• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
      • Trade and Investment
      • Administration and Human Resource Department
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ukaguzi wa Ndani
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

WANANCHI WA KIA KUNUFAIKA NA FIDIA YA BILIONI 11.5

Posted on: May 11th, 2024

Wananchi wa Kaya 1016 wa vijiji vya sanyastation, Tindigani na Chemka Wilayani Hai ambao walivamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuweka makazi kinyume na sheria wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwalipa fidia ya Bilioni 11.5 ambapo wameanza kuvunja makazi yao wenyewe na kupisha eneo hilo.

Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu ilifika katika maeneo hayo na kushuhudia jinsi wananchi wakivunja makazi yao wenyewe ambapo wamemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa busara aliochukua wa kuwalipa ilihali walivamia katika eneo la uwanja.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Babu amesema kuwa wananchi hao walivamia katika eneo hilo la uwanja wa ndge na kujenga makazi lakini kwa sasa linahitajika kwa ajili ya matumizi mengine.

Mhe. Babu emendelea kusema Serikali iliamua kutumia busara kuwalipa wananchi hao fidia ya Bilioni 11.5 kwa wananchi wa Wilaya ya Hai pamoja na Arumeru ili kupisha eneo hilo ambapo waliamua kuvunja nyumba zao wenyewe nakupisha eneo hilo.

“Hakuna mwananchi ambaye ameondoka katika eneo hili bila kulipwa fidia hivyo nawaombeni wananchi mumuonee huruma Rais kuna watu wengi wao kila kinachofanyika na serikali kwao ni kibaya hawataki lakini tambuei Serikali inaubinadamu na utu na inajali haki zote za binadamu na ndio maana zoezi hili tumeshirikishana mwanzo mwisho” alisema Babu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Amir Mkalipa amesema zipo nyumba kadhaa ambazo hazikulipwa fidia kutokana na sababu mbalimbali ambapo wameweza kurekebisha makosa yao na sasa wameshaingiziwa fedha za fidia.

Mkalipa amesema kuwa asilimia 95 ya wananchi wameshahama katika eneo hilo ambapo kwa sasa wanachofanya ni kusafisha eneo hilo kwa kuondoa mapagale baada ya wananchi kuhama wenyewe kwa hiari yao.

“zoezi la kuondoa pagale kwa ufanisi mkubwa na hakuna uharibifu wala uonevu uliofanyika na wala hakuna uharibifu wala uonevu uliofanyika na hakuna nyumba ambayo imevunjwa bali kinachofanyika ni kuvunja mapagale baada ya wananchi kuhama” amesema Mkalipa

Mhe. Mkalipa amesema wananchi walipaswa kuhama katika kijiji cha Sanya stesheni ni kaya 596, kijiji cha Tindigani kaya 402, kijiji cha Chemka kaya 62, ambapo jumla ya kaya 1061 zilizilipwa fidia kwa ajili ya kuhama.

Naye Diwani wa Kata ya KIA Tehera Mollel alisema kuwa kazi ya kuwahamisha wananchi waliovamia katika eneo la uwanja na kuweka makazi ilifanyika kwa uaminifu mkubwa ambapo wananchi wameridhika na fidia waliyopewa.

Amesema huyo mara baada ya kulipwa fidia hiyo wananchi waliamua kuhama wenyewe ambapo kwa sasa lipo greda ambalo hupita na kuvunja magofu yaliyopo katika maeneo hayo kusafisha eneo hilo baada ya wananchi kuhama wenyewe.

“hakuna wananchi wa KIA ambaye amebomolewa nyumba kama inavyoenezwa katika mitandao ya kijamii sisi tumevunja wenyewe nani baada ya kufanyiwa tathimini na kulipwa fidia ambapo tumeweza kwenda kujenga makazi mengine katika maeneo sahihi”alisema Mollel.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Loktol Daud Sokoine alisema kuwa, Serikali ilifanya tathimini awali na hakuna mtu yeyote aliyeachwa na baada ya tathimini hiyo serikali imelipa fidia ambapo imewawezesha wananchi kujenga nyumba katika maeneo mengine.

“ikiwa eneo si la kwako na umevamia na kujenga makazi kwamujibu wa taratibu kama hili la Serikali lakini bado ikaona ipo haja ya kutulipa fidia hili ni jambo la kiungwana na la kupongeza sana ikiwa umeingia kwa mtu bila utaratibu akaja akakuondoa nab ado akakupa nauli ni jambo la kushukuru” alisema Sokoine

Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • ZOEZI LA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA MEI 16 HADI MEI 22 2025 KILIMANJARO May 15, 2025
  • MRADI WA BOOST April 01, 2023
  • Angalia Zote

Habari

  • VIJANA NA WANAWAKE MSIKOPE BILA MALENGO

    May 15, 2025
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi kumsindikiza aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya katika safari yake ya mwisho.

    May 13, 2025
  • Mwili wa Hayati Cleopa D. Msuya waagwa katika viwanja vya CD Msuya wilayani Mwanga

    May 12, 2025
  • SERIKALI KUTENGA BILIONI 7 KUTEKELEZA UJENZI WA BARABARA YA MABOGINI - KAHE

    May 04, 2025
  • Angalia Zote

Video

Kujisajili kwenye mfumo wa NeST - Hatua ya Awali
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Watumishi Portal

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na Kufuatilia malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    17 Barabara ya Florida

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: +255 (027) 2754236/7

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa