Wanaume Mkoani Kilimanjaro wamepongezwa kwa kuitikia wito wa kampeni ya Furaha Yangu na kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya upimaji wa virusi vya UKIMWI.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira wakati wa kuzindua rasmi kampeni hiyo kimkoa ulifanyika katika viwanja vya Shree Hindu Mandal mjini Moshi.
Mhe. Mghwira amesema kuwa kumekuwa na tafsiri potofu kwa wanaume wengi kutegemea majibu ya vipimo vya afya za wenzi wao kuyachukulia kama ndiyo hali zao jambo ambalo amesema kiafya ni hatari kwa ustawi wa mtu binafsi, familia na taifa kwa ujumla.
Ili kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wote wa afya katika vita dhidi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Mhe. Mghwira amesema kila mtu anawajibu wa kupima afya yake ili aweze kujitambua na hatimaye aweze kuishi akiwa anaijua hali yake ya maambukizi.
Aidha Mhe. Mghwira amewataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upimaji lilioanza tarehe 10/09/2018 na kuishia tarehe 16/09/2018.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa kampeni hiyo kwa kipindi cha siku tatu kuanzia tarehe 10/09/2018 hadi tarehe 13/09/2018, mratibu wa masuala ya UKIMWI katika mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Eligy Mosile amesema jumla ya watu 1369 wamejitokeza kupima virusi vya UKIMWI ambapo kati yao wanaume kakiwa 905 sawa na asilimia 66 na wanawake 464 sawa na asilimia 34.
Katika taarifa hiyo Dkt. Mosile amesema watu11sawa na silimia 0.8 wamegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo kati yao wanaume walikuwa 6 sawa na asilimia 0.7 na wanawake 5 sawa na asilimia 1.1
Uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu, Pima, Jitambue, Ishi kimkoa ni mwendelezo wa kampeni iliyozinduliwa rasmi na Mhe. Kassim Majaliwa Waziri, Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa