Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kuchukua hatua za tahadhari ili kujikinga na ugonjwa wa CORONA unasababishwa na virusi vya COVID 19.
Akiongea wakati wa kupokea dawa za kutakasa mikono zilizotolewa na kampuni ya Mega Bevarage,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Dkt. Anna Mghwira amewataka wananchi mkoani Kilimanjaro kuhakikisha kuwa wananawa mikono kila wakati kwa maji na sabuni, wanavaa barakoa pamoja na kuepuka mikusanyiko.
Aidha amekumbusha kuwa kila mtu anapofika nyumbani baada ya kutoka katika shughuli zake za kutwa nzima aoge kwa maji na sabuni na abadilishe mavavi kabla ya kuwashika au kuwakaribia watoto na watu wengine ambao wanawakuta nyumbani.
Kwa kufanya hivyo Mhe. Mghwira amesema wataweza kuwalinda watoto na wapendwa wengine ndani ya familia wasipatwe na ugonjwa wa CORONA.
Kwa upande wa ke Meneja wa kampuni ya Mega Bevarage inayotengeneza vinywaji vya K Vant ,Christopher Ndosi amesema wametoa lita 1000 ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na janga la CORONA.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa