manyata nyakati za mvua.
Wakitoa kauli zao kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema hakika kwa sasa ni faraja kwani ujenzi wa miundombinu hiyo unaendelea na hivyo wataondokana na adha waliyokuwa wakiipata.
Wamesema walikuwa wakisafirisha mazao yao kwa shida na wakati mwingine hata watoto walikuwa wakishindwa kwenda shule kutokana na ubovu wa miundombinu uliokuwepo.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Bomang'ombe -Kikavuchini Meneja TARURA wilaya ya Hai Injinia Fransic Kuya amesema ujenzi umeanza Agosti 5,2024 na unatarajiwa kukamilika Agosti 4,2025 ambapo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.8.
Akizungumzia ujenzi wa daraja la Mawe MANYATA, Meneja TARURA wilayani Siha Injinia Protas Kavishe amesema mradi utagharimu kiasi cha shilingi milioni 336.9 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 92 ambapo unatarajiwa kukamilika Januari 15,2025.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu akasisitiza wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa miradi hiyo kukamilisha kwa wakati kwani Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi ili kuhakikisha wananchi wanaondoka na adha wanazozipata katika miundombinu hiyo.
Bodi hiyo ya barabara pia imetembelea ujenzi wa barabara kiwango cha lami ya Getifonga-Mabogini Kahe iliyoko wilayani Moshi yenye urefu wa kilomita 1.2 ambapo ujenzi wake unaendelea.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa